Friday 9 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Tusimtegemee Rooney!!
Darren Fletcher anaamini ikiwa watataka kutwaa tena Ubingwa wa Ligi Kuu England Manchester United itabidi waondoe lile tegemezi lao kwa Wayne Rooney pekee kuwafungia magoli.
Msimu uliokwisha Rooney alifunga jumla ya Mabao 43 katika Mashindano yote lakini Chelsea ndio wakaibuka Mabingwa na Man United wakamaliza nafasi ya pili.
Fletcher ametamka: “Kama Timu itabidi tuongeze bidii na Wachezaji waongeze ubora. Msimu uliokwisha tuliwaona Nani na Valencia wakiongeza ubora wao”
Pia aliisema Timu ya Msimu uliopita ilikuwa kwenye kipindi cha mpito na hivyo Msimu huu watatulia zaidi.
Pweza Paulo: Kutoa utabiri leo mechi ya kesho Germany v Uruguay!
Huko Oberhausen, Ujerumani, ndani ya Tangi lake la maji anakoishi, Pweza aitwae Paulo, ambae amejizolea sifa kubwa ya kuwa Mtabiri wa Soka, anangojewa kwa hamu kutoa utabiri wa Mechi ya kutafuta Mshindi wa Tatu wa Kombe la Dunia, kati ya Germany na Uruguay, itakayochezwa huko Afrika Kusini Siku ya Jumamosi.
Pweza Paulo alitabiri Spain itashinda Mechi kati ya Spain na Germany ya Nusu Fainali na kweli Spain ikashinda na kuwavunja moyo maelfu ya Wajerumani ambao baadhi walikasirishwa na kutishia kumkaanga na kumla.
Baadhi ya Magazeti huko Ujerumani yalibeba bango: ‘MHAINI!’
Awali Pweza huyo alitabiri sawa sawa kabisa Mechi zote za Germany za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini ambazo Germany ilizifunga Australia, Ghana, England na Argentina, na pia alitabiri kipigo cha Germany toka kwa Serbia.
Sasa Paulo amepata umaarufu mkubwa Duniani na kuonyeshwa kwenye TV kubwa kama CNN na BBC na pia kutoka katika Magazeti kila kona ya Dunia.
Ulinzi umeimarishwa kwa Pweza Paulo na inadaiwa Serikali ya Germany inafikiria kumpa hadhi ya Kiumbe alie hatarini ili apate hifadhi bora.
Kwa sasa Dunia nzima inagonja utabiri wa Mechi mbili za Kombe la Dunia na hasa ile Fainali ya Jumapili kati ya Holland v Spain.

No comments:

Powered By Blogger