Thursday 8 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Arsenal wapata Difenda
Arsenal wamemnyakua Beki Laurent Koscielny kutoka Klabu ya Lorient ya Ufaransa kwa dau ambalo halikutajwa.
Beki huyo Mfaransa amesifiwa na Meneja wa Arsenal Arsene Wenger kuwa ni Mpiganaji mzuri na ataziba vizuri pengo liloachwa na William Gallas na Mikel Silvestre ambao mikataba imekwisha na pia Senderos aliehamia Fulham.
Huyu ni Mchezaji wa pili kuchukuliwa na Arsenal baada ya Straika Marouane Chamakh kujiunga kutoka Bordeaux.
Moratti akiri Man United inamtaka Sneijder
Rais wa Inter Mila Massimo Moratti amekiri kuwa ni kweli Manchester United ina nia ya kumchukua Kiungo toka Uholanzi Wesley Sneijder.
Mbali ya kukiri hivyo, Moratti amedai Sneijder, Miaka 26, atabaki Inter Milan ambayo Msimu uliokwisha chini ya Kocha Jose Mourinho alitoa mchango mkubwa kwa Timu hiyo kubeba Trebo, yaani Ubingwa wa Serie A, Coppa Italia na UEFA CHAMPIONS LIGI.
FAINALI NI HOLLAND v SPAIN
Spain 1 Germany 0
Bao la kichwa la Carles Puyol la dakika ya 73 kufuatia kona limewafikisha Spain Fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia yao na watakutana na Holland Jumapili huko Soccer City, Soweto, Johannesburg na Siku hiyo atapatikana Bingwa mpya wa Dunia kwa vile Spain na Holland hawajawahi kuchukua Kombe la Dunia hata mara moja.
Spain walitawala kwa kipindi kirefu mechi hii lakini walishindwa kabisa kuipenya ngome ya Germany huku Germany wakionekana ni hatari kwa mashambulizi ya kushtukiza.
Germany watakutana na Uruguay Jumamosi kupata Mshindi wa Tatu.
Timu:
Spain: Casillas, Sergio Ramos, Pique, Puyol, Capdevila, Busquets, Alonso, Iniesta, Xavi, Pedro, Villa.
Akiba: Valdes, Albiol, Marchena, Torres, Fabregas, Mata, Arbeloa, Llorente, Javi Martinez, Silva, Jesus Navas, Reina.
Germany: Neuer, Lahm, Friedrich, Mertesacker, Boateng, Khedira, Schweinsteiger, Trochowski, Ozil, Podolski, Klose.
Akiba: Wiese, Jansen, Aogo, Tasci, Kiessling, Badstuber, Kroos, Cacau, Marin, Gomez, Butt.

No comments:

Powered By Blogger