Saturday, 6 February 2010

Man United kidedea, ipo kileleni!!
Manchester United wakiwa nyumbani Old Trafford leo wameitandika Timu iliyo mkiani Portsmouth kwa mabao 5-0 na kuchukua uongozi wa Ligi Kuu kutoka kwa Chelsea ambao kesho wana kibarua mahsusi watakapoivaa Arsenal huko Stamford Bridge.
Ili kutwaa tena uongozi wa Ligi kesho lazima Chelsea aifunge Arsenal kwani Manchester United sasa ana pointi 56 na tofauti ya magoli ni 41 na Chelsea ana pointi 55 na tofauti yao ya magoli ni 38 na hivyo akitoka sare na Arsenal, Chelsea atakuwa pointi sawa na Man United lakini Manu United watakuwa juu kwa ubora wao wa tofauti ya magoli.
Arsenal ni watatu na wana pointi 49.
Katika kisago hicho cha Old Trafford, Wayne Rooney ndie aliefungua mafuriko pale alipofunga bao dakika ya 40 kufuatia kona fupi ya Nani kumpa Fletcher alietia majalo tamu na Rooney akamaliza kwa kichwa.
Dakika 1 kabla ya mapumziko kizaazaa cha Nani kikazalisha bao la pili baada ya Beki Vanden Borre kujifunga mwenyewe.
Kipindi cha pili bao zikaongezwa kupitia Michael Carrick ambae kigongo chake kilimbabatiza Hughes wa Portsmouth na kutinga. Berbatov akapachika bao la 4 baada ya kuonyesha utaalam wa hali ya juu na bao la 5 Portsmouth walijifunga wenyewe baada ya krosi kuingizwa wavuni na Beki Wilson.
Vikosi vilivyoanza:
Man Utd: Van der Sar, Neville, Brown, Jonathan Evans, Evra, Valencia, Carrick, Fletcher, Nani, Berbatov, Rooney.
Akiba: Kuszczak, Owen, Park, Fabio Da Silva, Gibson, De Laet, Diouf.
Portsmouth: James, Vanden Borre, Rocha, Wilson, Ben-Haim, Webber, Hughes, Mullins, O'Hara, Belhadj, Piquionne.
Akiba: Ashdown, Owusu-Abeyie, Finnan, Boateng, Dindane, Yebda, Basinas.
Refa: Lee Mason
MATOKEO MECHI ZA Jumamosi, Februari 6
Liverpool 1 v Everton 0
Bolton 0 v Fulham 0
Burnley 2 v West Ham 1
Hull 2 v Man City 1
Man Utd 5 v Portsmouth 0
Stoke 3 v Blackburn 0
Sunderland 1 v Wigan 1
[MECHI INAANZA saa 2 na nusu usiku saa za bongo]
Tottenham v Aston Villa
Liverpool 1 Everton 0
Dirk Kuyt aliipa ushindi Liverpool alipopachika bao kwa kichwa kufuatia kona dakika ya 55 katika Dabi ya Jiji la Liverpool iliyoisha huku kila Timu ina Mtu 10 baada ya Kyrgiakos wa Liverpool na Pienaar kupewa Kadi Nyekundu katika nyakati tofauti.
Mechi hii ilitawaliwa na rafu nyingi na Refa Martin Atkinson alitembeza Kadi nyingi za Njano.
Vikosi vilivyoanza:
Liverpool: Reina, Carragher, Kyrgiakos, Agger, Insua, Mascherano, Lucas, Kuyt, Gerrard, Maxi, Ngog.
Akiba: Cavalieri, Aquilani, Riera, Aurelio, Babel, Degen, Skrtel.
Everton: Howard, Neville, Distin, Heitinga, Baines, Fellaini, Donovan, Osman, Cahill, Pienaar, Saha.
Akiba: Nash, Bilyaletdinov, Arteta, Yakubu, Senderos, Anichebe, Coleman.
Refa: Martin Atkinson
Saha na ulaji mpya Everton!!
Fowadi wa Everton Louis Saha, miaka 31, amesaini mkataba mpya wa miaka miwili na Klabu yake na hivyo kuondoa utata kuwa anaondoka.
Saha alijiunga na Everton mwaka 2008 akitokea Manchester United na msimu huu amekuwa moto mkali kwa kufunga mabao na mpaka sasa ana mabao 13.
Ilidaiwa kuwa Klabu za Bordeaux ya Ufaransa, Besiktas yaa Uturuki na AS Roma ya Italy zilikuwa zikimuwinda.
Hargreaves kurudi kutetea Ubingwa
Sir Alex Ferguson amesema Owen Hargreaves anaweza kucheza mechi za baadae za Ligi Kuu ingawa bado mpaka sasa haijajulikana lini atakuwa fiti kabisa kucheza.
Hargreaves hajacheza tangu Septemba 2008 na baada ya hapo akafanyiwa upasuaji katika magoti yake yote mawili yaliyokuwa na maumivu.
Hargreaves hakuingizwa kwenye Kikosi cha Wachezaji 25 cha Man United kilichosajiliwa UEFA kwa ajili ya mechi za Mtoano za UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Ferguson amesema: “Owen atarudi tu. Anaweza kucheza Ligi na kutusaidia sana. Ligi ina mechi nyingi kupita UEFA na sihitaji kumsajili kwa ajili ya Ligi.”
LIGI KUU: Rooney na Moyes ndio Bora Januari!!
Straika wa Manchester United Wayne Rooney ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Januari na David Moyes wa Everton ameipata kwa upande wa Mameneja.
Rooney kwa mwezi Januari ameifungia Man United mabao 6 na sasa ndie anaeongoza kwa ufungaji akiwa na mabao 20.
Hii ni mara yake ya 5 kushinda Tuzo hii.
Meneja wa Everton, David Moyes, amepewa Tuzo ya Meneja Bora kwa Januari baada ya kuiongoza Timu yake kupata ushindi mara 3 na sare moja.
Hii ni mara yake ya 6 kuipata Tuzo hii.
Tuzo hii ya Ubora wa kila mwezi hutolewa na Barclays ambao ndio Wadhamini Wakuu wa Ligi Kuu na uchaguzi wa nani bora hufanywa na Jopo lenye Wawakilishi kutoka FA, Vyombo vya Habari, Mashabiki na Wadau mbalimbali.
Wenger ageuka Sungura Mjanja!!!
• Adai kumaliza Ligi nafasi ya 3 ni bora kuliko kubeba FA au Carling Cup!!!
Meneja wa Arsenal, Arsène Wenger, amedai kumaliza Ligi Kuu ukiwa nafasi ya 3 ni kitu bora zaidi kuliko kunyakua Makombe ya FA na Carling.
Wenger ametamka: “Ukishinda Carling Cup kwangu huniambii umeshinda kitu! Kufanya vizuri kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE ni muhimu kuliko kuchukua Carling au FA! Sisi kwa mara ya 10 mfululizo tumefuzu kuingia hatua ya Mtoano ya UEFA!”
Kwa mara ya mwisho Arsenal ilitwaa taji lolote ni mwaka 2005 pale iliponyakua Kombe la FA na tangu wakati huo haijaambua kitu.
Msimu huu, Arsenal imeshatupwa nje ya Makombe ya FA na Carling na kwenye Ligi Kuu ipo nafasi ya 3 nyuma ya Chelsea na Manchester United lakini bado imo kwenye kinyang’anyiro cha UEFA CHAMPIONS LEAGUE na itacheza na FC Porto kwenye mechi za mtoano baadae mwezi huu.
Wenger alipoulizwa swali kama kumaliza Ligi wakiwa nafasi ya 3 ni bora kuliko kuchukua Vikombe vya FA na Carling, alijibu: “Tupo hapa kushinda Vikombe lakini inategemea ni Vikombe vipi. Ni Ubingwa wa Ulaya, Ligi Kuu, Carling au FA? Sisi tumeingia hatua ya Mtoano ya UEFA mara 10 mfululizo na hilo ni gumu kuliko kuchukua Vikombe vya FA na Carling!”
Kuhusu kumaliza nafasi ya 3 kwenye Ligi, Wenger amesema hata hilo ni mafanikio makubwa kwani utakuwa umezipiku Timu ngumu kama Manchester City, Liverpool, Tottenham na Aston Villa.
Matamshi hayo ya Wenger yatawastua Wadau wengi wa Arsenal ambao wamebaki kwa muda mrefu sasa bila Kikombe chochote na wale wrevu watamwona sasa wenger amegeuka Sungura aliekosa kuzitungua Zabibu mbivu na badala yake kuziita mbichi.
Hata hivyo, mwenyewe Wenger hajakata tamaa kuhusu Ligi Kuu na kama vile alivyoichukulia mechi na Manchester United Jumapili iliyokwisha, mechi ya kesho na Chelsea ambayo imebatizwa Bigi Mechi, yeye haioni kama ndio itaamua kitu kwenye Ligi Kuu.
Wenger anaelezea: “Baada ya kucheza na Man United na Chelsea, hatuchezi tena nao! Kuwa nyuma yao pointi 6 sio maafa! Tulikuwa pointi 11 nyuma ya Chelsea mwishoni mwa November, kwa nini tukate tamaa tukiwa nyuma pointi 9 kesho?”
KOMBE LA DUNIA: Marefa 30 wateuliwa kwa Fainali!!
• Refa wa ‘Mkono wa Thierry Henry’ yumo!!!
Marefa 30 kutoka kila pembe ya Dunia wameteuliwa na FIFA ili kuwa waamuzi kwenye Fainalli za Kombe la Dunia zitakazochezwa Afrika ya Kuni kuanzia Juni 11 hadi Julai 11.
Mabara ambayo wanatoka Marefa hao 30 ni 10 kutoka Ulaya, 6 kutoka Marekani ya Kusini. Afrika, Asia na Nchi za Carribean, Marekani ya Kati na Kaskazini zimetoa Marefa wanne kila mmoja. New Zealand imetoa Marefa wawili.
Kila Refa atakuwa na Wasaidizi wake, yaani Washika Vibendera, ambao wamekuwa wakifanya nae kazi kwa ukaribu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kwa Nchi zilizoendelea ni wenzake toka Nchi moja.
Katika Marefa hao 30, Refa kutoka Ligi Kuu England ni Howard Webb akisaidiwa na Darren Cann na Michael Mullarkey.
Refa kutoka Sweden, Martin Hansson, alieleta mzozo mkubwa kwenye mechi ya marudiano ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Ufaransa na Ireland aliposhindwa kumuona Thierry Henry wa Ufaransa akiukontroli mpira kwa mkono na kumpasia mwenzake Gallas alieisawazishia Ufaransa na kuwa bao 1-1 katika muda wa nyongeza na hivyo kuipeleka Ufaransa Fainali Kombe la Dunia, yumo kwenye listi hiyo ya Marefa 30.
Marefa kutoka Afrika ni Mohammed Benouza kutoka Algeria, Koman Coulibaly kutoka Mali, Jerome Damon kutoka Afrika Kusini na Eddy Allen Maillet kutoka Seychelles.
TATHMINI MECHI ZA WIKIENDI LIGI KUU:
Gumzo na hamu kubwa ya Wadau wengi, bila shaka, wikiendi hii italenga Dabi ya Liverpool ya Jumamosi inayowakutanisha Wapinzani wa Jadi Liverpool v Everton Uwanjani Anfield na ile Bigi Mechi itakayochezwa Stamford Bridge kati ya Chelsea na Arsenal.
Kwingineko katika wikiendi hii ambayo Timu zote 20 za Ligi Kuu zimo dimbani tutashuhudia Timu iliyo mkiani na ambayo ipo kwenye majaribu makubwa ya matatizo ya fedha yakichanganyika na Wamiliki kubadilika kila kukicha na pia ripoti za Meneja kukutwa kwenye danguro, Timu ya Portsmouth, ikiingia kwenye mdomo wa simba pale itakaposhuka Old Trafford kupambana na Bingwa Manchester United.
Pia kuna mechi tamu kati ya Tottenham na Aston Villa mechi inayozikutanisha Timu zinazogombea nafasi ya 4 ambayo ni muhimu kwa kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao.
Saa ni za Bongo.
JUMAMOSI, FEBRUARI 6
Liverpool v Everton [Anfield, saa 9 dak 45 mchana]
Wikiendi ya Ligi Kuu itafunguliwa rasmi Jumamosi kwa pambano la saa 9 dakika 45 mchana la Mahasimu Liverpool na Everton.
Everton, wakiwa chini ya Meneja David Moyes, hawajafungwa katika mechi 9 za Ligi na wameshinda mechi 4 katika 5 zao za mwisho. Mara ya mwisho Everton kufungwa kwenye Ligi ilikuwa ni Novemba walipofungwa na Liverpool 2-0.
Liverpool wapo pointi 9 mbele ya Everton na fomu yao kwenye Ligi imekuwa haitabiriki na hilo litalifanya pambano hili kuwa tamu.
Everton huenda ikwachezesha Mikael Arteta, aliekuwa majeruhi muda mrefu, na Joseph Yobo, aliekuwa Angola na Nigeria kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika. Lakini Everton itawakosa majeruhi Tony Hibbert na Phil Jagielka.
Liverpool itawakosa majeruhi Fernando Torres, Yossi Benayoun na Glen Johnson.
Vikosi vinategemewa kuwa:
Liverpool (4-2-3-1): Reina; Carragher, Skrtel, Kyrgiakos, Insua; Aquilani, Mascherano; Kuyt, Gerrard, Riera; Ngog.
Everton (4-4-1-1): Howard; Neville, Heitinga, Senderos, Baines; Donovan, Fellaini, Osman, Pienaar; Cahill; Saha.
Refa: Martin Atkinson
Manchester United v Portsmouth [Old Trafford, saa 12 jioni]
Huko Old Trafford, Manchester United wakitoka freshi kwenye ushindi mnono walioupata Emirates walipoichabanga Arsenal 3-1 wana nafasi kubwa ya kuwa kileleni mwa Ligi Kuu ikiwa wataifunga Portsmouth Timu iliyo mkiani kwa sababu Chelsea wanaoongoza Ligi kwa pointi mbili wanacheza Jumapili.
Man United itakuwa bila ya Rio Ferdinand anaetumikia kifungo cha mechi 4 hii ikiwa ni mechi yake ya pili. Pia majeruhi Owen Hargreaves, Nemanja Vidic na John O’Shea hawatakuwepo.
Portsmouth watawakosa Michael Brown na Papa Bouba Diop walioumia lakini Mchezaji mpya Riccardo Rocha huenda akacheza.
Vikosi vinategemewa:
Manchester United (4-3-3): Van der Sar; Fabio, Evans, Brown, Evra; Scholes, Carrick, Fletcher; Nani, Rooney, Park.
Portsmouth (4-3-3): James; Finnan, Ben-Haim, Rocha, Belhadj; Yebda, Basinas, Boateng, O’Hara; Dindane, Piquionne.
Refa: Lee Mason.
Hull City v Manchester City [KC Stadium, saa 12 jioni]
Baada ya kuisimamisha Chelsea hapo juzi Uwanja huo huo wao wa KC, Hull City watategemea matokeo mazuri tena watakapoivaa Manchester City.
Hull City wako nafasi ya 18 wakifungana na Timu nyingine tatu wote wakiwa na pointi 21 na chochote watakachopata kitawasaidia kujinasua toka chini.
Sunderland v Wigan Athletic [Stadium of Light, saa 12 jioni]
Ni mechi ya Timu zilizo kwenye kipindi cha matokeo mabovu kwao. Timu hizi mbili, kati yao, zimecheza jumla ya mechi 18 na kushinda moja tu.
Sunderland wako nafasi ya 13 wakiwa pointi mbili juu ya Wigan.
Bolton Wanderers v Fulham [Reebok Stadium, saa 12 jioni]
Baada ya vipigo vitano mfululizo, Fulham walishinda hapo juzi walipoipiga Portsmouth 1-0 huo ukiwa ushindi wao wa kwanza tangu walipoifunga Man United mapema Desemba mwaka jana.
Bolton wako nafasi ya 16 wakiwa na pointi 21 na matokeo yao kwa mechi za nyumbani si mazuri sana kwani wameshinda mechi 3 kati ya 12 walizocheza Reebok.
Burnley v West Ham [Turf Moor, saa 12 jioni]
Burnley wako nafasi ya 19 ikiwa ni juu tu ya Portsmouth walio mkiani lakini wako pointi moja tu nyuma ya wapinzani wao West Ham walio nafasi ya 15 na takwimu hizi zinaonyesha vita ilivyo kali kwa Timu za chini zinazopigana kujinusuru kushuka Daraja.
Hii ni Bigi Mechi kwa Timu hizi mbili katika vita hiyo.
West Ham, chini ya Meneja Gianfranco Zola, wameimarisha Kikosi chao katika dirisha la uhamisho la Januari na sasa wana Mastraika watatu wapya ambao huenda wakashushwa uwanjani.
Nao ni Mido, Benni McCarthy na Ilan.
Burnley wako chini ya Meneja mpya Brian Laws na hii ni mechi yake ya 4 tangu ashike wadhifa huo na zote 4 wamefungwa.
Ni mechi muhimu sana kwake.
Stoke City v Blackburn Rovers [Britannia, saa 12 jioni]
Timu hizi mbili zimeibuka upya katika mechi zao za mwisho na hazijafungwa katika mechi 3 za mwisho. Blackburn wako nafasi ya 11 wakiwa na pointi 28 na Stoke wako nafasi ya 12 na wana pointi 26.
Tottenham v Aston Villa [White Hart Lane, saa 2.30 usiku]
Pambano jingine tamu la Jumamosi ni lile la Timu mbili zinazowania nafasi ya 4, Tottenham v Aston Villa. Timu hizi zilikutana mwezi Novemba na kutoka suluhu. Kwa sasa Tottenham ndio wanaoshikilia nafasi ya 5 lakini Villa wako pointi 2 nyuma huku wana mechi moja mkononi.
JUMAPILI, FEBRUARI 7
Birmingham v Wolverhamton Wanderers [Molineux, saa 10.30]
Hii ni mechi ya kwanza ya Jumapili kabla ya ile Bigi Mechi Chelsea v Arsenal.
Hii ni mechi kati ya Timu zenye takwimu tofauti kabisa.
Birmingham wako nafasi ya 8 wakiwa na pointi 34 na wamefungwa mechi moja tu kati ya 14 walizocheza mwisho lakini kati ya hizo 14 wameshinda moja tu.
Wolves wako nafasi ya 17 na wana pointi 21.
Chelsea v Arsenal [Stamford Bridge, saa 1 usiku]
Pambano hili la Stanford Bridge ambalo limebatizwa 'Bigi Mechi' limegubikwa na kashfa ya Nahodha wa Chelsea John Terry ambae tayari ameshatimuliwa kama Nahodha wa England hapo jana.
Hata hivyo hili ni pambano muhimu kwani linakutanisha Timu iliyo nafasi ya kwanza na ya 3 huku Manchester United akitishia kuwapiku na kuchukua nafasi ya juu na pengine huenda akaipata kwani wakati mechi hii inachezwa Jumapili, Man United anacheza Jumamosi na akiifunga Portsmouth atakwea kilele na atabaki huko ikiwa Arsenal itaifunga Chelsea.
Kwa Arsenal, huu ni wakati mgumu na hili ni pambano gumu na la muhimu sana kwani mechi mbili za nyuma ya hii walitoka sare na Aston Villa na wakafungwa na Man United. Leo wako na Chelsea na Jumatano Liverpool iko mbele yao.
Hakika, ni wakati mgumu mno kwa The Gunners.
Chelsea watacheza bila ya majeruhi Juliano Belletti na Michael Essien lakini wale Cole wawili, Ashley Cole na Joe Cole, walioanza benchi mechi ya juzi na Hull City, huenda wakaanza mechi hii.
Arsenal bado itawakosa majeruhi wao Van Persie, Eduardo na Abou Diaby lakini huenda Nicklas Bendtner akashiriki.
Takwimu muhimu sana kwa Wadau wa mechi hii ni ile ya Refa atakaechezesha.
Refa Mike Dean katika mechi 16 za Ligi Kuu alizochezesha ametoa penalti 11.
Vikosi vinategemewa:
Chelsea (4-3-1-2): Cech; Ivanovic, Carvalho, Terry, A Cole; Kalou, Lampard, J Cole; Ballack; Anelka, Drogba.
Arsenal (4-3-3): Almunia; Sagna, Gallas, Vermaelen, Clichy; Fabregas, Song, Denilson; Nasri, Bendtner, Arshavin.
Refa: Mike Dean

Friday, 5 February 2010

MENEJA WA POMPEY DANGURONI: Mke amtetea kazi ngumu humfanya ahitaji kukandwa!!!
Mke wa Avram Grant, Meneja wa Portsmouth aliekutwa anatoka kwenye danguro, amemtetea Mumewe kwa kudai anahitaji kukandwa na kuchuliwa kwa sababu anafanya kazi ngumu mno ya kuiongoza Portsmouth ambayo ni Timu uchwara.
Mke huyo wa Grant, aitwae Tzofit Grant ni Mtangazaji wa TV maarufu na mwenye vituko huko kwao Israel, amesisitiza kuwa hajakasirika kwa Mume wake kwenda kukandwa na akaongeza kuwa yuko huru kufanya anachotaka kwa mwili wake.
Bibi huyo aliongeza kuwa ni yeye ndie anaemsistiza kwenda kukandwa na kuchuliwa.
Mama Grant, mwenye umri wa miaka 45, amesema: “Sielewi kwa nini habari hizi zimeleta msisimko. Avram anapenda kukandwa! Mie sijakasirika! Yeye ni Meneja wa Portsmouth. Hivi mnajua kazi hiyo ilivyo ngumu? Yeye ni Meneja mzuri sana kwenye Timu uchwara! Anafanya kazi ngumu sana, anahitaji kukandwa mara mbili kwa siku na tena toka kwa Wanawake wawili na si mmoja!”
Portsmouth wako mkiani kwenye Ligi Kuu na wana matatizo makubwa kifedha yaliyosababisha Klabu hiyo kubadilisha Wamiliki wanne katika msimu huu na pia Wachezaji kucheleweshewa Mishahara yao.
Mke huyo wa Grant ambae husifika kwa vituko vya ajabu kwenye kipindi chake cha TV kikiwemo kunywa mkojo wake kwenye programu laivu na kukoga chokoleti ya majimaji aliongeza na kusema Mumewe alimpigia simu na kumwambia sasa jina lake limetajwa kwamba kaenda danguro na yeye akacheka sana.
Mama huyo akahoji: “Yeye alikwenda kukandwa. Hakuna mtu aliethibitisha hapo ni danguro. Hebu tuwe wakweli, nani anaweza kwenda danguroni mchana kweupe huku kavaa magwanda ya Timu ya Portsmouth wakati akijijua yeye ni mtu maarufu?”
Klabu ya Portsmouth imethibitisha kuwa hawana ishu na Grant kuhusu matembezi hayo kwenye danguro kwani suala hilo haliingiliani na kazi yake.
Terry avuliwa Unahodha England!!
John Terry amevuliwa Unahodha wa Timu ya Taifa ya England kufuatia kufumuka kwa skandali kuwa alitembea na gelfrendi wa Mchezaji mwenzake wa Chelsea wakati huo na England, Wayne Bridge.
Terry, miaka 29, leo alikuwa na mazungumzo na Meneja wa England Fabio Capello kuhusu kashfa hiyo.
Taarifa ya Capello iliyosambazwa imesema kuwa baada ya kutafakari kwa undani ni bora kumvua Unahodha Terry.
Mwenyewe Terry amesema kuwa anauheshimu uamuzi wa Capello na yuko tayari siku zote kujitolea kwa moyo wote kuisaidia Timu ya England.
Taarifa hiyo ya Capello haikutaja nani atachukua wadhifa huo ingawa iligusia kuwa Terry alipochaguliwa Nahodha pia aliteuliwa Makamu Nahodha ambae ni Rio Ferdinand na uamuzi huo haubadiliki.
Terry, mwenye umri wa miaka 29, aliteuliwa kuwa Nahodha mwaka 2008 na kulikuwa na kila dalili yeye ndie ataiongoza England kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi Juni.
Terry, ambae ana Mke na watoto, alitajwa kwenye Magazeti wiki iliyokwisha mara baada ya amri ya Mahakama ya kutotaja jina kufutwa na vikatoka vilio toka kila upande kwamba hafai tena kuwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya England.
Klabu yake Terry, Chelsea, imetamka kuwa inamsapoti yeye na familia yake na imesema iko tayari kumpa likizo wakati wowote ule akiihitaji ili apunguze presha.
Ferguson aitetea rufaa ya Ferdinand
Katika rufaa ya Rio Ferdinand anayopinga kuongezewa adhabu ya kufungiwa mechi moja zaidi baada ya rufaa yake ya kupinga kufungiwa mechi 3 za awali kutupwa na Jopo la Nidhamu kwa misingi kuwa ilikuwa haina uzito na hivyo kumwongezea kifungo kwa mechi moja zaidi na kuwa jumla mechi 4, Klabu yake Manchester United itamtetea kwa kutoa mfano wa Mchezaji wa Liverpool Javier Mascherano.
Man United inadai Mascherano hakushitakiwa kwa kosa sawasawa na la Ferdinand la kumpiga Jermaine Beckford wa Leeds katika mechi iliyochezwa Septemba bila Refa Alan Wiley kuona lakini Refa huyo alipoonyeshwa video ya tendo hilo alisema asingetoa Kadi Nyekundu.
Bodi ya Rufaa itakaa Februari 12 kujadili rufaa hiyo ya pili ya Ferdinand.
Mpaka sasa Ferdinand ameshaanza kuitumikia adhabu yake na ameshaikosa mechi moja ile ya Ligi Kuu dhidi ya Arsenal na Jumamosi ataikosa nyingine ya Portsmouth ikifuatiwa na ya Aston Villa na mechi ya 4 ambayo inapingwa na Manchester United ni ile na Everton.
Lakini endapo rufaa hii ya pili ya Ferdinand itashindwa basi kuna hatari, kufuatia kanuni zilivyo, kuwa huenda akaongezewa tena adhabu ya kufungiwa mechi moja zaidi kwa kukata rufaa bila misingi na hilo likitokea basi Ferdinand ataikosa Fainali ya Kombe la Carling itakayochezwa Februari 28 dhidi ya Aston Villa.
Sir Alex Ferguson amezungumzia sakata hilo la Ferdinand kwa kusema: “Sisi tuna wasiwasi na hiyo kauli rufaa haina misingi thabiti! Marefa wenye uzoefu mkubwa kwenye Ligi Kuu ni Alan Wiley na Steve Bennett. Wanatakiwa wafuate misingi sawa ya sheria! Kwa Rio, Bennett anasema ni kosa lakini kwa Mascherano Wiley anasema si kosa! Vitendo vya Wachezaji hao wawili ni sawa kabisa! Ukisema rufaa haina misingi kwa jinsi Marefa hao wawili walivyoamua tofauti kwa kosa la aina moja unapingana!”
KWINGINEKO ULAYA: Ratiba ya Wikiendi
SERIE A:
Jumamosi, Februari 6
Livorno v Juventus
Palermo v Parma
Jumapili, Februari 7
Atalanta v Bari
Inter Milan v Cagliari
Lazio v Catania
Bologna v AC Milan
LA LIGA:
Jumamosi, Februari 6
Valencia v Valladoid
Barcelona v Getafe
Real Madrid v Espanyol
Jumapili, Februari 7
Osasuna v Tenerife
Racing Santander v Atletico Madrid
Athletic Bilbao v Xerez
BUNDESLIGA:
Ijumaa, Februari 5
Werder Bremen v Hertha Berlin
Jumamosi, Februari 6
Freiburg v Schalke
Wolfsburg v Bayern Munich
1899 Hoffenheim v Hannover
Bochum v Bayer Leverkusen
Cologne v Hamburg
Nurnberg v Stuttgart
Jumapili, Februari 7
Mainz 05 v Borussia Moenchengladbach
Borussia Dortmund v Eintracht Frankfurt
LIGI KUU: Jumamosi Dabi ya Liverpool, Jumapili Bigi Mechi London!!!
• Liverpool v Everton
• Chelsea v Arsenal
Wikiendi hii kuna jumla ya mechi 10 za Ligi Kuu England lakini gumzo kubwa ni mechi mbili nazo ni lile fungua dimba la Jumamosi Dabi ya Jiji la Liverpool huko Uwanja wa Anfield kati ya Wenyeji Liverpool na Mahasimu wao wakubwa Everton mechi itakayo kuwa ya kwanza kuchezwa hapo saa 9 dakika 45 mchana, bongo taimu.
Jumapili ni hekaheka Jijini London, Uwanjani Stamford Bridge, Chelsea wakiwa nyumbani watawaita Arsenal ambao wmetoka freshi tu toka kwenye kipondo cha mabao 3-1 toka kwa Mabingwa Manchester United.
Mpaka sasa takwimu muhimu za LIGI KUU ni:
MSIMAMO LIGI KUU England:
[Timu zimecheza mechi 24 isipokuwa inapotajwa]
1 Chelsea pointi 55
2 Man Utd pointi 53
3 Arsenal pointi 49
4 Tottenham pointi 42
5 Liverpool pointi 41
6 Manchester City pointi 41 [mechi 22]
7 Aston Villa pointi 40 [mechi 23]
8 Birmingham pointi 34 [mechi 23]
9 Everton pointi 32 [mechi 23]
10 Fulham pointi 30
11 Blackburn pointi 28
12 Stoke pointi 26 [mechi 26]
13 Sunderland pointi 24 [mechi 23]
14 Wigan pointi 22 [mechi 22]
15 West Ham pointi 21 [mechi 23]
16 Bolton pointi 21 [mechi 22]
17 Wolves pointi 21 [mechi 23]
18 Hull pointi 21
19 Burnley pointi 20 [mechi 23]
20 Portsmouth pointi 15 [mechi 23]
WAFUNGAJI BORA:
1 Wayne Rooney 20
2 Jermaine Defoe 15
   Didier Drogba 15
3 Darren Bent 14
4 Carlos Tevez 12
   Fernando Torres 12
   Carlos Tevez 12
5 Louis Saha 11
   Cesc Fabregas 11
6 Gabriel Agbonlahor 10
   Frank Lampard 10
Mancini alia kutompata Mkenya Mariga!!!
Bosi wa Manchester City Roberto Mancini ameuita uamuzi wa kutompa kibali cha kazi Mchezaji kutoka Kenya McDonald Mariga [pichani] na hivyo kumkosesha kuwa Mchezaji wa Klabu yake katika siku ya mwisho ya uhamisho ni wa ‘kuwashangaza mno!’
Mariga ambae alianza kucheza Ulaya huko Sweden na Klabu ya Helsingborgs na kisha kwenda Italia Klabu ya Parma alinyimwa kibali cha kazi kwa kuwa tu Kenya haimo kwenye Nchi 70 bora duniani katika listi ya FIFA.
Mancini amelalama: “Tulikuwa tunawawinda Wachezaji kama watatu hivi lakini Mariga alikuwa ndie chaguo letu la kwanza! Inashangaza, Mariga ni Kijana mzuri tu aliecheza Sweden na Italia kwa miaka 6 sasa na uhusiano wa Kiinchi kati ya Uingereza na Kenya ni mzuri! Sielewi kwanini wamekataa kumpa kibali!”
Inasemekana ishu ya Mariga iliingiliwa kati na hata Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ili kuokoa jahazi dakika za mwisho kwa kuongea na wazito wenzake huko Uingereza lakini hilo halikufua dafu na uhamisho ulishindikana hadi dirisha la uhamisho kufungwa.
Sasa Mariga amehamia kwa Jose Mourinho Klabu ya Inter Milan.
Droo ya UEFA EURO 2012 ni Jumapili!!!
Mabingwa Watetezi Spain ni miongoni mwa Nchi 9 zilizoteuliwa kuwemo kwenye Kapu la Kwanza la Miamba, na hivyo kuzitenganisha Nchi kubwa kutokutana katika mechi za awali za mtoano, katika droo ya kupanga Makundi ya raundi za mtoano za UEFA EURO 2012 Mashindano ambayo yanashirikisha Mataifa ya Ulaya.
Droo hiyo inafanyika Jumapili Februari 7 huko Mjini Warsaw, Poland.
Fainali za UEFA EURO 2012 zitafanyika katika Nchi mbili, Poland na Ukraine kwa pamoja, na itashirikisha jumla ya Nchi 16.
Wenyeji Poland na Ukraine wameingizwa Fainali moja kwa moja.
Katika droo hiyo Timu zimegawanywa katika Makapu 6 na zitapangwa katika Makundi 9 kugombea nafasi 14 za kuingia Fainali kujumuika na Poland na Ukraine.
Washindi wa kila Kundi pamoja na Timu moja iliyo nafasi ya Pili yenye matokeo bora kuliko wengine zitaingia Fainali. Washindi wa pili wengine wanane watapangiwa mechi nyngine maalum za mtoano ili kupata Timu za mwisho 4.
Mechi katika Makundi, zikichezwa kwa mtindo wa Ligi wa nyumbani na ugenini, zitachezwa kati ya Septemba, 2010 na Oktoba, 2011.
KAPU 1: Spain (Mabingwa Watetezi), Germany, Netherlands, Italy, England, Croatia, Portugal, France, Russia
KAPU 2: Greece, Czech Republic, Sweden, Switzerland, Serbia, Turkey, Denmark, Slovakia, Romania
KAPU 3: Israel, Bulgaria, Finland, Norway, Republic of Ireland, Scotland, Northern Ireland, Austria, Bosnia-Herzegovina
KAPU 4: Slovenia, Latvia, Hungary, Lithuania, Belarus, Belgium, Wales, FYR Macedonia, Cyprus
KAPU 5: Montenegro, Albania, Estonia, Georgia, Moldova, Iceland, Armenia, Kazakhstan, Liechtenstein
KAPU 6: Azerbaijan, Luxembourg, Malta, Faroe Islands, Andorra, San Marino
Mahakama yaifutia Chelsea adhabu ya kutosajili Wachezaji!!
Mahakama ya Usuluhishi katika Michezo [CAS=Court of Arbitration for Sports] imeondoa kizuizi kilichowekwa na FIFA kwa Chelsea kutosajili Wachezaji hadi mwaka 2011 kufuatia kupatikana na hatia ya kumrubuni na kumchukua Mchezaji chipukizi Gael Kakuta kutoka Klabu ya Ufaransa Lens mwaka 2007 kinyume cha taratibu.
Mwaka jana, FIFA iliifungia Chelsea kutosajili kwa vipindi viwili vya usajili pamoja na kuitaka iilipe fidia Lens.
Gael Kakuta alifungiwa miezi minne na kutakiwa kuilipa Lens kwa kumgharamia.
Chelsea ikakata rufaa CAS na hivyo adhabu zake zikasimama hadi uamuzi wa Mahakama hiyo ulipotakiwa kutolewa na hili lilimruhusu Gael Kakuta kuichezea mechi moja Chelsea kwenye Ligi Kuu mwezi Novemba dhidi ya Wolves.
CAS imeondoa adhabu kwa Chelsea baada ya Klabu hizo mbili, Chelsea na Lens, kufikia makubaliano nje ya Mahakama ambayo inasadikiwa ni pamoja na Chelsea kuilipa fedha Lens.
Uamuzi huu unamaanisha kuwa Chelsea wako huru kusajili Wachezaji dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwishoni mwa msimu huu mwezi Juni.

Thursday, 4 February 2010

Hargreaves nje UEFA!!
Owen Hargreaves hayumo kwenye Kikosi cha Wachezaji 25 cha Manchester United kilichosajiliwa UEFA ili kucheza hatua ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ambayo Man United watacheza na AC Milan kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na mshindi anaingia Robo Fainali.
Hargreaves, miaka 29, hajaonekana uwanjani tangu tarehe 21 Septemba 2008 na baada ya hapo alifanyiwa operesheni ya magoti yake yote mawili yaliyokuwa yakimpa maumivu.
Ilitegemewa, na hili lilizungumzwa na Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson, kwamba Hargreaves atakuwemo kwenye Kikosi hicho cha UEFA lakini sasa nafasi yake imechukuliwa na Beki Chipukizi kutoka Ubelgiji Ritchie de Laet, miaka 21.
Ferguson alitoa matumaini hivi karibuni pale aliposema Hargreaves yupo kwenye programu ya mazoezi ya nguvu akizunguka na kupokezana kwenye Timu za Akiba na za Kwanza ya siku mbili mfululizo mazoezi na siku moja mapumziko.
Lakini inaelekea nafuu yake na kuwa fiti kumechelewa.
Katika Kikosi hicho cha Wachezaji 25, jina la Straika kijana Danny Welbeck limeondolewa kwa vile sasa yupo Preston kwa mkopo, Timu ambayo Meneja wake ni Darren Ferguson ambae ni mtoto wa Sir Alex Ferguson.
Nafasi ya Welbeck imechukuliwa na Kijana kutoka Senegal Mame Biram Diouf.
Evra: Fergie haondoki!!!
Beki wa Manchester United Patrice Evra ana imani kubwa kwamba Meneja wake Sir Alex Ferguson atabaki hapo kwa muda mrefu bila kustaafu.
Ferguson yuko kwenye wadhifa huo wa Umeneja kwa miaka 23 sasa na hajatamka lolote kuhusu lini atastaafu ingawa huko nyuma aliwahi kusema atastaafu mwishoni mwa msimu wa mwaka 2001/2 lakini akabadili uamuzi wake.
Evra alitoboa kuwa mara baada ya mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Carling ambayo Manchester United waliwafunga Mahasimu wao wakubwa Manchester City mabao 3-1 Uwanjani Old Trafford na kutinga Fainali, Sir Alex Ferguson alikuwa akicheza dansi kwa furaha kwenye vyumba vya kubadilishia jezi na hilo lilimdhihirishia Evra kuwa bado Ferguson ana njaa kubwa ya ushindi.
Evra amesema: “Tulimwona akirukaruka kama mtoto! Unaweza ukasema ni kama vile hajawahi kushinda mechi! Hilo linamfanya ashindwe kustaafu! Atabaki hapa hadi mwisho!”
Meneja Pompey akutwa danguro!!!
Wakati Klabu yake Portsmouth iko majaribuni kwa ukosefu wa fedha huku ikiwa imepata Mnunuzi mpya wa 4 katika mwaka mmoja, zimeibuka ripoti kuwa Meneja wao Avram Grant ambae ni raia wa Israel alikutwa kwenye danguro Desemba 18 mwaka jana na alipohojiwa na Mwandishi wa Habari wakati akitoka humo ndani ya danguro alikokaa kwa muda wa saa moja, Grant alikubali hilo ni danguro lakini alikataa kusema alikwenda kufanya nini.
Ingawa habari za kwamba Meneja wa Klabu ya Ligi Kuu akutwa danguroni zilijulikana wakati huo huo, jina na Klabu yake halikutajwa kwa kuogopa sheria lakini tangu Mahakama ifute amri za kutotaja majina kwenye kesi iliyomhusu John Terry, Magazeti yamepata uhuru kuyataja na ndio maana sasa jina la Grant limetajwa waziwazi.
Danguro hilo lipo jirani tu na Uwanja wa mazoezi wa Portsmouth na linaendeshwa kwa kisingizio cha mahala pa kukanda na kuchua watu.
Huko Uingereza ukahaba si kosa na kumtumia kahaba katika mahali pa faraha si kosa pia lakini kuendesha danguro ni kosa na hukumu yake ni miaka 7 jela.
Pompey yapigwa bei mara ya 4 katika mwaka mmoja!!!
Portsmouth, Klabu ya Ligi Kuu England iliyo mashakani sana ikiwa mkiani kwenye Ligi hiyo na pia kuwa taabani kifedha, imeuzwa kwa mara ya 4 katika kipindi cha mwaka mmoja na safari hii imenunuliwa na Mfanya biashara wa Hong Kong Balram Chainrai.
Wamiliki wa Klabu hiyo wa mwanzoni ni Sacha Gaydamak, Sulaiman al-Fahim na Ali al-Faraj.
Chainrai ambae alikuwa ni Mwanahisa katika Klabu hiyo iliponunuliwa na Mmiliki wa mwisho Ali al-Faraj imebidi aichukue Klabu hiyo baada ya kushindwa kumlipa pesa alizoikopesha mwanzoni mwa msimu huu.
Chainrai aliikopesha Portsmouth Pauni Milioni 17 na dhamana ilikuwa ni Uwanja wa Klabu hiyo, Fratton Park, mapato kutoka Kampuni za TV na Hisa za al-Faraj.
Portsmouth hapo jana usiku ilifungwa bao 1-0 na Fulham kwenye mechi ya Ligi Kuu na Wachezaji wao walicheza mechi hiyo huku Mishahara yao imecheleweshwa kulipwa hii ikiwa ni mara ya 4 kwa tukio kama hilo.
Vilevile, Klabu hiyo tarehe 10 Februari inatakiwa Mahakamani ilikopelekwa kufilisiwa na Mamlaka za Mapato ya Kodi kwa kushindwa kulipa kodi.
Portsmouth pia imefungiwa kusajili Mchezaji yeyote kwa kushindwa kulipa madeni kwa Klabu nyingine yanayotokana na ununuzi wa Wachezaji na hili limesababisha FA kuchukua pesa zao za mapato toka Kampuni za TV ili kuzilipa Klabu zinazoidai.
Jumamosi, Portsmouth itakuwa Old Trafford kuchuana na Mabingwa Manchester United kwenye mechi ya Ligi Kuu.
FA Cup: Leeds 1 Tottenham 3
Kwenye mechi ya marudianoya Kombe la FA huko Elland Road hapo jana, Leeds ilishindwa kuutumia vyema Uwanja wa nyumbani na kujikuta ikipigwa bao 3-1 na bao zote 3 za Tottenham zilifungwa na Starika Jermaine Defoe.
Timu hizi zilitoka sare 1-1 huko White Hart Lane mwishoni mwa Januari.
Tottenham imesonga mbele Raundi ya 5 ya Kombe hili na itasafiri kwenda kucheza na Bolton wiki inayokuja.
LIGI KUU: Fulham 1 Portsmouth 0
Bao pekee la Jonathan Greening limeipa ushindi Fulham na kuendeleza balaa kwa Timu ya mkiani Portsmouth ambayo pia ipo kwenye hali ngumu kifedha huku Wachezaji wake jana kwa mara ya 4 wakiingia Uwanjani Craven Cottage, nyumbani kwa Fulham, wakiwa hawana mishahara baada ya kuchelewa kuipata kwa mara ya 4 sasa.
Portsmouth walishindana kume pambano hilo na kukosa nafasi kadhaa za kufunga lakini walizamishwa kwa bao la dakika ya 74 kufuatia krosi ya Damien Duff kumkuta Greening aliepachika wavuni.
Jana Straika wa Italia Stefano Okaka aliichezea Fulham kwa mara ya kwanza tangu ahamie hapo kwa mkopo akitokea AS Roma hivi juzi.
Skandali la Terry: Hautemi Unahodha hadi abonge na Capello
Kuna taarifa kuwa John Terry, alieandamwa na kashfa kubwa ya kutembea na gelfrendi wa Mchezaji mwenzake Wayne Bridge aliekuwa nae Chelsea kabla hajahamia Manchester City, hatajiuzulu Unahodha wa Timu ya Taifa ya England kabla hajakutana na Meneja wa England Fabio Capello.
Terry na Capello wanategemewa kukutana siku ya Ijumaa ili kuzungumzia mkasa huo wa Terry na hatima yake kama Nahodha wa England ukizingatia skandali hilo.
Kashfa ya Terry ilifumuka baada ya Mahakama kuiondoa amri ya kutomtaja Terry iliyowekwa awali ili kuyazuia Magazeti yasiandike habari hizo.
FA imesema kuwa uamuzi wa Terry kubaki Nahodha au la anao Capello ambae kwa sasa yuko Uswisi akiuguza goti lake alilofanyiwa operesheni na anategemewa kutua London Alhamisi.
Huku Wadau wakimngoja kwa hamu Capello kusema yake, skandali hili la Terry linaweza kuchukua hatua mpya baada ya kuibuka tetesi kuwa huyo gelfrendi wa Wayne Bridge ambae ni Mfaransa aitwae Vanessa Perroncel ameshapokea bulungutu la Pauni Laki 250 kutoka Gazeti maarufu ili aelezee upande wake wa sakata hilo na hivyo kumfedhehesha zaidi John Terry.
LIGI KUU England: RATIBA WIKI NZIMA IJAYO
[saa za kibongo]
Jumamosi, Februari 6
[saa 9 dak 45 mchana]
Liverpool v Everton
[saa 12 jioni]
Bolton v Fulham
Burnley v West Ham
Hull v Man City
Man Utd v Portsmouth
Stoke v Blackburn
Sunderland v Wigan
[saa 2 na nusu usiku]
Tottenham v Aston Villa
Jumapili, Februari 7
[saa 10 na nusu jioni]
Birmingham v Wolverhampton
[saa 1 usiku]
Chelsea v Arsenal
Jumanne, Februari 9
[saa 4 dak 45 usiku]
Fulham v Burnley
Man City v Bolton
Portsmouth v Sunderland
Wigan v Stoke
Jumatano, Februari 10
[saa 4 dak 45 usiku]
Arsenal v Liverpool
Aston Villa v Man Utd
Blackburn v Hull
West Ham v Birmingham
Wolverhampton v Tottenham
[saa 5 usiku]
Everton v Chelsea
Beckham: ‘Man United ni kipenzi changu!’
Supastaa David Beckham amekiri kuwa Manchester United ni kipenzi chake cha kwanza na ana hamu kubwa sana ya kurudi kucheza Old Trafford wakati Timu anayochezea sasa hivi kwa mkopo AC Milan itakapoenda huko kuikwaa Man United baadae mwezi huu kwa pambano la Mtoano la UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Beckham alianza kucheza soka tangu akiwa mtoto kwenye Chuo cha Watoto hapo Manchester United na aliinukia na kuchezea Timu ya kwanza mechi 265 katika kipindi cha miaka 12 na kutwaa Mataji mengi hadi alipohama na kwenda Spain kuchezea Real Madrid mwaka 2003.
Beckham sasa anacheza soka lake huko Marekani akiwa na Timu ya LA Galaxy.
Beckham amesema: “Nilipoondoka Man United miaka ya mwanzoni ilikuwa migumu sana kwani niliimisi sana Timu hiyo! Ni Klabu pekee niliyotaka niichezee daima! Siku zote natamani bado ningebakia Man United! Mie ni shabiki mkubwa wao na hutazama mechi zao zote nikiwa na nafasi!”

Wednesday, 3 February 2010

FA CUP: Crystal Palace na Notts County wazinanga Timu Kubwa!!!
• Mufilisi Palace wairarua Wolves!!
• County waipiga Wigan!!
Crystal Palace na Notts County, Klabu za Daraja la chini, zimezitoa toka kwenye Kombe la FA Timu za Ligi Kuu Wolves na Wigan katika mechi za marudiano hapo jana baada ya kutoka suluhu mechi za awali.
Crystal Palace ambayo iko hali mbaya kifedha na huenda ikafilisiwa imeikung'uta Wolves mabao 3-1.
Notts County wao wamewapiga Wigan bao 2-0.
Crystal Palace sasa watakutana na Aston Villa kwenye Raundi ya 5 ya Kombe hilo la FA hapo Februari 14 na Notts County watacheza na Fulham.
Ancelotti amruhusu John Terry kupumzika!!
Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti amesema Nahodha wao John Terry ambae anasakamwa na skandali la kutembea na gelfrendi wa Wayne Bridge ambae alikuwa Mchezaji wa Chelsea kabla hajahamia Manchester City, yuko huru kuchukua likizo wakati wowote ili kupumzisha akili kufuatia kuandamwa kwa siku kadhaa sasa baada ya Mahakama kufuta amri ya kutomtaja jina kwenye kashfa hiyo.
Pia, kumekuwa na wito kutoka kila pembe kwa Terry kujiuzulu wadhifa wa Unahodha wa Timu ya Taifa ya England.
Tangu kuibuka kwa kashfa hiyo John Terry ameshacheza mechi mbili za Ligi Kuu ya kwanza ikiwa ile Chelsea waliyoifunga Burnley 2-1 huku Terry akifunga bao la pili na la ushindi na mechi nyingine ni ya jana Chelsea waliyotoka sare 1-1 na Hull City.
Ancelotti alitamka: “Bado anacheza vizuri! Nitamruhusu akitaka kupumzika!”
Mameneja watwangana Uwanjani!!!
Meneja wa Nottingham Forest, Billy Davies, amedai kuwa Meneja wa Derby County, Nigel Clough, alimshindilia na goti wakati kulipotokea fujo kati ya Timu hizo mbili zilipocheza wiki iliyopita na ameitaka FA imchukulie hatua kali Nigel Clough.
Hata hivyo FA imeamua kutowashitaki watu binafsi na badala yake imezishitaki Timu zote mbili kwa kuleta fujo.
Nae Nigel Clough ambae enzi za Uchezaji wake alikuwa Mchezaji wa Nottingham Forest wakati huo Baba yake Mzazi, Brian Clough, akiwa Meneja hapo Forest, amezikana tuhuma hizo za Billy Davies na kudai kuwa ikiwa alimgusa Davies basi ilikuwa ni bahati mbaya tu kwani kulikuwa na vurugu na rabsha iliyowahusu Wachezaji wa pande hizo mbili na watu wengi wengine.
Timu za Nottingham Forest na Derby County zinatoka Mji mmoja wa Derby na zilipokutana mara ya mwisho mwezi Agosti mwaka jana pia kulizuka fujo na Klabu hizo mbili zikapigwa faini na FA.
LIGI KUU England: Hull City 1 Chelsea 1
Hull City walikipiga kiume na kuisimamisha Chelsea kwa kutoka droo ya 1-1 katika mechi ya LigI kuu iliyochezwa Uwanja wa KC hapo jana na hivyo kuwazuia vinara wa Ligi Chelsea kuongeza uongozi wao wa Ligi kuwa pointi 4 mbele ya Timu ya Pili Manchester United.
Kwa matokeo hayo, msimamo wa Ligi huko kileleni ni:
[Timu zimecheza mechi 24 isipokuwa inapotajwa]
1 Chelsea pointi 55
2 Man Utd pointi 53
3 Arsenal pointi 49
4 Tottenham pointi 42
5 Liverpool pointi 41
6 Manchester City pointi 41 [mechi 22]
7 Aston Villa pointi 40 [mechi 23]
Hull City ndio walipata bao la kwanza kupitia Steven Mouyokolo aliefunga kwa kichwa dakika ya 30.
Didier Drogba akicheza mechi yake ya kwanza tangu arudi toka Angola alikoichezea Nchi yake Ivory Coast kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika alisawazisha kwa frikiki muda mfupi kabla haftaimu.
Ingawa Hull City wamepata pointi moja kwenye mechi hii lakini bado wako kwenye lile eneo la hatari la Timu 3 za chini zinazoporomoka Daraja.
Hull City wako nafasi ya 18 wakiwa juu tu ya Burnley na Timu iliyo mkiani Portsmouth.
MECHI YA LIGI KUU LEO jumatano Februari 3:
[saa 5 usiku, saa za bongo]
Fulham v Portsmouth
Licha ya kuchelewa Uhamisho, Benjani aruhusiwa na FA!!!
Mchezaji kutoka Zimbabwe, Benjani Mwaruwaru, ameruhusiwa na FA kuhama kwa mkopo kutoka Manchester City kwenda Sunderland licha ya makabrasha yake ya uhamisho kuchelewa kufika FA na kupokelewa Masaa 23 baada ya dirisha la uhamisho kufungwa hapo Jumatatu Februari 1.
FA ilichunguza na kuridhika kuwa matatizo ya kiufundi ndio yaliyosababisha barua pepe za uhamisho wa Benjani kuchelewa kuwafikia kwa wakati na hivyo kuubariki uhamisho huo.
Kwa Benjani Sunderland ni Klabu yake ya 3 kuichezea kwenye Ligi Kuu England baada ya kuwepo Portsmouth na Manchester City.
Meneja wa Sunderland, Steve Bruce, akiwa mwenye furaha alisema: “Ni jitu kubwa lenye nguvu na ni Sentafowadi tuliemtaka siku nyingi!”

Tuesday, 2 February 2010

LIGI KUU England: Leo vinara Chelsea wako KC!!!
Timu inayoongoza Ligi Kuu, Chelsea, leo wako ugenini Uwanja wa KC nyumbani kwa Hull City ambao hali yao ni taaban kwenye Ligi hiyo na wako nafasi ya 19 ikiwa ni nafasi moja toka mkiani.
Chelsea, kama kawaida, wataongozwa na Nahodha wao John Terry ambae kwa sasa anasakamwa na skandali la kutembea na gelfrendi wa Mchezaji mwenzake wa Chelsea wakati huo, Wayne Bridge, lakini hilo halikumzuia katika mechi iliyopita dhidi ya Burnley kupachika bao la pili na la ushindi kwa Chelsea.
Chelsea pia wataongezwa nguvu baada ya kurudi Wachezaji wao Didier Drogba, Salomon Kalou na Mikel Obi waliokuwa Angola kwenye Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Hull City nao huenda wakamchezesha Mchezaji wao mpya kutoka Misri Amr Zaki ambae alianza kucheza mechi ya juzi akitokea benchi walipocheza na Wolves.
Endapo Chelsea atashinda mechi hii atakuwa amejivuta pointi 4 mbele ya Timu ya Pili Manchester United na Timu zitakuwa zimecheza mechi sawa.
Mechi hii itaanza saa 4 dakika 45 saa za bongo.
MSIMU WA ARSENAL WAENDA ALIJOJO???????
HII TULIITOA:
Friday, 22 January 2010
Arsenal yupo kileleni lakini kimbembe chao kinakuja!!!
Wiki 3 zijazo, Mechi 6 zijazo kuamua MBIVU au MBICHI!!!!
Baada ya kuwatungua Bolton mabao 4-2 hapo juzi huku wakipata ‘msaada mkubwa’ wa Refa Alan Wiley na hivyo kukaa kileleni mwa Ligi Kuu, Arsenal sasa ndio wanaingia hatua ngumu mno kwao kwa kukumbana na Vigingi na Vigogo vya kila aina ambavyo wakivishinda basi wanaweza wakatwaa Mataji yao ya kwanza tangu Mwaka 2005 walipotwaa FA Cup kwa mara ya mwisho.
RATIBA YAO YA WIKI 3 ZIJAZO NI:
Jumapili, Januari 24
FA Cup: Stoke v Arsenal====== 3-1 AUTI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Jumatano, Januari 27
LIGI KUU: Aston Villa v Arsenal========SARE 0-0
Jumapili, Januari 31
LIGI KUU: Arsenal v Man United========KIPONDO 1-3
Jumapili, Februari 7
LIGI KUU: Chelsea v Arsenal=========ITAKUWAJE??????????????
Jumatano, Februari 10
Arsenal v Liverpool============NINI??????????????
Jumatano, Februari 17
UEFA CHAMPIONS LEAGUE: FC Porto v Arsenal=========VIPI????????????????
UHAMISHO-Januari 2010
Dirisha la uhamisho la Januari liliendelea hadi Jumatatu Februari 1 kwa vile Januari 31 ilikuwa ni Jumapili.
Ifuatayo ni orodha kamili ya Wachezaji waliohama au kuhamia Timu za Ligi Kuu katika kipindi hicho cha lala salama.
-Mkopo Troy Archibald-Henville [Tottenham - Exeter]
-Ada haikutajwa Asmir Begovic [Portsmouth - Stoke]
-£3.25m Marcus Bent [Birmingham - QPR]
-Mkopo Wayne Brown [Fulham - Bristol Rovers]
-Mkopo Christopher Buchtmann [Liverpool - Fulham]
-Mkopo Jack Cork [Chelsea - Burnley]
-Mkopo Daniel Cousin [Hull – Larissa]
-Mkopo Peter Halmosi [Hull - Szombathely Haladas]
-Mkopo David Healy [Sunderland - Ipswich]
-Haikutajwa Alan Hutton [Tottenham - Sunderland] –
-Mkopo Ilan [St Etienne - West Ham]
-Mkopo Adam Johnson [Middlesbrough - Manchester City]
-Haikutajwa Damien Johnson [Birmingham - Plymouth]
-Bure Toni Kallio [Fulham - Sheffield United]
-Mkopo Diomansy Kamara [Fulham - Celtic]
-Mkopo Robbie Keane [Tottenham – Celtic]
-Mkopo Ben Marshall [Stoke – Carlisle]
-Bure Benni McCarthy [Blackburn - West Ham]
-Bure Mido [Middlesbrough - West Ham]
-Bure Marcelo Moreno [Shakhtar Donetsk - Wigan]
-Bure Victor Moses [Crystal Palace - Wigan]
-Haikutajwa Daryl Murphy [Sunderland – Ipswich]
-Haikutajwa Kyle Naughton [Tottenham - Middlesbrough]
-Mkopo Lewis Nightingale [Huddersfield - Wakefield]
-Mkopo Nyron Nosworthy [Sunderland - Sheffield United]
-Haikutajwa David Nugent [Portsmouth - Burnley]
-Mkopo Stefano Okaka [Roma - Fulham]
-Mkopo Jim Paterson [Plymouth - Aberdeen]
-Mkopo Alessandro Pellicori [QPR - AC Mantova
-Haikutajwa Nicky Shorey [Aston Villa – Fulham]
Rio kukata rufaa tena!!!
Rio Ferdinand wa Manchester United alifungiwa mechi 3 kwa kosa la kumpiga Craig Fagan wa Hull City huku Refa Steve Bennett haoni kwenye mechi ya Ligi Kuu kati ya Manchester United na Hull City na akakata rufaa kupinga adhabu hiyo lakini Jopo la Nidhamu likaona misingi yake ya kukata rufaa haina msingi hivyo wakamwongezea adhabu ya kumfungia mechi moja zaidi.
Tayari Ferdinand ameshaanza kutumikia kifungo chake na aliikosa mechi ya juzi na Arsenal na mechi nyingine atakazozikosa ni zile dhidi ya Portsmouth, Aston Villa na Everton.
Sasa Ferdinand amekata rufaa kupinga hiyo nyongeza ya mechi moja na akishinda rufaa hii ataweza kucheza mechi na Everton.
Kisheria, Ferdinand haruhusiwi kukata rufaa kupinga adhabu yote bali ni ile ya nyongeza tu lakini kisheria pia akishindwa rufaa hii ya pili, Ferdinand anaweza kuongezewa mechi moja zaidi na kufanya kifungo chake kuwa mechi 5 na hivyo kuikosa Fainali ya Kombe la Carling hapo Februari 28 dhidi ya Aston Villa.
Lakini adhabu za Ferdinand hazimzuii kucheza mechi ya Februari 16 ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE dhidi ya AC Milan.
UHAMISHO SIKU YA MWISHO: Mkenya akosa ulaji Man City!!!
• Mido, McCarthy watua West Ham!!
McDonald Mariga, miaka 22, anaechezea Klabu ya Italia Parma ambae ni Mchezaji wa Kimataifa kutoka Kenya amekataliwa kupewa kibali cha kazi cha England na hivyo kumkosesha uhamisho wa ada ya Pauni Milioni 7 kwenda Manchester City na pia kumkosesha kuwa Mchezaji wa kwanza toka Kenya kucheza Ligi Kuu England.
Mariga, aliechezea Harambee Stars mechi 24 na hivyo kutimiza kipengele kinachotaka Wachezaji kucheza asilimia 75 ya mechi za Kimataifa katika miaka miwili, ombi lake la kibali lilitupwa nje kwa vile Kenya ipo nafasi ya 98 kwenye msimamo wa ubora wa FIFA na ni Wachezaji waliotoka Nchi zilizo nafasi 70 za juu ndio wanahusishwa kupatiwa vibali.
Wakati huohuo huku ule muda wa kufungwa dirisha la uhamisho ukikaribia, Klabu kadhaa zimefanikiwa kunyakua Wachezaji katika dakika za mwisho na West Ham wameweza kuwachukua Wachezaji wawili wanaotoka Afrika.
Mido, ambae anachezea Zamalek ya Misri, amechukuliwa West Ham kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu.
Nae Benni McCarthy kutoka Afrika Kusini aliekuwa akicheza Blackburn Rovers amehamia rasmi West Ham.
Robbie Keane wa Tottenham yuko mbioni kupelekwa kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu huko Celtic ya Scotland.
Manchester City imemsaini Mchezaji kutoka Middlesbrough aitwae Adam Johnson.
Habari kamili za uhamisho tutawaletea baadae.
KASHFA YA TERRY: Wachezaji Man City wamsapoti mwenzao Bridge!!
Wacheza watatu wa Manchester City walivaa tisheti chini ya Jezi zao zilizoandikwa ‘Team Bridge’ ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono mwenzao Wayne Bridge ambae imedaiwa gelfrendi wake alitembea na Nahodha wa Chelsea na England, John Terry.
Wachezaji hao watatu walivaa tisheti hizo katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa City of Manchester Stadium Jumapili na Man City kuifunga Portsmouth 2-0.
Wachezaji hao ni Carlos Tevez, Stephen Ireland na Nigel de Jong.
Meneja wa Man City Roberto Mancini alitamka: “Wachezaji wako karibu na Wayne Bridge. Ni ishara yao kumuunga mkono.”
Mancini aliongeza: “Bridge ni Mchezaji mzuri na mtu safi sana!”
KISAGO CHA EMIRATES:
Wenger alaumu Wachezaji wake
• Fergie asifia Timu yake, Nani apewa heko!!
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amewaponda Wachezaji wake kufuatia kipigo cha 3-1 walichokipata nyumbani Uwanjani Emirates toka kwa Manchester United katika mechi ya Ligi Kuu hapo Jumapili.
Wenger alisema: “Tulikuwa wazembe! Hatukucheza kitimu! Hatukuwa kwenye fomu!”
Kipigo hicho kilimaliza wimbi la mechi 10 katika Ligi bila kufungwa baada ya kupigwa bao 3 na Chelsea Uwanjani hapo hapo Emirates mwezi Novemba mwaka jana.
Sasa Arsenal ina kibarua kingine kigumu Jumapili ijayo huko Stamford Bridge watakapoenda kuwatembelea vinara wa Ligi Chelsea.
Wenger alikiri: “Man United walikuwa bora kupita sisi! Tuliwapa nafasi kubwa! Hatukucheza vizuri na sijui kwa nini! Itabidi tubadilike kwa mechi ijayo!”
Nae Sir Alex Ferguson, Meneja wa Manchester United, ameitaka Timu yake sasa ikaze buti na iendeleze wimbi la ushindi.
Ferguson amewasifia Wayne Rooney na Nani kwa uchezaji wao wa kujituma kwenye mechi hiyo.
Ferguson alisema: “Tulicheza vizuri mno! Wachezaji wote walikuwa tayari kwa pambano hili! Walikuwa shapu na walipasiana vizuri na tulipata nafasi nyingi sana za wazi!”
Ferguson aliongeza kwa kusema Timu yake hutumia sana mbinu ya kushambulia kwa kushtukiza, yaani ‘kaunta ataki’, na kwa vile Arsenal wanamiliki sana mipira na huja kwenye boksi lako mara kwa mara ukiunasa mpira hapo na kushambulia kwa haraka sana utawafunga tu.
Kuhusu Rooney, Ferguson alisema: “Ana furaha hapa. Yeye hajabadilika na utajiri na ustaa haujambadilisha chochote! Watu wengi hubadilika wakifanikiwa lakini Rooney yu vilevile! Kwa mara nyingine alikuwa shujaa wetu!”
Rooney alifunga bao moja katika ushindi huo wa 3-1 dhidi ya Arsenal na hilo ni goli lake la 100 katika Ligi Kuu na limemfanya awe Mchezaji wa 18 kufunga goli 100 katika Ligi Kuu.
Kuhusu Nani, Ferguson alitamka: “Alikuwa majeruhi lakini amepona na sasa amekomaa!! Mechi zake 3 za mwisho amecheza vizuri na hii amecheza bora zaidi!”

Sunday, 31 January 2010

Arsenal 1 Man United 3
Wakiwa kwao Uwanja wa Emirates, Arsenal leo walikiona cha mtema kuni pale walipobebeshwa magoli 3-1 na Mabingwa Watetezi Manchester United.
Mpaka mapumziko Man United walikuwa mbele kwa mabao ya Nani na Rooney.
Kipindi cha pili, Park akapachika bao la 3 kwa Man United.
Bao la Arsenal lilifungwa na Vermaelen.
VIKOSI VILIKUWA:
Arsenal: Almunia, Sagna, Gallas, Vermaelen, Clichy, Fabregas, Song Billong, Denilson, Nasri, Arshavin, Rosicky.
Akiba:: Fabianski, Walcott, Ramsey, Silvestre, Eboue, Traore, Bendtner.
Man Utd: Van der Sar, Rafael Da Silva, Jonathan Evans, Brown, Evra, Scholes, Carrick, Fletcher, Nani, Rooney, Park.
Akiba: Kuszczak, Owen, Berbatov, Giggs, Valencia, Gibson, De Laet.
Refa: Chris Foy
KOMBE LA AFRIKA: Misri Mabingwa tena!!
Kwa mara ya tatu mfululizo, Misri wameweza kutwaa Ubingwa wa Afrika baada ya kuifunga Ghana bao 1-0 katika Fainali iliyochezwa huko Luanda, Angola.
Bao la ushindi la Misri limefungwa na Gedo.
Man United: ‘Rooney hauzwi kwa bei yeyote ile!!’
Mkurugenzi Mtendaji wa Manchester United, David Gill, ametamka kuwa Straika wao Wayne Rooney hauzwi kwa bei yeyote ile.
Msimu huu Rooney ni moto wa kuotea mbali na tayari ameshafunga jumla ya mabao 21 na kwenye Ligi Kuu yeye ndie anaeongoza kwa ufungaji.
Kumekuwa na tetesi kuwa Klabu za Spain Real Madrid na Barcelona zinamnyemelea Rooney.
David Gill amesema: “Labda atake Meneja wake Sir Alex Ferguson, lakini sisi hatukubali ofa yeyote kwake! Sisi tunataka abaki hapa!”
Vile vile, David Gill aliwapoza Mashabiki wenye wasiwasi kuwa Man United hamna pesa za kununua Wachezaji kwa kutoboa kuwa Klabu hiyo ilitoa ofa ya Euro Milioni 35 kumnunua Karim Benzema lakini ofa hiyo ikakataliwa na Mchezaji huyo akanunuliwa na Real Madrid kwa zaidi ya Euro Milioni 40 kiwango ambacho David Gill amesema Sir Alex Ferguson aliona ni kikubwa mno.
Gill alisistiza kuwa Rooney ana mkataba hadi 2012 na mwishoni mwa msimu huu mazungumzo yataanza na Wawakilishi wa Rooney ili kuuboresha na kuurefusha mkataba wake.
Katika dirisha la uhamisho la Januari Man United imemnunua Mlinzi Chipukizi Chris Smalling, miaka 20, kutoka Fulham kwa dau linalokadiriwa kuwa Pauni Milioni 7 na Mchezaji huyo ameachwa aendelee Fulham hadi mwishoni mwa msimu.
Adebayor: “Hayatou ameisaliti Togo!!”
Nahodha wa Togo, Emmanuel Adebayor, ambae pia huichezea Manchester City, amechukizwa na uamuzi wa CAF, Chama cha Soka cha Afrika, wa kuifungia Togo kutocheza Mashindano yajayo mawili ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kosa la kujitoa kucheza Fainali za Kombe hilo huko Angola.
Togo walijitoa baada ya Serikali yao kuwataka warudi nyumbani baada ya Dereva wa Basi lao pamoja na Kocha Msaidizi na Afisa Habari kuuawa kwa risasi wakati wakisafiri ndani ya Basi hilo kuelekea Mji wa Cabinda wakitokea Congo.
Adebayor amesema Issa Hayatou, Rais wa CAF anaetoka Cameroun, amewasaliti na inabidi aachie ngazi cheo hicho.
CAF wamedai kufungiwa kwa Togo ni kwa sababu mambo ya Soka kuingiliwa na Serikali yao.
Lakini Adebayor anadai: “Hawajali vilio vya dunia! Ni Nchi iliyotutuma twende Angola! Ni Nchi iliyotutaka turudi nyumbani kuomboleza!”
KASHFA YA TERRY: Terry kubaki Kepteni Chelsea!!
• Jana alicheza na kufunga bao la ushindi!!!
Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti amesema Beki wao John Terry atabaki kuwa Kepteni wa Klabu hiyo licha ya kulipuliwa kwa kashfa juu yake kuwa alitembea na gelfrendi wa Mchezaji mwenzake wa Chelsea wakati huo, Wayne Bridge, kashfa ambayo imeibuka na Terry kutajwa baada ya Mahakama kufutilia mbali amri ya kutomtaja Terry.
Kumekuwa na kauli mbiu kuwa Terry ambae pia ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya England aondolewe Unahodha wa Timu hiyo ya Taifa.
Jana Chelsea waliifunga Burnsley 2-1 kwenye Ligi Kuu na Terry alicheza huku akivaa utepe wa Unahodha wa Chelsea na pia kuifungia Chelsea bao la pili na la ushindi.
Ancelotti ametamka: “Hamna mjadala kuhusu Terry. Sijui kwa nini naulizwa! Yeye ni Nahodha wetu! Klabu yote tunamsapoti yeye na familia yake!”
Mpaka sasa FA, Chama cha Soka cha England, hakijatoa tamko lolote.
Lakini Wayne Bridge, ambae kwa sasa ni Mchezaji wa Manchester City na pia huchezea England, ametoa tamko kupitia kwa Wanasheria wake wa kuomba faragha yake na familia yake iheshimiwe na asiingliwe. 
KOMBE LA AFRIKA: Mshindi wa 3 Nigeria!
Nigeria jana waliweza kunyakua nafasi ya 3 katika Kombe la Mataifa ya Afrika walipoifunga Algeria bao 1-0.
Bao la Nigeria lilifungwa dakika ya 55 na Victor Nsofor Obinna.
Leo Uwanjani Novemba 11 Mji Mkuu wa Angola Luanda, Fainali ndio itafanyika kati ya Bingwa Mtetezi Misri na Ghana.
Mechi hii itaanza saa 1 usiku, saa za bongo.
MATOKEO LIGI za Ulaya jana:
SERIE A:
AS Bari 4 v Palermo 2
Napoli 0 v Genoa 0
LA LIGA:
RCD Espanyol 1 v Athletic de Bilbao 0
Sporting Gijon 0 v FC Barcelona 1
Deportivo la Coruna 1 v Real Madrid 3
BUNDESLIGA:
Bayern Munich 3 v FSV Mainz 0
Borussia Munchen Gladbach 4 v SV Werder Bremen 3
Hannoverscher 1896 1 v FC Nurnberg 3
Hertha Berlin 0 v VFL Bochum 0
Eintracht Frankfurt 1 v FC Koln 2
Schalke 04 2 v TSG Hoffenheim 0
LIGUE 1:
FC Girondins de Bordeaux 0 v US Boulogne 0
Lille OSC 1 v Racing Club de Lens 0
Le Mans 1 v Toulouse FC 3
AS Nancy Lorraine 1 v Lorient 0
AS Monaco FC 3 v Nice 2
Stade Rennais FC 4 v Grenoble 0
Montpellier HSC 2 v Olympique de Marseille 0
Powered By Blogger