Wednesday 2 September 2009

Ranieri ateuliwa Meneja Roma huko Italia!
Meneja wa zamani wa Chelsea Claudio Ranieri, miaka 57, ameteuliwa kuwa Bosi mpya wa AS Roma ambayo iko Serie A huko Italia kuchukua nafasi ya Luciano Spalletti aliejiuzulu Jumanne iliyopita.
Spalletti alichukua hatamu hapo AS Roma mwaka 2005 na kuiwezesha kushinda Kombe la Italia na kushika nafasi ya pili Serie A mwaka 2007 na 2008 lakini msimu uliopita walimaliza nafasi ya 6 na hivyo kukosa kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE na badala yake wako EUROPA LIGI.
Msimu huu katika mechi 2 za Ligi, Roma imefungwa zote na hilo likamfanya Spalletti ang’atuke.
Ranieri aliiongoza Chelsea kati ya mwaka 2000 na 2004 na hivi karibuni alikuwa Juventus lakini akatimuliwa mwezi Mei baada ya Timu hiyo kucheza mechi 7 mfululizo bila ushindi.
UEFA yamfungia Eduardo mechi 2!!
Mshambuliaji wa Arsenal Eduardo amefungiwa mechi 2 na UEFA kwa kujidondosha makusudi kwenye mechi na Celtic na hivyo kumhadaa Refa ili apate penalti aliyoifungia Arsenal bao la kwanza katika ushindi wa 3-1 kwenye mechi ya mtoano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Eduardo atazikosa mechi za Arsenal dhidi ya Standard Liege na Olympiakos za Makundi UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Arsenal wamepewa siku 3 kuikatia rufaa adhabu hiyo.
Wadhamini FA Cup kujitoa!!
FA, Chama cha Soka England, kimetangaza Mdhamini wa Kombe la FA, E.On, hataongeza mkataba ukiisha mwaka 2010.
E.On walikuwa na mkataba na FA wa miaka minne uliokuwa na thamani ya zaidi ya Pauni Milioni 32.
Mchezaji akatwa mguu baada ya kupigwa Radi kwenye mechi!!
Mchezaji wa Klabu ya FC Nordsjaelland ya Denmark, Jonathan Richter, amelazimika kukatwa mguu hospitali wiki 6 baada ya kupigwa na Radi akiwa uwanjani akiichezea Timu yake iliyokuwa ikicheza mechi ya kirafiki na Hvidovre.
Madaktari walisema mguu wake uliharibika vibaya na kulikuwa hamna njia ila kuukata ili kumwokoa.

No comments:

Powered By Blogger