Sunday 4 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Nigeria watimuana!
NFF, Chama cha Soka cha Nigeria, kimewatimua Viongozi wawili ambao ni Rais wa NFF na Makamu wake ili kumbembeleza Rais wa Nchi yao, Goodluck Jonathan, abadilishe msimamo wa kuizuia Nchi hiyo kucheza Mashindano ya Kimataifa kwa Miaka miwili na hivyo kukwepa adhabu ya kusimamishwa na FIFA kwa kuingiliwa na Serikali.
FIFA imeipa Nigeria mpaka Jumatatu jioni Julai 5 ili iondoe uamuzi wa kuizuia kucheza Kimataifa la sivyo itachukuliwa hatua.
Hodgson ahofia kufa urafiki na Fergie
Meneja mpya wa Liverpool, Roy Hodgson, ana wasiwasi kujiunga kwake na Liverpool kutatia doa uhusiano wake na rafiki yake Sir Alex Ferguson, Meneja wa Manchester United.
Liverpool na Manchester United ni Klabu Mahasimu na wapinzani wakubwa sana huko England.
Hodgson amesema: “Najua Sir Alex si mtu wa Liverpool hivyo nina wasiwasi uhusiano wetu utaharibika! Lakini itabidi niongee nae na tunywe mvinyo pamoja hata kwa siri!”

No comments:

Powered By Blogger