Wednesday 7 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Pweza Mtabiri aitia kiwewe Germany!!!
Ni Pweza anaeitwa Paul na anafugwa kwenye Zuu, hifadhi ya Wanyama na Viumbe wa Majini huko Berlin , Ujerumani na amepata umaarufu mkubwa kwa kutabiri matokeo ya mechi za Soka.
Lakini juzi, huku akirushwa laivu na TV za Ujerumani, aliwastua Watu pale alipotabiri Spain ndio itashinda kwenye Mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Germany.
Kawaida, Pweza huyo hutoa utabiri wake kwa kutumbukiziwa kwenye Bwawa lake glasi mbili za chakula chake na kila moja ina Bendera ya Timu zinazocheza na atakayoifuata ili kuchukua chakula ndie Mshindi.
Paul alitoa utabiri wake baada ya kutumbukiziwa kwenye sanduku lake la maji anakoishi glasi mbili zenye chakula moja ikiwa na Bendera ya Germany na nyingine Bendera ya Spain lakini Pweza huyo akafuata chakula kilichomo kwenye glasi ya Spain na hivyo huashiria ushindi kwa Spain.
Katika Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini, Pweza huyo ameshatoa utabiri uliokuja kuwa kweli mara 5 zikiwemo mechi za ushindi wa Ujerumani dhidi ya Australia, Ghana, England na Argentina na kipigo cha Ujerumani mikononi mwa Serbia.
Lakini Wajerumani wanafarijika kuwa mara pekee Paul alipotoa utabiri ambao haukutokea kuwa kweli ni wakati ule wa Fainali ya EURO 2008 ambapo alitabiri Germany itaifunga Spain na kuwa Bingwa wa Ulaya lakini ikaja Spain kuifunga Germany 1-0.
Safari hii, katika mechi ya Germany v Spain, ameitabiria Spain ushindi!! Je itakuwa kama 2008?

No comments:

Powered By Blogger