Tuesday 6 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Holland yajikita Fainali!!!!
Holland 3 Uruguay 2
Holland imeipiga Uruguay bao 3-1 na kuingia Fainali za Kombe la Dunia katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Green Park, Cape town.
Holland watakutana Fainali Siku ya Jumapili Uwanjani Soccer City, Soweto na Mshindi kati ya Germany na Spain.
Hii itakuwa ni Fainali ya 3 kwa Holland lakini katika mbili za Mwaka 1974
walifungwa na Germany na ile ya Mwaka 1978 walitolewa na Argentina.
Holland ndio waliopata bao mwanzo kwa shuti kali la mbali la Van Bronckhorst dakika ya 18.
Nae Diego Forlan akajibu mapigo kwa shuti la aina hiyo hiyo dakika ya 40.
Hadi mapumziko bao 1-1.
Kipindi cha pili, Holland wakapata bao mbili Wafungaji wakiwa Sneijder dakika ya 69 huku Van Persie akiwa wazi ofsaidi akimbabaisha Kipa na la tatu alifunga Arjen Robben dakika ya 72.
Kwenye dakika ya 90, Uruguay wakapata bao lao la pili kupitia Max Pereira.
Timu:
Uruguay: 1-Fernando Muslera; 3-Diego Godin, 6-Mauricio Victorino, 5-Walter Gargano, 16-Maximiliano Pereira, 22-Martin Caceres, 15-Diego Perez, 11-Alvaro Pereira, 17-Egidio Arevalo, 7-Edinson Cavani, 10-Diego Forlan.
Holland: 1-Maarten Stekelenburg; 12-Khalid Boulahrouz, 3-John Heitinga, 4-Joris Mathijsen, 5-Giovanni van Bronckhorst; 7-Dirk Kuyt, 6-Mark van Bommel, 10-Wesley Sneijder, 14-Demy de Zeeuw, 11-Arjen Robben; 9-Robin van Persie.
Refa: Ravshan Irmatov (Uzbekistan)

No comments:

Powered By Blogger