Thursday 8 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Pweza Mtabiri kuimarishiwa ulinzi!!
Yule Pweza, aitwae Paul, ambae anafugwa kwenye Zuu huko Ujerumani na ambae amekuwa akitabiri mechi za Fainali za Kombe la Dunia na kupatia matokeo ambapo juzi alitabiri kuwa Spain itaishinda Germany katika mechi ya Nusu Fainali na kweli Spain ikaifunga Germany 1-0, atawekewa ulinzi mkali baada ya kuzuka hofu kuna Watu wanamuwinda wamle ikiwa ni hasira ya Germany kufungwa.
Msimamizi wa Pweza huyo, Oliver Walenciak, amesema: “Wapo Watu wanataka kumla Pweza wetu! Sisi tupo kumlinda!”
Awali Mashabiki wa Argentina walimlaumu Pweza huyo kwa wao kupigwa 4-0 na Germany mechi ambayo pia alitabiri sawa sawa na wakatishia kumla.
Wenger kutoa tamko kuhusu Kipa Arsenal
Arsene Wenger amesema atatoa msimamo wake kuhusu nani atakuwa Kipa Nambari Wani wa Arsenal baada ya kukiri Kipa wa sasa Manuel Almunia huingiwa na mchecheto kwenye mechi kubwa.
Msaidizi wa Almunia ni Lukasz Fabianski lakini nae ameshindwa kumpiku Almunia kwani alipopata nafasi za kucheza amekuwa akifanya makosa makubwa yakiwemo makosa mawili kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI dhidi ya FC Porto Msimu uliokwisha.
Kumekuwa na tetesi Kipa wa Fulham Mark Schwarzer huenda akatua Ze Gunners.

No comments:

Powered By Blogger