Thursday 8 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Hargreaves mashakani tena!
Owen Hargreaves ataukosa mwanzo wa Msimu mpya wa Ligi Kuu England utakaoanza Agosti 14 kwa sababu ya kuendelea kusumbuliwa na matatizo yake ya magoti na anategemewa kurudi kwa Daktari speshelisti aliemfanyia opersheni huko Marekani kwa uchunguzi zaidi.
Habari hizo za matatizo ya Hargreaves zilithibitishwa na Meneja wake wa Manchester United, Sir Alex Ferguson.
Kiungo huyo alikuwa nje ya uwanja kwa Miezi 18 baada ya kupasuliwa magoti yote mawili na Msimu uliokwisha alirudi uwanjani na kuichezea Man United mechi moja tu.
Jumatatu ijayo, Man United inasafiri hadi Marekani ili kuanza ziara yao ya mazoezi na mechi za kirafiki na pia watazuru Canada na Mexico.
Ferguson vilevile alitoboa kuwa Michael Owen amepona na yupo mazoezini.
Kuhusu Anderson alieumia vibaya goti, Ferguson amesema anaendelea vizuri na huenda akarudi Uwanjani Mwezi Septemba.
Jovanovic atua Anfield
Fowadi kutoka Serbia, Milan Jovanovic, ambae alifunga bao moja na la ushindi Serbia ilipoifunga Germany kwenye mechi ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini, amesaini Mktaba wa Miaka mitatu na Liverpool.
Jovanovic, Miaka 29, ni Mchezaji Huru baada ya Mkataba wake na Klabu ya Ubelgiji Standard Liege kumalizika mwishoni mwa Msimu uliopita.
Inasemekana, Rafael Benitez ndie alietaka Jovanovic aende Liverpool kabla yeye kujua atahamia Inter Milan na hilo liliibua hisia huenda Jovanovic akaenda Inter badala ya Liverpool ili kuungana na Benitez.

No comments:

Powered By Blogger