Friday 23 May 2008



SIR ALEX FERGUSON AFOKA NA KUISHUTUMU REAL MADRID JUU YA RONALDO!!
Awaita ni WAKOSA MAADILI!


Meneja wa MAN U, Sir Alex Ferguson ameishutuma vikali Klabu ya Spain, REAL MADRID, kwa kukosali maadili, utu na nidhamu.

Kocha wa REAL, Bernd Schuster na Rais wa Klabu hiyo, Ramon Calderon, wote wamekaririwa wakidai watamsajili RONALDO msimu huu.

Ferguson alifoka:'Schuster anabwabwaja na Calderon anabwabwaja'

'REAL wanadhani wanaweza wakazifosi timu ila wakae wakijua kwetu hawawezi. Barcelona ni Klabu ya kiungwana kuliko REAL ambayo ni wakosa maadili. REAL wanafikiri wanaweza kutumia Gazeti la Spain, MARCA, kuwachota akili wachezaji.'

Ferguson aliendelea:'Hivi mnafikiri Klabu nyingine kubwa Ulaya hazitaki wachezaji wetu? Wanataka ila ni waungwana na hawatangazi ovyo nia zao kama hao wapuuzi wa REAL. Wakae wakijua RONALDO bado ana mkataba wa miaka minne.'

'Huyo Calderon anadai biashara ya utumwa iliondolewa miaka 100 nyuma! Si wangemwambia Jenerali Franco basi?' [JENERALI FRANCO ALIKUWA MTAWALA DHALIMU NA DIKTETA WA SPAIN MIAKA YA NYUMA].

No comments:

Powered By Blogger