Baada ya kufukzwa kazi Manchester City juzi Jumatatu, Sven-Goran Eriksson amepata kazi ya kuiongoza Timu ya Taifa ya Mexico kwa mkataba wa miaka miwili.
Kabla ya kuwa Meneja wa Man City, Sven-Goran Eriksson alikuwa Meneja wa Uingereza kwa miaka mitano na nusu kuanzia Januari, 2001 hadi Julai, 2007 ambapo aliiwezesha Uingereza kuingia Robo Fainali za Kombe la Dunia mara mbili.
Mexico kwa sasa wako kwenye mtoano wa kupata nafasi ya kucheza Kombe la Dunia la 2010 huko Afrika Kusini.
*******************************************************
Lehmann asaini mkataba na Stuttgart
Kipa wa Arsenal Jens Lehmann amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Klabu ya Ujerumani ya VFB Stuttgart.
Mkataba wa Kipa huyo mwenye umri wa miaka 38 na Arsenal utaisha hivi karibuni na tayari alishapoteza namba kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya nafasi yake kuchukuliwa na Manuel Almunia.
Lakini kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Ujerumani ambacho kitacheza michuano ya EURO 2008 inayoanza Jumamosi huko Switzerland na Austria, kipa huyo bado ni nambari wani.
No comments:
Post a Comment