Monday 5 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Dunga atimuliwa Brazil
CBF, Chama cha Soka Brazil, kimemfukuza kazi Kocha wao Dunga kufuatia kutolewa kwenye Kombe la Dunia hatua ya Robo Fainali walipofungwa na Holland bao 2-1.
CBF imetamka kuwa Kocha mwingine atateuliwa kabla ya mwisho wa Mwezi wa Julai.
Dunga na Kikosi chake waliwasili Brazil kutoka Afrika Kusini siku ya Jumapili na mwenyewe alishatamka huo ndio mwisho wake na Timu ya Brazil.
Dunga alianza Ukocha na Timu ya Brazil Mwaka 2006 alipochukua nafasi hiyo toka kwa Carlos alberto Parreira ingawa hakuwa na sifa za Ukocha.
Dunga ndie aliekuwa Nahodha wa Brazil Mwaka 1994 walipotwaa Kombe la Dunia huko USA.
Brazil ndio watakuwa Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2014.

No comments:

Powered By Blogger