Saturday, 24 May 2008

NANI ATAINGIA LIGI KUU: HULL CITY AU BRISTOL CITY?
fainali WEMBLEY leo saa 11 jioni!!

Mbele ya mashabiki wapatao 80,000 leo itapatikana timu ya tatu kupanda daraja kuungana na timu za WEST BROMWICH ALBION na STOKE CITY ambazo zilipanda kuingia LIGI KUU UINGEREZA moja kwa moja baada ya kushika nafasi za kwanza na za pili.
Timu zilizoingia fainali ya mtoano ya kupata timu ya tatu kupanda daraja ni timu za HULL CITY na BRISTOL CITY. Timu zote hizi hazijawahi kuchezea LIGI KUU.
HULL CITY iliitoa WATFORD kwa jumla ya mabao 6-1 na BRISTOL CITY iliifunga CRYSTAL PALACE jumla ya mabao 4-2.
Itakumbukwa timu zilizoshuka daraja ni DERBY, BIRMINGHAM na READING.

Friday, 23 May 2008



SIR ALEX FERGUSON AFOKA NA KUISHUTUMU REAL MADRID JUU YA RONALDO!!
Awaita ni WAKOSA MAADILI!


Meneja wa MAN U, Sir Alex Ferguson ameishutuma vikali Klabu ya Spain, REAL MADRID, kwa kukosali maadili, utu na nidhamu.

Kocha wa REAL, Bernd Schuster na Rais wa Klabu hiyo, Ramon Calderon, wote wamekaririwa wakidai watamsajili RONALDO msimu huu.

Ferguson alifoka:'Schuster anabwabwaja na Calderon anabwabwaja'

'REAL wanadhani wanaweza wakazifosi timu ila wakae wakijua kwetu hawawezi. Barcelona ni Klabu ya kiungwana kuliko REAL ambayo ni wakosa maadili. REAL wanafikiri wanaweza kutumia Gazeti la Spain, MARCA, kuwachota akili wachezaji.'

Ferguson aliendelea:'Hivi mnafikiri Klabu nyingine kubwa Ulaya hazitaki wachezaji wetu? Wanataka ila ni waungwana na hawatangazi ovyo nia zao kama hao wapuuzi wa REAL. Wakae wakijua RONALDO bado ana mkataba wa miaka minne.'

'Huyo Calderon anadai biashara ya utumwa iliondolewa miaka 100 nyuma! Si wangemwambia Jenerali Franco basi?' [JENERALI FRANCO ALIKUWA MTAWALA DHALIMU NA DIKTETA WA SPAIN MIAKA YA NYUMA].




MABINGWA WA UINGEREZA NA ULAYA, MANCHESTER UNITED, WARUDI NYUMBANI BAADA YA KUFANYA PATI USIKU KUCHA HOTELINI MJINI MOSCOW!!!
Timu ya MAN U jana usiku iliwasili nyumbani Manchester na waliteremka kwenye ndege huku wamebeba MAKOMBE MAWILI-LA UBINGWA WA LIGI KUU UINGEREZA na KOMBE LA KLABU BINGWA ULAYA.

Thursday, 22 May 2008


NI MABINGWA!!!!!!!!!!!!!!!!

Wednesday, 21 May 2008



SI JUU YA ROON NA RON TU!!!!!

Sir Alex Ferguson amesema MAN UNITED haitawategemea nyota wake ROONEY na RONALDO pekee ili kupata ushindi.

Alitamka: 'Hawa bado ni wadogo na chipukizi na bila shaka hapo baadae watapata mafanikio makubwa na ni kweli wanatubeba sana. Lakini mechi ya leo ni ya wachezaji wote 11'

DONDOO ZA FAINALI YA LEO KLABU BINGWA ULAYA






'FAINALI YA LEO ITAAMULIWA NA REFA!-ARSENE WENGER


Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amejikita kwenye mjadala wa nani bingwa leo kati ya MAN U na CHELSEA huko LUZHNIKI STADIUM, MOSCOW, URUSI kwa kudai REFA, kutoka SLOVAKIA LUBOS MICHEL [pichani], ndie atakaeamua nani BINGWA. Kauli yake inafuatia madai yake kuwa msimu huu MAREFA walileta utata mkubwa.






REFA huyu wa leo tayari alishawaletea mzozo Chelsea mwaka 2005 alipowapa ushindi Liverpool katika nusu fainali ya mashindno haya aliporuhusu bao la Luis Garcia wakati Chelsea wnadai halikuvuka mstari.


===================================================



DROGBA: 'MAREFA HUNIONYA KABLA YA MECHI NISIJIANGUSHE MAKSUDI!'

Nyota wa Chelsea, Didier Drogba, amesema MAREFA wamekuwa na kawaida ya kumpa onyo kabla ya mechi kuwa asijifanye kuangushwa.

Nae anasema huwa nawajibu: 'MIE NI MWANASOKA NA SIO MWOGELEAJI!'

Tuesday, 20 May 2008

NI MWAKA 1997!!! BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU UINGEREZA!!!!

JE UNAWAKUMBUKA HAWA?

NI 'VIFARANGA WA FERGUSON' kama Mapaparazi UINGEREZA WALIVYOWABATIZA!

Kutoka kushoto ni NICKY BUTT, RYAN GIGGS, DAVID BECKHAM, GARRY NEVILLE, PAUL SCHOLES na mbele amekaa PHILLIP NEVILLE!



MAHOJIANO YA MWISHO NA MAPAPARAZI-KABLA FAINALI KESHO!!!!

MAMENEJA SIR ALEX FERGUSON WA MAN U NA AVRAM GRANT WA CHELSEA LEO WAMEFANYIWA MAHOJIANO YAO YA MOJA KWA MOJA [LIVE] KABLA YA MECHI YA FAINALI KATI YA TIMU ZAO HAPO KESHO UWANJANI LUZHNIKI, MOSCOW, URUSI.
KWA MENEJA FERGUSON SWALI KUBWA ALILOPAMBANA NALO AMBALO LILIKUWA LA UDADISI MKUBWA KWA WENGI LILIKUWA JE RONALDO ATAKUWEPO MAN U MSIMU UJAO? AKIONEKANA ALIETULIA NA MWENYE FURAHA KUBWA, FERGUSON ALILIPUUZA NA KUJIBU: 'KAMA UNATAKA KUWEKA DAU WEKA, NA MIMI NITAWEKA DAU KUBWA SANA!'
KUHUSU MECHI ALISEMA:'HATUWEZI KUIMILIKI MECHI YOTE ILA TUNAJUA NGUVU ZETU NA KASORO ZETU. NAWAAMINI WACHEZAJI WANGU'
'CHELSEA NI TIMU NGUMU NA YENYE NGUVU NA WANATEGEMEA HILO. SISI HATUHITAJI KUSHINDANI NAO KWA HILO. SISI TUNATAKIWA KUELEKEZA NGUVU ZETU KWENYE UHODARI WETU WA KUMILIKI MPIRA, KUZUNGUKA UWANJA MZIMA NA UWEZO WETU WA KUFUNGUA MIANYA.'
NAE MENEJA WA CHELSEA, AVRAM GRANT, AKIKERWA NA WANDISHI WENGI WALIOHOJI HATMA YAKE, ALISEMA:'KWA NINI? TUKO HAPA SIKU 11 BAADA YA LIGI KWISHA NA KAMA INGEKUWA MSIMU WA KAWAIDA SAA HIZI TUKO LIKIZO. LAKINI TUKO HAPA KWA SABABU NI MECHI MUHIMU KWA KLABU DUNIANI, NI FAINALI YA MABINGWA. INABIDI MUHESHIMU WATU WOTE WA CHELSEA NA MUULIZE MASWALI KUHUSU FAINALI NA SI MIMI!'
AKIGEUKIA MECHI ALISEMA:'MAN U NI TIMU NZURI SANA. WALIKUWA NA MSIMU MZURI NA NI MABINGWA. NINI ZAIDI UTASEMA? UNAWEZA KUJITAYARISHA KWA KILA AINA YA HALI LAKINI HUJUI NINI KITATOKEA WAKATI TIMU NZURI ZIKIPAMBANA'

MAN U vs CHELSEA


NJIA WALIYOPITA KWENDA MOSCOW

MAN U


KUNDI F


SPORTING LISBON 0 MAN U 1

MAN U 1 ROMA 0

DYNAMO KIEV 2 MAN U 4

MAN U 4 DYNAMO KIV 0

MAN U 2 SPORTING LISBON 1

ROMA 1 MAN U 1


RAUNDI YA PILI


LYON 1 MAN U 1


MAN U 1 LYON 0


ROBO FAINALI


ROMA 0 MAN U 2


MAN U 1 ROMA 0


NUSU FAINALI


BARCELONA 0 MAN U 0


MAN U 1 BARCELONA 0


CHELSEA


KUNDI B


ROSENBORG 1 CHELSEA 1

VALENCIA 1 CHELSEA 2

CHELSEA 2 SCHALKE 0

SCHALKE O CHELSEA 0

ROSENBORG 0 CHELSEA 4

CHELSEA 0 VALENCIA 0


RAUNDI YA PILI


OLYMPIACOS 0 CHELSEA 0


CHELSEA 3 OLYMPIACOS 0


ROBO FAINALI


FENERBAHCE 2 CHELSEA 1


CHELSEA 2 FENERBAHCE 0


NUSU FAINALI


LIVERPOOL 1 CHELSEA 1


CHELSEA 3 LIVERPOOL 2


REFA AMBAYE 2005 CHELSEA WALIDAI AMEWAFUNGISHA GOLI LA MAZIMWI KESHO KUCHEZESHA FAINALI!

MIZUKA YA KLABU BINGWA ULAYA IMEIBUKA VIBAYA KWA CHELSEA BAADA YA REFA ALIEIFUNGISHA VIRAGO TIMU HIYO KATIKA NUSU FAINALI YA MASHINDANO HAYO MWAKA 2005 WALIPOTELEWA NA LIVERPOOL HUKO ANFIELD KWA BAO LA UTATA LA LUIS GARCIA KUPANGWA KUCHEZESHA KESHO KATIKA FAINALI YA KLABU BINGWA ULAYA DHIDI YA MAN U HUKO UWANJA WA LUZHNIKI MJINI MOSCOW, URUSI.

Refa huyo, Lubos Michel na msaidizi wake, Roman Slysko, wamekuwa wakichukiwa na Chelsea tangu waliporuhusu hilo bao la LIVERPOOL.
Meneja wa Chelsea wakati huo, JOSE MOURINHO, alikasirika na kusema: 'LILIKUWA GOLI LILILOTOKA MWEZINI. GOLI LA KIZIMWI'.

ILIDAIWA MPIRA HUO HAUKUVUKA MSTARI WA GOLI INGAWA MSAIDIZI WA REFA ALIASHIRIA NI GOLI. HATA HIVYO ILIONEKANA DHAHIRI KIPA WA CHELSEA PETR CECH AKIMCHEZEA MFUNGAJI RAFU NA BAADAE REFA HUYO ALINUKULIWA AKISEMA KAMA MSAIDIZI WAKE ASINGESEMA HILO NI GOLI BASI LAZIMA AGEMPA KADI NYEKUNDU CECH NA KUTOA PENALTI.

Lubos Michel na Roman Slysko wataungana na Waslovakia wengine wawili kusimamia fainali hiyo.
MCHEZAJI WA LIGI KUU UINGEREZA JELA!
Mchezaji wa NEWCASLTE, JOEY BARTON, leo amefungwa miezi 6 jela baada ya kuhukumiwa kufuatia kukamatwa kwake 27 Desemba 2007 huko Liverpool baada ya kuwapiga watu. Ingawa alikuwa nje kwa dhamana, Joey Barton alikubali makosa yake mwezi uliopita na leo ndio ilikuwa hukumu.
Klabu yake ya NEWCASTLE imetoa taarifa kuwa imesikia hukumu hiyo na kwa wakati huu hawazungumzi lolote.









PATASHIKA PICHANI KUELEKEA FAINALI YA KESHO LUZHNIKI STADIUM, MOSCOW=




MAN UNITED vs CHELSEA
SANAMU YA MWANAMAPINDUZI WA KIRUSI VLADIMIR LENIN NJE YA UWANJA WA LUZHNIKI, MOSCOW .


WACHEZAJI WA MAN U WAKIWA KWENYE NDEGE KUELEKEA MOSCOW, URUSI HAPO JANA.




UWANJA WA LUZHNIKI, MOSCOW UTAKAOCHEZWA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA KATI YA MAN UNITED NA CHELSEA HAPO KESHO UMELETA WASIWASI MKUBWA !!!!!!
KIWANJA HICHO AMBACHO AWALI KILIKUWA NA MAJANI YA BANDIA WAKATI WA MECHI YA MTOANO YA EURO 2008 KATI YA URUSI NA UINGEREZA MWEZI OKTOBA MWAKA JANA ILIBIDI KUNG'OLEWA MAJANI HAYO BANDIA NA KUPANDWA MAJANI ASILI BAADA YA MECHI HIYO.
LAKINI MAJANI HAYO HAYAKURIDHISHA NA KAMA SIKU 15 ZILIZOPITA YAKALETWA MAJANI MAPYA TOKA SLOVAKIA NA KUPANDWA MITHILI YA VIPANDE VYA MARUMARU [ONA PICHA].
HATA HIVYO MTAALAM MSIMAMIZI WA KAZI HIYO, MWINGEREZA MATT FROST, HAKUFURAHISHWA NA KAZI HIYO NA ALILAUMU SANA NAMNA YA USAFARISHAJI WA NYASI HIZO.
INGAWA AMESEMA KIWANJA KINACHEZEKA ILA PICHA ZA TELEVISHENI ZITAONYESHA SEHEMU KAMA ZIMEKAUKA NA KUUKOSA ULA UKIJANI ASILIA WA MAJANI.
CHAMA CHA MPIRA CHA ULAYA, UEFA, KIMETAMKA UWANJA UNACHEZEKA.
Powered By Blogger