Monday 5 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

FIFA yatangaza Marefa wa Nusu Fainali
Kamati ya Marefa ya FIFA imetangaza Marefa watakaochezesha mechi za Nusu Fainali za Kombe la Dunia kati ya Uruguay v Holland na Germany v Spain zitakazochezwa Jumanne na Jumatano.
Refa wa Uruguay v Holland atakuwa ni Ravshan Irmatov kutoka Uzbekistan ambae ana Miaka 32 na ndie Refa mdogo kuchezesha mechi za Fainali za Kombe la Dunia tangu Mwaka 1934.
Refa Irmatov atasaidiwa na Rafael Ilyasov kutoka Uzbekistan na Bakhadyr Kochkarov kutoka Kazakhstan.
Mechi ya Germany v Spain itasimamiwa na Refa Viktor Kassai kutoka Hungary na atasaidiwa na wenzake kutoka Hungary, Gabor Eros na Tibor Vamos.
Mchezaji Bora Duniani kuwa na Tuzo moja tu!
Rais wa FIFA, Sepp Blatter, ametoboa kuwa kuanzia Mwakani Tuzo za Mchezaji Bora Duniani wa Mwaka wa FIFA na ile ya Ballon d’Or, yaani ‘Mpira wa Dhahabu’, zitaunganishwa na kuwa Tuzo moja tu.
Ballon d’Or ilianzishwa Mwaka 1956 na Gazeti la Ufaransa la Soka liitwalo ‘France Football’ na uteuzi wake wa Mchezaji Bora hufanywa na Wanahabari wa Soka wa Kimataifa na awali Washindi wake walikuwa ni Wachezaji wa Ulaya tu lakini baadae milango ikawa wazi kwa kila Mchezaji kuishinda.
Mwaka 2009, Lionel Mess indie alietwaa Ballon d’Or.
Mchezaji Bora Duniani wa Mwaka wa FIFA ilianzishwa Mwaka 1991 na Washindi huteuliwa na Makocha wa Timu za Taifa na Manahodha wao.
Mwaka 2009, Lionel Mess indie pia alitwaa Tuzo hii.
Tuzo hiyo moja mpya ya Mchezaji Bora Duniani wa Mwaka sasa itajulikana kama FIFA Ballon d’Or na itatolewa tarehe 10 Januari 2011 Mjini Zurich, Uswisi.
Jopo litalochagua Mshindi wa Tuzo hiyo mpya litakuwa ni mchanganyiko wa Waandishi wa Habari wa Kimataifa na Makocha wa Timu za Taifa na Makepteni.
Rio kupona kabla Ligi Kuu kuanza
Manchester United imetangaza kuwa Difenda wao Rio Ferdinand atapona goti aliloumia akiwa mazoezini na England huko Rustenburg, Afrka Kusini kabla kuanza kwa Kombe la Dunia na hivyo kuweza kucheza Ligi Kuu England itakayoanza Agosti 14.
Katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Man United itacheza na Newcastle, Timu iliyopanda Daraja, Uwanjani Old Trafford.

No comments:

Powered By Blogger