Brazil yaanua Nembo ya Kombe la Dunia 2014
Brazil, ambao ndio watakuwa Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2014, leo wameanua rasmi Nembo itayotumika kwenye Mashindano hayo.

Rais Lula, katika uzinduzi huo, alisema wana mzigo mkubwa kuyafanya Mashindano ya Mwaka 2014 yawe ya mafanikio kama hayo ya Afrika Kusini.
Lula alitamka: “Mafanikio ya Ndugu zetu wa Afrika ni changamoto kubwa kwa Brazil. Tutajifunza kutoka kwao.”
Nae Rais wa FIFA, Sepp Blatter, amesema Soka huko Brazil ni kama dini na ameisifia kwa kuipa umuhimu kuliko Nchi yeyote.
Brazil ni Mabingwa wa Dunia mara 5 na walikuwa Wenyeji wa Kombe la Dunia Mwaka 1950.
No comments:
Post a Comment