Wednesday 7 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Barca wakopa kulipa Wachezaji Mishahara!!
Rais mpya wa FC Barcelona, Sandro Rosell, amekiri walishindwa kuwalipa Wachezaji wao Mishahara ya Juni na imebidi wachukue mkopo Benki ili kuwalipa.
Sandro, alierithi wadhifa huo kutoka kwa Joan Laporta, amesema wamekopa Pauni milioni 125 ili kuhakikisha Wachezaji wanalipwa.
Amesema: “Tumeikuta Klabu ina madeni na haina mtiririko wa fedha. Imebidi tuchukue mkopo”
Hata hivyo, Sandro amedai Barca bado wana uwezo wa kumnunua Cesc Fabregas toka Arsenal kwa vile wanaingiza pesa na pia wamewauza Dmitro Chygrynskiy kwa Shakhtar Donetsk kwa Pauni milioni 12.5 na Yaya Toure kwa Manchester City kwa Pauni Milioni 20.
Pia Sandro amedai wanacho kitita cha zaidi ya Pauni Milioni 50 kununua Wachezaji wengine ikiwa Kocha Pep Guardiola atahitaji hilo.
Barcelona ndio Mabingwa wa Spain.

No comments:

Powered By Blogger