NI FAINALI!!!
Jumapili, Julai 11 Saa 3.30 usiku [bongo]
Kesho, pazia la kufunga Mashindano ya Kombe la Dunia 2010 iliyofanyika huko Afrika Kusini kuanzia Juni 11, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kuchezwa Afrika, litafungwa.
Kwa ujumla, Mashindano haya yameleta msisimko mkubwa hasa kwa vile Timu zile Vigogo zote, kama Italy, Brazil, Argentina na Ujerumani, zilibwagwa nje nyingine zilitolewa mapema mno.
Holland:
-Meneja: Bert van Marwijk
-Listi ya FIFA ya Ubora: nafasi ya 4
-Majeruhi: De Zeeuw
-Aliefungiwa: Hamna
Spain:
-Meneja: Vicente del Bosque
-Listi ya FIFA ya Ubora: nafasi ya 2
-Majeruhi: Albiol-Aliefungiwa: Hamna
DONDOO ZA MECHI:
-Hii ni Fainali ya kwanza ya Kombe la Dunia ambayo haina moja ya Nchi za Brazil, Argentina, Italy au Germany.
-Ikiwa Spain watashinda, itakuwa Nchi ya kwanza kutwaa Kombe la Dunia baada ya kufungwa mechi yao ya kwanza kwenye mechi za Fainali. Juni 16, Spain walifungwa na Uswisi bao 1-0.
-Ikiwa Holland watashinda, watakuwa ni Nchi ya Pili [Brazil ya kwanza Mwaka 1970] kwa kushinda mechi zao zote za Kombe la Dunia kuanzia mechi za Mchujo.
-Spain wamecheza pasi 3,387 katika Fainali hizi ambazo ni nyingi kupita Timu yeyote.
-Wesley Sneijder amefunga bao 7 katika mechi zake za Kimataifa 8 zilizopita.
Timu: Wachezaji wanaotegemewa kuanza
Holland: Stelenburg, Heitinga, Mathijsen, Van der Wiel, Van Bronkhorst, Van Bommel, Sneijder, De Jong, Robben, Kuyt, Van Persie
Spain: Casillas, Pique, Puyol, Ramos, Capdevila, Busquets, Xavi, Alonso, Iniesta, Pedro, Villa
Refa: Howard Webb [England]
No comments:
Post a Comment