Thursday 5 June 2008

MANCHESTER UNITED KUJA AFRIKA MWEZI UJAO MABINGWA WA ULAYA na LIGI KUU UINGEREZA MAN U watashuka bondeni Afrika Kusini kati ya Julai 19 na 26 mwaka huu kucheza mechi tatu na Klabu za Afrika Kusini za Kaiser Chiefs and Orlando Pirates.
Wakiwa njiani kurudi Uingereza watatua mjini Abuja, Nigeria kucheza mechi ya maonyesho na Mabingwa wa Kombe la FA la Uingereza Portsmouth ambayo pia imo LIGI KUU UINGEREZA.
"Utafiti umeonyesha Nigeria ni nyumbani kwa mashabiki wetu milioni 13 na ni ya nne kwa kuwa na mashabiki wengi" alikaririwa Mkurugenzi Mkuu wa Man U David Gill na akaongeza: "Ziara hii ni kutoa shukrani zetu za dhati kwa mashabiki hao. Wachezaji wetu wote muhimu watakuwepo isipokuwa wale wanaocheza EURO 2008 kwani wamepewa muda wa nyongeza wa likizo"
Mechi hiyo ya mjini Abuja pengine ni majaribio mazuri kwa timu hizi za Man U na Portsmouth kwani pia zitakutana katika mechi ya kufungua rasmi msimu wa soka wa Uingereza wa mwaka 2008/09 zitakapoingia Wembley tarehe 10 Agosti 2008 kuwania NGAO YA HISANI.
NGAO YA HISANI ni mechi ya kufungua pazia msimu mpya wa soka wa Uingereza na huchezwa kati ya BINGWA LIGI KUU na BINGWA WA KOMBE LA FA wiki moja kabla msimu haujaanza.
Msimu uliopita MAN U alinyakua UBINGWA wa LIGI KUU na Portsmouth alitwaa KOMBE LA FA.

No comments:

Powered By Blogger