Saturday, 26 September 2009

LIGI KUU ENGLAND: Mvua ya Magoli yashuka!!! Chelsea atwangwa na Wigan, Man U kileleni, Liverpool na Tottenham washusha vipigo vitakatifu!!!
Wakati Mabingwa Watetezi Manchester United wakicheza ugenini huko Britannia Stadium na kuwafunga wenyeji wao Stoke City mabao 2-0, Chelsea nae alikuwa ugenini lakini akaambulia kipigo cha mabao 3-1 kwenye Uwanja wa DW toka kwa wenyeji wao Wigan huku Kipa wao Petr Cech akiwashwa Kadi Nyekundu na kutoa penalti baada ya kumwangusha Mshambiliaji wa Wigan, Hugo Rodalega, penalti ambayo ilifungwa na Rodallega mwenyewe na kuandika bao la pili kwa Wigan.
Wigan walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0 hadi mapumziko.
Kipindi cha pili Drogba aliisawazishia Chelsea lakini ndipo likaja tukio la Kipa Cech kutolewa nje na kutoa penalti iliyoipa Wigan bao la pili. Bao la 3 la Wigan lilifungwa na Pul Scharner.
Kipigo cha Chelsea kimewapa mwanya Man U kushika hatamu baada ya Mabingwa hao kuishinda Stoke City 2-0 mabao yaliyofungwa na Berbatov na John O’Shea.
Man U na Chelsea zote zimecheza mechi 7 na zina pointi 18 kila moja lakini Man U yuko mbele kwa tofauti ya magoli.
Liverpool ikiwa nyumbani Anfield iliibamiza Hull City mabao 6-1 huku nyota wao Fernando Torres akifunga mabao matatu, Babel bao 2 na Nahodha Gerrard bao 1.
Nao Tottenham waliisulubu Burnley kwa mabao 5-0 Wafungaji wao wakiwa Robbie Keane mabao manne na Jermaine Jenas bao 1.

MATOKEO KAMILI:
Liverpool 6 v Hull City 1
Stoke City 0 v Manchester United 2
Wigan 3 v Chelsea 1
Blackburn 2 v Aston Villa 1
Birmingham 1 v Bolton 2
Tottenham 5 v Burnley 0
Arsenal kuikwaa Liverpool Kombe la Carling
Katika Droo ya Raundi ya 4 ya Kombe la Carling, Arsenal wataikaribisha Liverpool Uwanjani Emirates na Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo, Manchester United, watacheza ugenini na Timu ya Daraja la Coca Cola Championship, Barnsley.
Mechi hizo za Raundi ya 4 zitachezwa Jumanne Oktoba 27 na Jumatano Oktoba 28.
Ratiba kamili ni:
Blackburn Rovers v Peterborough United
Manchester City v Scunthorpe United
Tottenham Hotspur v Everton
Barnsley v Manchester United
Chelsea v Bolton Wanderers
Sunderland v Aston Villa
Arsenal v Liverpool
Portsmouth v Stoke City

Portsmouth yapokea kipigo cha 7 mfululizo LIGI KUU!!!!
Wako mkiani bila pointi!!!
Portsmouth leo tena wameendelea kula kisago baada ya bao la dakika ya 42 la Luis Saha kuwapa ushindi Everton waliokuwa wakicheza ugenini katika mechi ya Ligi Kuu.
Hiki ni kipigo cha 7 mfululizo kwa Portsmouth na hawana pointi hata moja katika mechi 7 za ligi.
Hii ni mechi ya 6 kwa Everton na wameshinda mechi 3 na kufungwa mechi 3.
MECHI NYINGINE ZA LIGI KUU LEO Jumamosi Septemba 26 ni:
Liverpool v Hull City
Stoke City v Manchester United
Wigan v Chelsea
Blackburn v Aston Villa
Birmingham v Bolton
Tottenham v Burnley
Fulham v Arsenal
Jumapili, Septemba 27:
Sunderland v Wolverhampton
Jumatatu, Septemba 28:
Manchester City v West Ham
Powered By Blogger