Monday 5 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Bundesliga kuanza Agosti 20
Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich, wataanza kampeni yao ya kutetea Ubingwa wao wa Ligi ya Ujerumani, Bundesliga, wakiwa Uwanja wa nyumbani kwa kuivaa VfL Wolfsburg, waliokuwa Mabingwa 2009, hapo Agosti 20 wakati mechi za ufunguzi za Ligi zitakapoanza kuchezwa.
Msimu wa 2010/11 wa Bundesliga utamalizika Mei 14, 2011 na kutakuwa na mapumziko majira ya baridi kuanzia Desemba 19, 2010 hadi Januari 14, 2011.
Mechi nyingine Siku ya ufunguzi Agosti 20 ni ile ya Mshindi wa Pili, Schalke, atakaekuwa ugenini kucheza na SV Hamburg.
Timu iliyopanda Daraja St Pauli Hamburg itakuwa ugenini kuikwaa SC Freiburg na Cologne itaikaribisha Kaiserslautern.

No comments:

Powered By Blogger