Saturday, 7 June 2008


EURO 2008 INAANZA LEO SAA 1 USIKU:
Wenyeji USWISI kuwavaa CZECH!
Mashindano ya 13 ya kuwania Kombe la Mataifa ya Ulaya ambayo mwaka huu yanachezwa katika nchi mbili zinazopakana, Switzerland na Austria, safari hii yakiitwa EURO 2008, yanaanza leo SAA 1 USIKU kwa mechi baina ya wenyeji USWISI na CZECH kwenye Uwanja wa ST JAKOB-PARK, mjini Basel, Uswisi.
Timu hizi zimeshawahi kupambana mara 30 hapo nyuma huku Czech wakishinda mara 16 na Uswisi mara 8.
Vikosi vya kila timu ni kama ifuatavyo:
SWITZERLAND
Meneja: Jakob ‘Kobi’ Kuhn
Kepteni: Alexander Frei
Diego Benaglio (Wolfsburg), Pascal Zuberbuehler (Neuchatel Xamax), Eldin Jakupovic (Grasshoppers Zurich), Ludovic Magnin (Stuttgart), Christoph Spycher (Eintracht Frankfurt), Philippe Senderos (Arsenal), Patrick Mueller (Olympique Lyon), Johan Djourou (Arsenal), Stephane Grichting (Auxerre), Philipp Degen (Borussia Dortmund)Stephan Lichtsteiner (Lille), Valon Behrami (Lazio), Gokhan Inler (Udinese)Gelson Fernandes (Manchester City), Benjamin Huggel (Basel), Tranquillo Barnetta (Bayer Leverkusen), Hakan Yakin (Young Boys Berne), Ricardo Cabanas (Grasshoppers Zurich), Johan Vonlanthen (Salzburg), Daniel Gygax (Metz), Alex Frei (Borussia Dortmund), Marco Streller (Basel), Eren Derdiyok (Basel
CZECH
Meneja: Karel Bruckner
Kepteni: Nafasi tupu baada ya Kepteni wao Tomas Rosicky [mchezaji wa ARSENAL kuumia]
Petr Cech (Chelsea), Jaromir Blazek (Nuremberg), Daniel Zitka (Anderlecht), Zdenek Grygera (Juventus), Marek Jankulovski (AC Milan), Michal Kadlec (Sparta Prague)Zdenek Pospech (Copenhagen), David Rozehnal (Lazio), Rudi Skacel (Southampton)Tomas Ujfalusi (Fiorentina), Tomas Galasek (Nuremberg), David Jarolim (Hamburg)Radoslav Kovac (Spartak Moscow), Marek Matejovsky (Reading), Jaroslav Plasil (Osasuna), Jan Polak (Anderlecht), Tomas Sivok (Sparta Prague), Milan Baros (Lyon), Martin Fenin (Frankfurt), Jan Koller (Nuremberg), Libor Sionko (Copenhagen), Vaclav Sverkos (Banik Ostrava), Stanislav Vlcek (Anderlecht)
MECHI YA PILI LEO JUMAMOSI 7 JUNI 2008 ni SAA 3 DAKIKA 45 [SAA ZA BONGO]:
URENO VS UTURUKI
Uwanja wa STADE DE GENEVE, mjini Geneva, Uswisi
VIKOSI:
PORTUGAL
Meneja: Luiz Felipe Scolari
Kepteni: Hawana Kepteni ingawa Cristiano Ronaldo anatajwatajwa.
Ricardo Pereira (Real Betis), Quim Silva (Benfica), Rui Patricio (Sporting), Miguel Monteiro (Valencia), Jose Bosingwa (Porto, anajiunga Chelsea msimu ujao), Paulo Ferreira (Chelsea), Ricardo Carvalho (Chelsea), Fernando Meira (VfB Stuttgart), Bruno Alves (Porto), Pepe (Real Madrid), Jorge Ribeiro (Boavista), Raul Meireles (Porto), Joao Moutinho (Sporting), Deco (Barcelona), Armando Petit (Benfica), Miguel Veloso (Sporting), Cristiano Ronaldo (Manchester United), Simao Sabrosa (Atletico Madrid)Ricardo Quaresma (Porto), Nuno Gomes (Benfica), Hugo Almeida (Werder Bremen)Nani (Manchester United), Helder Postiga (Panathinaikos
TURKEY
Meneja: Fatih Terim
Kepteni: EmreVolkan Demirel (Fenerbahce), Rustu Recber (Besiktas), Tolga Zengin (Trabzonspor)Sabri Sarioglu (Galatasaray), Gokhan Zan (Besiktas), Emre Asik (Ankaraspor), Servet Cetin (Galatasaray), Hakan Kadir Balta (Galatasaray), Ugur Boral (Fenerbahce), Emre Gungor (Galatasaray), Mehmet Aurelio (Fenerbahce), Mehmet Topal (Galatasaray)Emre Belozoglu (Newcastle United), Tumer Metin (Larissa), Hamit Altintop (Bayern Munich), Ayhan Akman (Galatasaray), Arda Turan (Galatasaray), Tuncay Sanli (Middlesbrough), Kazim Kazim (Fenerbahce), Gokdeniz Karadeniz (Rubin Kazan)Nihat Kahveci (Villarreal), Semih Senturk (Fenerbahce), Mevlut Erdinc (Sochaux
MECHI ZA KESHO JUMAPILI 8 JUNI 2008:
Austria v Croatia Vienna, SAA 1 USIKU
Germany v Poland Klagenfurt, SAA 3.45 USIKU


TETESI ZA LEO!
  • Emmanuel Adebayor atapewa mkataba mpya na Arsenal baada ya kuthibitisha atabakia na the Gunners. Inasemekana AC Milan, Inter Milan na Barcelona zilkuwa zinamnyatia.
==
  • Kiongozi wa Chelsea Peter Kenyon amepaa kwenda Italy kujaribu kumbembeleza Kocha wa AC Milan Carlo Ancelotti ahamie Stamford Bridge na awe Meneja.
==
  • Manchester United wamewashitaki Real Madrid kwa FIFA kwa kujaribu kumrubuni Ronaldo ajiunge nao kinyume cha sheria.
    Nae mama mzazi wa Ronaldo, Bibi Dolores Aveiro amemtaka mwanawe abakie Old Trafford.

***************************************************************************

Friday, 6 June 2008


Mutu aamrishwa kuilipa Chelsea £9.6m
Mshambuliaji wa Romania Adrian Mutu ameamriwa na FIFA jana kuilipa Chelsea Pauni za Kiingereza milioni 9 na laki 6 kama fidia baada ya kugundulika ametumia madawa ya kulevya aina ya cocaine mwaka 2004 na hatimaye kufukuzwa klabuni hapo.
Chelsea walimnunua Mutu kutoka Parma mwaka 2003 kwa Pauni milioni £15 na kumtimua Oktoba 2004 baada ya kashfa hiyo ya madawa ya kulevya kugundulika na ambayo ilisababisha afungiwe miezi saba kucheza soka.
***************************************************************************************
Adebayor akanusha kuhama
Mshambuliaji wa kutegemewa wa Arsenal amekanusha habari zilizogaa kwamba yuko njiani kumfuata mchezaji mwingine aliehama Arsenal Mathieu Flamini na kujiunga na Klabu ya Serie A ya Italia Inter Milan.
Adebayor ametamka: 'Ni upuuzi mtupu kwani sihami na niko kwenye timu nzuri hapa na nina furaha. Tulikuwa na msimu mzuri na msimu ujao tutatwaa vikombe.'


*************************************************************************************
Barca wamuuza Giovani kwa Tottenham
Mchezaji wa miaka 19 Giovani raia wa Mexico amesaini mkataba wa miaka mitano na Tottenham Hotspurs kwa dau la Pauni za Kiingereza milioni 4 laki 7.
Giovani, ambae ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Brazil Zizinho alikulia Barcelona alipoaanzia timu ya watoto.
SAKATA LA RONALDO!

Rio - Ronaldo lazima abaki

Rio Ferdinand ambae katika kipindi cha kuelekea mwisho wa msimu alikuwa ndie Nahodha wa Manchester United amemtaka Cristiano Ronaldo abaki MAN U na akatamka:' Timu hii itakuwa bora lakini lazima tuwe pamoja. Tumefanya kazi kwa bidii kufika hapa na tunataka kujenga mafanikio tulopata. Maana yake ni tubaki na wachezaji wetu walewale.'

Globaleyes==SAPOTA MAN U ABATUKA!
Haya tumeanza tena.
Mie ni nazi wa muda mrefu wa MAN U ambae nilimshabikia Ronaldo tangu alipotua Old Trafford akiwa mbavu za mbwa mpaka leo anaonekana mchezaji bora duniani aliefunga goli 42 kupita hata Alan Shearer alivyomudu maishani LIGI KUU.
Baada ya kutamka hivyo, ukweli ni kwamba leo mtizamo wangu kwake umebadilika. Msimamo na tabia yake siku hizi za karibuni zimenikera sana kwani amejionyesha yeye ni kama CD asiyekuwa hana hata chembe ya maadili ya kazi ya u-CD!
Na nikizungumza kama mtu nilieishi Spain, huo wenda wazimu wake wa kutaka kwenda Real unaonyesha kabisa hana akili. Angekuwa na akili kidogo tu agegundua Real ni mahala ambapo kumejaa wehu, wachezaji choka mbaya kiuchezaji, wala hongo, mafuska na wasiopendana huku uongozi wa klabu umenawiri ndumilakuwili, wanafiki, mafisadi na washenzi ambao labda ungewakuta katika Hekalu la Mfalme wa Karne ya 16. Au katika Klabu ya Chelsea ya sasa.
Akitaka kuhama- mwache ahame. Lakini kwanza agande na kuoza benchi mpaka Januari mwakani. Na asiondoke bila kulipwa Pauni za Kiingereza Milioni 100- isipungue hata ndururu!!!
Si wanamtaka basi yawatokee puani!!!

KINDUMBWENDUMBWE KESHO KINAANZA!
Saa moja usiku kesho mjini Basel, Switzerland, wenyeji SWITZERLAND watafungua pazia la UBINGWA WA MATAIFA YA ULAYA yaitwayo EURO2008 kwa kupambana na CZECH katika Uwanja wa ST JAKOB-PARK.

Baadae SAA 3 DAKIKA 45 usiku huo huo mjini Geneva katika Uwanja wa STADE DE GENEVE, URENO watapambana na UTURUKI.

Mechi zote hizi mbili za ufunguzi ni za la KUNDI A.
Ronaldo avunja ukimya!
Winga wa Man U akubali anataka kujiunga Real ila kauli yake ni fumbo la utata!!

Tovuti ya Kibrazil iitwayo Terra imeripoti kumnukuu Ronaldo wakati akiwa kwenye kambi ya Timu yake ya Taifa ya Ureno huko nchini Uswisi mjini Neuchatel akijitayarisha kwa Fainali za EURO 2008 akisema: ‘Nataka kuchezea Real Madrid ikiwa tu ni kweli wako tayari kunilipa mimi na Manchester United kile wanachosema watalipa. Lakini, hii haitegemei kwangu. Ni muhimu kutuma ujumbe. Kuanzia sasa sizungumzi tena kuhusu hili mpaka mwisho wa EURO. Hamna faida kuniuliza swali kwani sitojibu.’

WADAU WAJITOSA KWENYE MJADALA:

Scotty Stevens (shabiki wa Manchester United) anasema...

Nakumbuka juzi tu Ronaldo katamka anataka kuwa staa wa MAN U kama kina George Best, Bobby Charlton, Cantona nk. Yeye kacheza miaka mitano tu na watu watamsahau! Moyoni namkumbuka sana na kumthamini sana Cantona aliechezea miaka minne na nusu tu na hakuwahi kuchukua Kombe la Ulaya!

John Clarke anena..

Kwaheri Ronaldo. Ulaghai wako wa kujiangushaangusha utapendwa sana huko Uhispania kwani ndio tabia yao! Ulafi na Pesa ndio mzizi wa mabaya yote duniani! Mie si mnazi wa ManU lakini nakubaliana na wote kwamba United ndio Klabu kubwa Ulaya na kuhama kwako ni kushuka ngazi. Nenda na potelea mbali!!

Thomas Vince (shabiki wa Arsenal) apasua...

Atakuwa mchezaji bora duniani akibaki Manchester United! Lakini huwezi kuwa na mchezaji asiekuwa na motisha na mapenzi klabuni kwako! Atafanya walichofanya Anelka na Thierry Henry na wengine wote waroho waliohamia Spain na wakadoda na hawakung’ara tena! Acheni ende na atajuta!. --


Okocha aondolewa Hull City

Jay-Jay Okocha ametemwa na Hull City, timu mpya iliyopanda daraja kuingia LIGI KUU UINGEREZA, aliyojiunga nayo Septemba 2007 akitokea timu ya Qatar SC ya Qatar. Tangu alipojiunga na Hull City Okocha alicheza mechi 11 tu kwa kuwa majeruhi.
Hull City imepanda daraja kwenda LIGI KUU pamoja na timu za West Bromwich Albion na Stoke City.
Kabla ya kwenda Qatar, Okocha aliichezea Bolton Wanderers tangu Julai 2002 na alishiriki mechi 106 za LIGI KUU UINGEREZA na kufunga magoli 14 katika miaka minne aliyokuwa na timu hiyo.
Okocha alijiunga na Bolton akitokea Paris St Germain ya Ufaransa na ameichezea Timu ya Taifa ya Nigeria mara 70 na kushiriki katika Fainali za Kombe la Dunia mara tatu.

Thursday, 5 June 2008

MPIRA UTAKAODUNDA EURO 2008: ADIDAS 'EUROPASS'
Mpira utakaochezewa katika michuano ya EURO 2008 unaitwa ADIDAS “EUROPASS” na una rangi nyeupe na mabaka 12 meusi na nyongeza ya rangi ya fedha na nyekundu pamoja na bendera za Mataifa ya wenyeji wa mashindano Switzerland na Austria.

Mpira huu ambao umetengenezwa na Kampuni ya ADIDAS umeundwa kutoka vipande 14 kwa teknolojia ya kisasa kabisa. Mpira huu umepewa jina la “EUROPASS” kwa sababu mbili. Ya kwanza ni kumaanisha bonde la mpakani kati ya nchi hizi mbili wenyeji wa mashindano haya ya EURO 2008 yaani Switzerland na Austria.
Ya pili ni msisitizo wa pasi za uhakika za mpira katika mechi zenyewe.
Ngozi ya nje ya mpira huu imeundwa mahsusi na ina ‘vipele’ vidogo vitakavyosaidia usiteleze wakati unapopigwa au kudakwa na makipa huku ukichezeka vizuri tu katika hali zote za hewa iwe mvua, barafu au jua.

Majaribio ya mpira huu yalifanyika katika Chuo Kikuu cha Loughborough nchini Uingereza na katika Maabara Maalum ya Kampuni ya Adidas mjini Scheinfeld huko Ujerumani.
SHINAWATRA NA ERIKSSON
Mmiliki wa Manchester City Thaksin Shinawatra, ambae alikuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand, ametoa ufafanuzi kwanini alimtimua Sven Goran Eriksson kwa kudai Meneja huyo hakutoa mchango wa kutosha kuiinua timu.
Shinawatra alisema: 'Eriksson ni jemedari mzuri sana wa soka lakini tulikuwa tunataka zaidi. Lazima tucheze kwa ubora na uhakika zaidi. Awamu ya pili ya LIGI KUU tulikuwa dhaifu sana, tena sana! Tulibamizwa 8-1 na Middlesbrough katika mechi ya mwisho!!! Aibu, aibu kubwa!!!'
Shinawatra sasa amemwajiri aliekuwa Meneja wa Blackburn Rovers Mark Hughes kuendesha jahazi wakati Eriksson amevuka bahari ya Atlantic kwenda Mexico kuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya nchi hiyo.
MANCHESTER UNITED KUJA AFRIKA MWEZI UJAO MABINGWA WA ULAYA na LIGI KUU UINGEREZA MAN U watashuka bondeni Afrika Kusini kati ya Julai 19 na 26 mwaka huu kucheza mechi tatu na Klabu za Afrika Kusini za Kaiser Chiefs and Orlando Pirates.
Wakiwa njiani kurudi Uingereza watatua mjini Abuja, Nigeria kucheza mechi ya maonyesho na Mabingwa wa Kombe la FA la Uingereza Portsmouth ambayo pia imo LIGI KUU UINGEREZA.
"Utafiti umeonyesha Nigeria ni nyumbani kwa mashabiki wetu milioni 13 na ni ya nne kwa kuwa na mashabiki wengi" alikaririwa Mkurugenzi Mkuu wa Man U David Gill na akaongeza: "Ziara hii ni kutoa shukrani zetu za dhati kwa mashabiki hao. Wachezaji wetu wote muhimu watakuwepo isipokuwa wale wanaocheza EURO 2008 kwani wamepewa muda wa nyongeza wa likizo"
Mechi hiyo ya mjini Abuja pengine ni majaribio mazuri kwa timu hizi za Man U na Portsmouth kwani pia zitakutana katika mechi ya kufungua rasmi msimu wa soka wa Uingereza wa mwaka 2008/09 zitakapoingia Wembley tarehe 10 Agosti 2008 kuwania NGAO YA HISANI.
NGAO YA HISANI ni mechi ya kufungua pazia msimu mpya wa soka wa Uingereza na huchezwa kati ya BINGWA LIGI KUU na BINGWA WA KOMBE LA FA wiki moja kabla msimu haujaanza.
Msimu uliopita MAN U alinyakua UBINGWA wa LIGI KUU na Portsmouth alitwaa KOMBE LA FA.

Porto wapoteza nafasi LIGI YA MABINGWA ULAYA
Mabingwa wa Ureno Porto wamapigwa marufuku na Chama cha Soka Ulaya UEFA kushiriki michuano ya LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA kwa msimu ujao kufuatia kuthibitishwa kwao kushiriki kuhonga Marefa katika msimu wa mwaka 2003/04.
Tuhuma hizi zinahusu mechi za Porto waliposhinda 2-0 dhidi ya Estrela da Amadora na suluhu ya 0-0 na Beira Mar.
Porto walishinda Ubingwa wa nchi yao na pia kunyakua Kombe la KLABU BINGWA ULAYA katika msimu huo wa 2003/04 wakiwa chini ya Kocha Jose Mourinho ambae hakuhusishwa chochote na tuhuma hizo za rushwa.
Porto imesema itakata rufaa.
Mwezi uliopita, Porto walipatikana na hatia ya kuhonga katika mechi hizo mbili za LIGI YA URENO na wakapigwa faini ya takriban Shilingi za kibongo bilioni 270 na kupunguzwa pointi 6 kwenye msimamo wa ligi ingawa adhabu ya kukatwa pointi haikuwazuia kunyakua Ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo wakiwa mbele ya Sporting Lisbon kwa pointi 14.

GUMZO…uvumi na tetesi………za leo!!!!!

  • Meneja wa Roma Luciano Spalletti ameungana na Mtaliana mwenzake Carlo Ancelotti kukataa ofa ya kujiunga na Klabu ya Chelsea inayohaha kupata bosi mpya tangu wamtimue Avram Grant .


 

  • Nae Didier Drogba hayumo kwenye listi ya wanaotakiwa kwenda kumfuata Inter Milan Jose Mourinho kwani listi ya bosi huyo mpya haina mshambuliaje yeyote!


     

  • Juventus wameshaafikiana na kiungo wa Liverpool Xabi Alonso malupulupu yake binafsi ila kuna mvutano kati ya Klabu na Klabu kuhusu ada ya uhamisho huku Wekundu hao wakitaka Pauni za Kiingereza milioni 16 wakati Wataliana hao wako tayari kutoa Pauni milioni 14.5 za Kiingereza.


     


 


 

Wednesday, 4 June 2008

Habari mpya 4 juni 2008





Hughes atua Man City kama Meneja

Mark Hughes ameteuliwa kuwa Meneja wa Manchester City kwa mkataba wa miaka mitatu kuchukua nafasi ya Eriksson aliefukuzwa juzi.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United na Chelsea alikuwa Meneja wa Blackburn Rovers kwa miaka mitatu na nusu na aliwezesha Blackburn kumaliza msimu uliopita wa LIGI KUU UINGEREZA kwenye nafasi ya saba. Vilevile, aliiwezesha Blackburn kufika Nusu Fainali ya Kombe la FA mara mbili mnamo miaka ya 2004 na 2007.***************

Sagna asaini mkataba mpya Arsenal
Beki wa kulia wa Arsenal Bacary Sagna amesaini mkataba mpya ambao Klabu hiyo wameuita wa muda mrefu.
Beki huyo mwenye miaka 25 alijiunga na the Gunners kutoka Auxerre ya Ufaransa mwanzoni mwa msimu uliopita na aliichezea Arsenal mechi 40 katika msimu wa 2007/08.



GUMZO……uvumi na tetesi………………..za leo!!!!
Mameneja wa Kitaliana wa Roma Luciano Spalletti na wa Fiorentina Cesare Prandelli ni majina yaliyojitokeza kuchukua nafasi ya Umeneja iliyo wazi ya Klabu ya Chelsea baada ya Mtaliana mwingine Bosi wa AC Milan Carlo Ancelotti kutamka yeye atabaki AC Milan. Chelsea wanatafuta Meneja baada ya kumtimua Myahudi Avram Grant.

xxxxxxxxxxxx
Jose Mourinho, Bosi mpya wa Inter Milan, anasemekana amemuweka mlinzi wa Chelsea Ashley Cole kama mchezaji wa kwanza atakaemleta kwenye Klabu yake hiyo mpya. Itakumbukwa ni Mourinho aliemng’oa Ashley Cole Arsenal na kumpeleka Chelsea wakati alipokuwa Meneja wa Chelsea.
xxxxxxxxxxx


Winga wa Kireno Cristiano Ronaldo inadaiwa amesema ataihama Manchester United ndani ya mwaka mmoja na kutimiza ndoto yake ya kuhamia Real Madrid.
xxxxxxxxxx

Mark Hughes, Meneja wa sasa wa Blackburn Rovers, amefikia makubaliano ya mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Pauni za Kiingereza milioni 9 ili kuwa Meneja mpya wa Manchester City.
xxxxxxxxxx
Hoteli moja mjini Manchester ina kilio baada ya kusikia Sven-Goran Eriksson anaondoka Man City kwenda Mexico kwani alikuwa anaingizia hoteli hiyo Pauni za Kiingereza £350,000 kwa mwezi kama gharama ya makazi yake ya kifahari hotelini hapo.
xxxxxxxxxx

Arsene Wenger amedai Arsenal itashinda kila kitu msimu ujao.


Eriksson ateuliwa Meneja wa Mexico

Baada ya kufukzwa kazi Manchester City juzi Jumatatu, Sven-Goran Eriksson amepata kazi ya kuiongoza Timu ya Taifa ya Mexico kwa mkataba wa miaka miwili.

Kabla ya kuwa Meneja wa Man City, Sven-Goran Eriksson alikuwa Meneja wa Uingereza kwa miaka mitano na nusu kuanzia Januari, 2001 hadi Julai, 2007 ambapo aliiwezesha Uingereza kuingia Robo Fainali za Kombe la Dunia mara mbili.

Mexico kwa sasa wako kwenye mtoano wa kupata nafasi ya kucheza Kombe la Dunia la 2010 huko Afrika Kusini.

*******************************************************


Lehmann asaini mkataba na Stuttgart

Kipa wa Arsenal Jens Lehmann amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Klabu ya Ujerumani ya VFB Stuttgart.
Mkataba wa Kipa huyo mwenye umri wa miaka 38 na Arsenal utaisha hivi karibuni na tayari alishapoteza namba kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya nafasi yake kuchukuliwa na Manuel Almunia.

Lakini kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Ujerumani ambacho kitacheza michuano ya EURO 2008 inayoanza Jumamosi huko Switzerland na Austria, kipa huyo bado ni nambari wani.

Tuesday, 3 June 2008

Italy watikiswa na kuumia Kepteni Cannavaro!!!
Ataikosa EURO 2008!
Nahodha wa Italy Fabio Cannavaro ataikosa Euro 2008 baada ya kuumia kisigino kwenye mazoezi.
Mlinzi huyo wa Klabu ya Real Madrid aligongana na Giorgio Chiellini katika mazoezi kwenye kambi ya timu hiyo nchini Austria hapo jana.
Mchezaji wa Fiorentina Alessandro Gamberini ameitwa kuchukua nafasi ya Cannavaro katika michuano hiyo ya Euro 2008 inayoaanza Jumamosi na Kipa Gianluigi Buffon anasemekana atapewa Unahodha wa Italy.
Cannavaro, 34, amechezea Timu ya Taifa ya Italy mara116 na alikuwa Nahodha Italy walipochukua Kombe la Dunia huko Ujerumani mwaka 2006 na mwaka huohuo akachukua Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani.
Pengo la Cannavaro ni kubwa kwani Italy wako kwenye 'Kundi la Kifo' ambalo timu nyingine ni Ufaransa, Uholanzi na Romania.
Hata hivyo Italy watawategemea Andrea Barzagli, Marco Materazzi, Chiellini na Christian Panucci kuziba ufa huo.
Italy watacheza mechi yao ya kwanza dhidi ya Uholanzi Jumatatu tarehe 9 June mjini Berne, Switzerland.
*********************************************************************************
Beckham amuasa Ronaldo abaki MAN
Nyota wa zamani wa Manchester United David Beckham amemtaka Cristiano Ronaldo asifuate nyayo zake na kuondoka Old Trafford kujiunga Real Madrid.
Mafahali hao wa Uhispania wanamuwania Ronaldo ingawa wameshapewa onyo kali na Sir Alex Ferguson.
Beckham, aliejiunga Real mwaka 2003 akitokea MAN U, amesema: "Naamini yuko katika Klabu nzuri na Klabu anayostahili kubaki. Kwanza yuko hapo kwa miaka michache tu na kuna watu wazuri wengi watakaomlinda na kumlea.'
Beckham akaongeza: "Ingawa Real ni timu nzuri na moja ya Klabu kubwa duniani, Ronaldo bado chipukizi."
Beckham alimaliza kwa kutamka Ronaldo anastahili Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani mwaka huu.

TETESI NA UVUMI…………wa leo!!!!
=Manchester City wanahaha kumsaini Ronaldinho toka Barcelona na wako tayari kumlipa mshahara wa Pauni za Kiingereza laki £200,000-kwa wiki.


=Mourinho ambae ni Meneja mpya wa Inter Milan anataka kuwachukua wachezaji wake wa zamani toka Chelsea Ricardo Carvalho, Michael Essien and Frank Lampard kuwaleta Inter.


=Fabio Capello, Meneja wa Timu ya Taifa ya Uingereza, anasemekana atamchagua Nahodha wa kudumu wa Timu hiyo kati ya John Terry au Rio Ferdinand.


=Nicolas Anelka anajuta kwanini aliondoka Arsenal kujiunga na Real Madrid mwaka1999 na amesema ni bora angekuwa na Gunners kwa kipindi hiki chote.



Mourinho aukwaa Umeneja Inter Milan!

Bosi wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho ameteuliwa kuwa Meneja wa Klabu ya Serie A Inter Milan.
Mourinho amesaini mkataba wa miaka mitatu ikiwa ni kazi yake ya kwanza tangu atimuliwe Chelsea Septemba 2007.
Mourinho,45, anamrithi Roberto Mancini aliefukuzwa kazi majuzi mbali ya kuipa Inter Ubingwa wa Serie A mara tatu mfululizo ikiwa pamoja na msimu huu.
Mourinho atatangzwa rasmi leo saa 6 mchana mbele ya Waandishi habari.
**************************************************************************************

Nae Eriksson amwaga unga MAN CITY!!
Manchester City wamemtimua Meneja Sven-Goran Eriksson kwa amri ya mmiliki wa Klabu hiyo aliekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand Thaksin Shinawatra mbali ya kuiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya 9 katika LIGI KUU UINGEREZA.
Man City tayari washaomba kibali toka kwa Blackburn Rovers ili wafanye mazungumzo na Meneja wao Mark Hughes ili wakikubaliana ahamie Man City. Blackburn Rovers wamekubali ombi hilo na kuna uwezekano mkubwa Mark Hughes akahama.

Sunday, 1 June 2008



Ferguson aonya kuhusu Ronaldo
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema klabu iko tayari Cristiano Ronaldo asicheze na badala yake akae vitini kama mtazamaji kuliko kumuuza kwa Real Madrid.
Man United tayari wameshatoa onyo kali kwa Real kuwa watawashitaki FIFA kwa kumrubuni Ronaldo kinyume na taratibu.
Ferguson amekutana na familia ya Glazer ambao ndio wanamiliki klabu na amesema:"Wao wana msimamo 'POTELEA MBALI NA TUKO TAYARI MCHEZAJI AKAE JUKWAANI KULIKO KUMUUZA'. Wako tayari kufanya hivyo ili kuonyesha msimamo kuwa sisi si klabu ya kuuza wachezaji wetu bora!'
Ronaldo, 23, kwa sasa yuko na kikosi cha Portugal kinachojitayarisha na Euro 2008 baada ya msimu bora ulioifanya Old Trafford iwe nyumbani mwa makombe ya LIGI KUU UINGEREZA na KLABU BINGWA BARANI ULAYA huku yeye akiwa ndio mfungaji bora katika Makombe yote mawili.

Mkataba wa Ronaldo unaisha 2012 na mwenyewe amesema ana furaha MAN U.
Baada ya onyo la MAN U kwa REAL kuwa watapelekwa FIFA, REAL walikuja hadharani na kutamka hawataki ugomvi na MAN U na hawawezi kumchukua mchezaji ambae klabu yake haitaki kumuuza.

********************************************************************************

TETESI NA UVUMI WA LEO..................................................

  • MAN U wako tayari na kitita cha pauni milioni 30 za Kiingereza kumnunua mshambuliaji chipukizi na mahiri wa LYON na Timu ya Taifa ya Ufaransa Karim Benzema.
  • Kiungo wa ARSENAL Alexander Hleb atajiunga na BARCELONA kwa dau la Pauni za Kiingereza milioni 12.
  • Mdogo wake Rio Ferdinand, mlinzi wa WEST HAM Anton Ferdinand yuko njiani kujiunga na TOTTENHAM.
Powered By Blogger