Tuesday 6 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Kitimtim leo: Holland v Uruguay
Macho ya Ulimwengu mzima yatakuwa Uwanja wa Green Park, Cape Town kushuhudia Nusu Fainali ya kwanza kati ya Holland na Uruguay.
Holland ilijikita Nusu Fainali hii baada ya kuwatoa Brazil bao 2-1 kwenye Robo Fainali baada ya kuwa nyuma 1-0 hadi mapumziko kwenye mechi hiyo.
Nao Uruguay wametinga hapa kwa msaada wa ujangili mkubwa wa Luis Suarez aliedaka mpira kwenye mstari wa goli dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza wa dakika 30 na Ghana kupewa penalty ambyo Gyan Asamoah alipiga mwamba na kukosa kuipa ushindi Ghana na ndipo Uruguaya wakashinda kwa matuta 4-2.
Suarez, kwa uhalifu wake, alipewa Kadi Nyekundu na ataikosa mechi hii na nafasi yake itachukuliwa na Sebastian Abreu.
Mbali ya kumkosa Suarez, Kocha wa Uruguay, Oscar Tabarez, anakabiliwa na na kuumia kwa Wachezaji na pia kufungiwa kwa Jorge Fucile mechi moja.
Wachezaji wake majeruhi ni Nicolas Lodeiro, alievunjika mguu, na Diego Lugano.
Holland nao wanao Wachezaji wenye Kadi na hivyo kuikosa mechi hii na nao ni Gregory van der Wiel na Nigel de Jong.
Nafasi zao zinategemewa kujazwa na Khalid Boulhrouz na Demy de Zeeuw.
Mshindi wa mechi hii atacheza Fainali na Mshindi wa Argentina v Germany watakaocheza kesho.
Uruguay hawajaingia Fainali ya Kombe la Dunia tangu Mwaka 1950 walipowafunga Wenyeji Brazil 2-1 Uwanja wa Maracana na kutwaa Ubingwa wa Dunia kwa mara ya pili mara ya kwanza ilikuwa Mwaka 1930.
Holland wanawania kuingia Fainali yao ya 3, mara ya kwanza ilikuwa 1974 walipofungwa na Ujerumani nay a pili ilikuwa 1978 walipotolewa na Argentina.

No comments:

Powered By Blogger