Friday 9 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Kuyt: ‘Spain haitutishi!’
Dirk Kuyt ameiponda Germany kwa kucheza na woga walipokutana na Spain kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini na kutolewa kwa bao 1-0 na amedai kuwa Holland Jumapili kwenye Fainali wataingia kupambana na Spain wakiwa na nia ya kushambulia tu.
Holland wataingia mechi hiyo ya Fainali wakiwa hawajafungwa katika mechi zao 25 za mwisho huku wakiwa wameshinda mfululizo mechi 14 za Michuano ya Kombe la Dunia kuanzia hatua ya mchujo.
Kuyt amesema: “Hatuogopi hata chembe! Uliona Germany walivyowaogopa na nini kimewakuta. Sie tutashambulia na kasoro zao zitajitokeza. Hatuna Wachezaji waoga!”
Hii ni mara ya 3 kwa Holland kutinga Fainali za Kombe la Dunia lakini mara mbili walifungwa na kuukosa Ubingwa wa Dunia.
Nae Kocha wa Holland, Bert van Marwijk, amekiri kupata ushauri kutoka kwa Mastaa wa Uholanzi wa zamani kina Johan Cruyff na Ruud Gullit muda wote ambao wako Afrika Kusini.
Belhadj ahama Pompey kwenda Qatar
Beki wa Portsmouth kutoka Algeria, Nadir Belhadj, amejiunga na Klabu ya Qatar Al Sadd bila ya kutajwa dau na pia aina ya Mkataba.
Uhamisho huo umethibitishwa na Klabu hiyo ya Qatar ambayo imekiri walikuwa wakimwinda Belhadj kwa muda mrefu.
Belhadj, Miaka 28, alikuwa na Kikosi cha Algeria kilichotolewa kwenye Kombe la Dunia huko Afrika Kusini, na alijiunga na Portsmouth Mwaka 2009 toka Klabu ya Ufaransa Lens.

No comments:

Powered By Blogger