Kikosi cha Wachezaji 22 cha Man United kwenda USA
Sir Alex Ferguson ataongoza Kikosi cha Wachezaji 22 Siku ya Jumatatu Julai 12 kwenda kwenye ziara ya Marekani, Canada na Mexico itakayomalizika Julai 30.
Kikosi hichi ni mchanganyiko wa Wakongwe na Chipukizi ambamo Wakongwe ni kina Edwin van der Sar, Ryan Giggs na Paul Scholes na Vijana ni kina Corry Evans, Ben Amos na Tom Cleverley.Wachezaji waliokuwa kwenye Kombe la Dunia huko Afrika Kusini, Wayne Rooney, Michael Carrick, Patrice Evra na Nemanja Vidic, hawatakuwemo kwani wapo likizo.
Mchezaji mpya ambae aliiwakilisha Mexico kwenye Kombe la Dunia, Javier Hernandez, atajiunga na wenzake Julai 27 huko Houston, USA.
Nahodha Gary Neville hatakuwemo kwenye Kikosi hicho kwa vile ana tatizo la musuli za mguu.
Man United watatua kwanza huko Chicago na kupiga kambi ya mazoezi na mechi yao ya kwanza itakuwa dhidi ya Celtic ya Scotland huko Toronto, Canada hapo Julai 16.
Halafu watasafiri hadi Philadelphia, USA kucheza na Philadelphia United hapo Julai 21 na Julai 25 watakuwa Kanasas City kucheza na Kansas City Wizards.
Kisha wataenda Houston kucheza na Kombaini ya Mastaa wa MLS, Ligi ya huko Marekani.
Ziara ya Man United itamalizikia huko Mexico Julai 30 watakapocheza na Timu ya zamani ya Javier Hernandez, Chivas, Mjini Guadalajara.
Kikosi kamili: Edwin van der Sar, Tomasz Kuszczak, Paul Scholes, Ryan Giggs, Dimitar Berbatov, John O'Shea, Wes Brown, Rafael, Jonny Evans, Darren Fletcher, Darron Gibson, Chris Smalling, Nani, Fabio, Federico Macheda, Danny Welbeck, Javier Hernandez (atajiunga Julai 27 huko Houston), Mame Biram Diouf, Tom Cleverley, Ritchie De Laet, Corry Evans, Ben Amos, Gabriel Obertan.