Thursday, 5 June 2008


Porto wapoteza nafasi LIGI YA MABINGWA ULAYA
Mabingwa wa Ureno Porto wamapigwa marufuku na Chama cha Soka Ulaya UEFA kushiriki michuano ya LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA kwa msimu ujao kufuatia kuthibitishwa kwao kushiriki kuhonga Marefa katika msimu wa mwaka 2003/04.
Tuhuma hizi zinahusu mechi za Porto waliposhinda 2-0 dhidi ya Estrela da Amadora na suluhu ya 0-0 na Beira Mar.
Porto walishinda Ubingwa wa nchi yao na pia kunyakua Kombe la KLABU BINGWA ULAYA katika msimu huo wa 2003/04 wakiwa chini ya Kocha Jose Mourinho ambae hakuhusishwa chochote na tuhuma hizo za rushwa.
Porto imesema itakata rufaa.
Mwezi uliopita, Porto walipatikana na hatia ya kuhonga katika mechi hizo mbili za LIGI YA URENO na wakapigwa faini ya takriban Shilingi za kibongo bilioni 270 na kupunguzwa pointi 6 kwenye msimamo wa ligi ingawa adhabu ya kukatwa pointi haikuwazuia kunyakua Ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo wakiwa mbele ya Sporting Lisbon kwa pointi 14.

No comments:

Powered By Blogger