Wednesday 7 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

NUSU FAINALI YA PILI:
Leo tena: German v Spain
Timu na Wachezaji:
Germany watamkosa tu Thomas Mueller ambae amefungiwa mechi moja baada ya kupata Kadi za Njano mbili na Wachezaji wao waliokuliwa na maumivu, Kiungo Sami Khedira, Arne Friedrich na Cacau, wote wako fiti.
Kocha wa Spain, Vicente del Bosque, itabidi afanye uamuzi mzito wa ama kumbakisha Fernando Torres au kumweka benchi kwa vile yuko chini ya kiwango.
Majeruhi wa Spain ni Cesc Fabregas na Carles Puyol ingawa wote wana nafasi kubwa ya kucheza.
Tathmini ya Mechi:
Hii ni Nusu Fainali ya 11 kwa Germany na safari hii ni Timu inayocheza staili tofauti na ya kuvutia kwa jinsi wanavyoonana Uwanjani na kushambulia kwa kasi.
Staili hiyo imeifanya Germany wazisage England bao 4-1 na kisha Argentina 4-0.
Spain iko tofauti mno na Spain inayojulikana na kila Mtu kwani safari hii inacheza Soka la kusuasua tofauti na lile Soka lao zuri lililozoeleka.
Hi ii mara ya kwanza kwa Spain, ambao ndio Mabingwa wa Ulaya, kufika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia.
Historia kati ya Timu hizi mbili:
Katika mechi 8 za Miaka ya hivi karibuni, Spain wameifunga Germany mara mbili tu moja ikiwa ni Fainali ya Kombe la Mataifa ya Ulaya, EURO 2008.
Katika mechi 3 za Kombe la Dunia ambazo Nchi hizi zimekutana, Germany waliifunga Spain 2-1 Mwaka 1966 na pia kwa idadi hiyo hiyo ya magoli Mwaka 1982.
Huko USA Mwaka 1994, Germany na Spain zilitoka sare 1-1.
Nchi hizi zimekutana mara 20, Germany wakishinda mara 8, Spain mara 6 na sare 6.
Waamuzi:
Refa: Viktor Kassai (Hungary)
Wasaidizi: Gabor Eros naTibor Vamos (Wote toka Hungary)
Ujerumani kuipiku Brazil!!
Wakicheza mechi yao ya Nusu Fainali ya Kombe la Dunia Uwanja wa Moses Mabhida, Durban dhidi ya Spain Jumatano Julai 7, Germany watakuwa wanacheza mechi yao ya 98 kwenye Fainali za Kombe la Dunia tangu Kombe la Dunia lianzishwe Mwaka 1930 na hivyo kuipiku Brazil iliyocheza mechi 97.
Germany hawakuruhusiwa kucheza Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 1950 kwa sababu ya matatizo yao ya kusababisha Vita Kuu ya Pili Duniani iliyomalizika Mwaka 1945.
Brazil ndio wanaonongoza kwa kuwa na rekodi nzuri kwa kucheza mechi 97, kushinda 67, sare 15 na kufungwa 15.
Ujerumani wameshinda 59, sare 19 na kufungwa 19.
Katika mechi hizo Brazil imefunga bao 211 na kufungwa 88 huku Germany ikiwa imefunga bao 203 na kufungwa 114.
Italy wamecheza jumla ya mechi 80, Argentina 70 na England 59.

No comments:

Powered By Blogger