REFA AMBAYE 2005 CHELSEA WALIDAI AMEWAFUNGISHA GOLI LA MAZIMWI KESHO KUCHEZESHA FAINALI!
MIZUKA YA KLABU BINGWA ULAYA IMEIBUKA VIBAYA KWA CHELSEA BAADA YA REFA ALIEIFUNGISHA VIRAGO TIMU HIYO KATIKA NUSU FAINALI YA MASHINDANO HAYO MWAKA 2005 WALIPOTELEWA NA LIVERPOOL HUKO ANFIELD KWA BAO LA UTATA LA LUIS GARCIA KUPANGWA KUCHEZESHA KESHO KATIKA FAINALI YA KLABU BINGWA ULAYA DHIDI YA MAN U HUKO UWANJA WA LUZHNIKI MJINI MOSCOW, URUSI.
Refa huyo, Lubos Michel na msaidizi wake, Roman Slysko, wamekuwa wakichukiwa na Chelsea tangu waliporuhusu hilo bao la LIVERPOOL.
Meneja wa Chelsea wakati huo, JOSE MOURINHO, alikasirika na kusema: 'LILIKUWA GOLI LILILOTOKA MWEZINI. GOLI LA KIZIMWI'.
ILIDAIWA MPIRA HUO HAUKUVUKA MSTARI WA GOLI INGAWA MSAIDIZI WA REFA ALIASHIRIA NI GOLI. HATA HIVYO ILIONEKANA DHAHIRI KIPA WA CHELSEA PETR CECH AKIMCHEZEA MFUNGAJI RAFU NA BAADAE REFA HUYO ALINUKULIWA AKISEMA KAMA MSAIDIZI WAKE ASINGESEMA HILO NI GOLI BASI LAZIMA AGEMPA KADI NYEKUNDU CECH NA KUTOA PENALTI.
Lubos Michel na Roman Slysko wataungana na Waslovakia wengine wawili kusimamia fainali hiyo.
No comments:
Post a Comment