Tuesday 3 June 2008

Italy watikiswa na kuumia Kepteni Cannavaro!!!
Ataikosa EURO 2008!
Nahodha wa Italy Fabio Cannavaro ataikosa Euro 2008 baada ya kuumia kisigino kwenye mazoezi.
Mlinzi huyo wa Klabu ya Real Madrid aligongana na Giorgio Chiellini katika mazoezi kwenye kambi ya timu hiyo nchini Austria hapo jana.
Mchezaji wa Fiorentina Alessandro Gamberini ameitwa kuchukua nafasi ya Cannavaro katika michuano hiyo ya Euro 2008 inayoaanza Jumamosi na Kipa Gianluigi Buffon anasemekana atapewa Unahodha wa Italy.
Cannavaro, 34, amechezea Timu ya Taifa ya Italy mara116 na alikuwa Nahodha Italy walipochukua Kombe la Dunia huko Ujerumani mwaka 2006 na mwaka huohuo akachukua Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani.
Pengo la Cannavaro ni kubwa kwani Italy wako kwenye 'Kundi la Kifo' ambalo timu nyingine ni Ufaransa, Uholanzi na Romania.
Hata hivyo Italy watawategemea Andrea Barzagli, Marco Materazzi, Chiellini na Christian Panucci kuziba ufa huo.
Italy watacheza mechi yao ya kwanza dhidi ya Uholanzi Jumatatu tarehe 9 June mjini Berne, Switzerland.
*********************************************************************************
Beckham amuasa Ronaldo abaki MAN
Nyota wa zamani wa Manchester United David Beckham amemtaka Cristiano Ronaldo asifuate nyayo zake na kuondoka Old Trafford kujiunga Real Madrid.
Mafahali hao wa Uhispania wanamuwania Ronaldo ingawa wameshapewa onyo kali na Sir Alex Ferguson.
Beckham, aliejiunga Real mwaka 2003 akitokea MAN U, amesema: "Naamini yuko katika Klabu nzuri na Klabu anayostahili kubaki. Kwanza yuko hapo kwa miaka michache tu na kuna watu wazuri wengi watakaomlinda na kumlea.'
Beckham akaongeza: "Ingawa Real ni timu nzuri na moja ya Klabu kubwa duniani, Ronaldo bado chipukizi."
Beckham alimaliza kwa kutamka Ronaldo anastahili Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani mwaka huu.

No comments:

Powered By Blogger