Friday 9 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Pweza Paulo atabiri Spain Bingwa Duniani, Germany Mshindi wa 3!!!
Yule Pweza Paulo, aliejijengea umaarufu Duniani kwa kutabiri mechi za Kombe la Dunia zinazochezwa huko Afrika Kusini, leo akiwa laivu kwenye TV alitabiri Spain ndie atashinda Jumapili dhidi ya Holland na kutwaa Kombe la Dunia.
Pweza Paulo hutoa utabiri wake kwa kutumbukiziwa kwenye tangi lake la maji anakoishi glasi mbili zenye chakula ambapo kila glasi inakuwa na bendera ya Timu moja.
Leo Paulo alifuata glasi yenye bendera ya Spain akiashiria Spain ndio Mshindi.
Kwenye mechi kati ya Germany na Uruguay itakayochezwa Jumamosi kutafuta Mshindi wa Tatu, Pweza Paulo aliifuata glasi ya Germany.
Listi ya wanaowania Mpira wa Dhahabu Kombe la Dunia yatolewa
FIFA imetoa Listi ya Wachezaji 10 watakaogombea Tuzo ya Mpira wa Dhahabu wa Kombe la Dunia 2010 ambayoi hutunukiwa Mchezaji Bora wa Mashindano hayo.
Listi hiyo ya Wachezaji hao 10 ni:
-David Villa [Spain]
-Xavi [Spain]
-Andres Iniesta [Spain]
-Wesley Sneijder [Holland]
-Arjen Robben [Holland]
-Bastian Schweinsteiger [Germany]
-Mesut Ozil [Germany]
-Lionel Messi [Argentina]
-Diego Forlan [Uruguay]
-Asamoah Gyan [Ghana]
Listi nyingine iliyotolewa na FIFA inahusu Mchezaji Bora Kijana na wamo:
-Thomas Mueller [Germany]
-Andrew Ayew [Ghana]
-Giovani dos Santos [Mexico]
Washindi wa Tuzo hizo watatangzwa Jumapili mara baada ya Fainali ya Kombe la Dunia itakayochezwa kati ya Holland na Spain Uwanja wa Soccer Cuty, Soweto, Johannesburg.

No comments:

Powered By Blogger