Friday, 9 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

MECHI YA MSHINDI WA 3:
Germany v Uruguay
Jumamosi Julai 10 Saa 3.30 usiku [bongo]
Hali za Kila Timu:
Germany huenda wakamkosa Straika Miroslav Klose mwenye maumivu ya mgongo na hivyo, akiwa amefunga jumla ya mabao 14 kwenye Fainali za Kombe la Dunia zote alizocheza, huenda akaikosa nafasi ya kuifikia rekodi ya Ronaldo de Lima ya kufunga jumla ya mabao 15 kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Thomas Muller amemaliza kifungo chake cha mechi moja na bila shaka ataonekana dimbani.
Uruguay watamkaribisha tena Luis Suarez aliefungiwa mechi moja kwa kushika mpira kwa makusudi na kuwakosesha Ghana ushindi.
Pia Beki wao Jorge Fucile atarudi tena baada ya kumaliza kifungo chake.
Tathmini:
Hii ni mechi ambayo kila Timu haitaki kuicheza kwa vile kila Timu inataka iingie Fainali na kutwaa Kombe la Dunia.
Lakini safari hii Mabingwa mara 3 wa Kombe la Dunia, Germany, wataivaa Uruguay ambao ni Mabingwa mara mbili.
Hii ni mechi ambayo kila Kocha huwa na wakati mgumu kuwapa motisha Wachezaji wao baada ya kuvunjika moyo kwa kutoingia Fainali ya Kombe la Dunia.
Historia kati yao:
Hii ni mechi ya 10 kati yao na Uruguay ilishinda mechi ya kwanza kwa bao 4-1 Mwaka 1928 lakini hawajashinda tena kati mechi 8 zilizofuata.
Germany wameshinda mechi 6, suluhu 2 na wamefungwa moja.
Waamuzi:
Refa:Benito Archundia (Mexico)
Wasaidizi: Hector Vergara (Canada) & Marvin Torrentera (Mexico)

No comments:

Powered By Blogger