Tuesday, 6 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Kocha mpya Ufaransa kujenga upya Les Bleus!!
Laurent Blanc, Miaka 44, amechukua wadhifa wa Kocha wa Ufaransa baada ya Raymond Domenech kumaliza Miaka 6 iliyoisha kwa fedheha na kuaibishwa huko Afrika Kusini walipotolewa Raundi ya Kwanza baada ya kushika mkia na pia Kikosi kukumbwa na ugomvi uliofanya Nicolas Anelka kutimuliwa.
Blanc, aliewahi kuwa Nahodha wa Ufaransa, amebainisha kuwa vitendo vilivyotokea huko Afrika Kusini vilimfedhehesha na ana nia kubwa ya kukutana na baadhi ya Wachezaji ili kuongea nao.
Mechi ya kwanza kwa Ufaransa chini ya Blanc itakuwa ni ile ya kirafiki dhidi ya Norway hapo Agosti 11 na kisha ni mechi ya mchujo ya EURO 2012 dhidi ya Balarus.
Blanc, aliewahi pia kuwa Difenda wa Manchester United, amekiri anahitaji bahati ili awe na mwanzo mwema kwa kuwa Timu haijakaa sawa na ina matatizo makubwa.
Pia amesema atakutana na Patrice Evra, aliekuwa Nahodha wa France huko Afrika Kusini, ambae Mchezaji wa Zamani wa France, Liliam Thuram, ametaka asiichezee tena Ufaransa kwa kuhusiana na mgomo huko Afrika Kusuni.
Mbali ya Evra, Blanc amesema atazungumza na Franck Ribery, Thierry Henry, William Gallas na Eric Abidal, ambao wote ndio wanaotuhumiwa kuchochea mgomo huko Afrika Kusini.
Man United kumchukua Sneijder?
Kuna uvumi mzito kuwa Manchester United huenda wakatoa ofa ya Pauni Milioni 30 kwa Inter Milan ili kumnunua Kiungo Wesley Sneijder, Miaka 26, ambae sasa anang’ara mno huko Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia na Nchi yake Uholanzi.
Sneijder, Mchezaji wa zamani wa Ajax na Real Madrid, alijiunga na Inter Milan Msimu uliokwisha baada ya kutemwa na Real na aliisaidia Inter, chini ya Jose Mourinho, kutwaa Ubingwa wa Ulaya.
Man United wanamchukulia Sneijder kama ni mrithi anaestahili kwa Kiungo wao Veterani, Paul Scholes, anaetegemewa kustaafu 2011.
Hata hivyo, Man United huenda wakapata upinzani mkubwa toka kwa Meneja mpya wa Inter Milan, Rafael Benitez, ambae huenda akagoma kumtoa Sneijder kwa Man United ambao ni Mahasimu wakubwa wa Klabu yake ya zamani Liverpool.

No comments:

Powered By Blogger