Monday 5 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Nigeria ‘Mikono Juu!’
Kuna taarifa kuwa Serikali ya Nigeria imefuta ile amri ya kuzuia Timu yake ya Taifa isicheze Soka la Kimataifa kwa Miaka miwili ikiwa ni saa moja tu kabla ule muda uliotolewa na FIFA wa kutaka amri hiyo ifutwe ufike na hivyo kukwepa kufungiwa na FIFA.
Amri hiyo ilitolewa baada ya Nigeria kutupwa nje ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini iliposhika mkia Kundi lake.
Jumapili, NFF, Chama cha Soka cha Nigeria, kiliwafukuza Rais wake na Makamu wake ili kuibembeleza Serikali iondoe amri yake ili kukwepa rungu la FIFA na inasemekana Kamati ya NFF leo ilikwenda kuonana na Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ili kumpigia magoti aifute amri yake.

No comments:

Powered By Blogger