Saturday, 17 October 2009

GOLI LA PUTO JEKUNDU LAIUA LIVERPOOL!!!
Goli la dakika ya 5 Mfungaji akiwa Darren Bent aliepiga shuti na kugonga puto lililorushwa uwanjani na Shabiki wa Liverpool na kumbabaisha Kipa wa Liverpool Pepe Reina huku mpira ukipita kushoto kwake na puto kupita kulia limewapa ushindi Sunderland wakiwa nyumbani Stadium of Light.
Puto hilo lilimbabaisha Kipa Reina ambae alionekana kutaka kudaka puto badala ya mpira na Wachezaji wa Liverpool walilalamika lakin Refa aliamua ni goli halali.
Liverpool, wakicheza bila ya mihimili yao Nahodha Steven Gerrard na Straika Fernando Torres, kipigo cha leo ni cha nne kwa msimu huu.
Mabingwa MAN U washinda 2-1 na kutinga kileleni!!!
Ndani ya Old Trafford, Manchester United, leo wameifunga Bolton Wanderers 2-1 na kuchukua uongozi wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 22 na kufuatiwa na Chelsea, waliofungwa na Aston Villa 2-1 leo, wakiwa na pointi 21.
Goli la kwanza lilifungwa dakika ya 5 baada ya kichwa cha Michael Owen kumbabatiza Beki Zat Knight na bao la pili alifunga Antonio Valencia dakika ya 33 likiwa ni goli lake la kwanza kwa Winga huyo kuifungia Man U.
Bao la Bolton lilifungwa na Matty Taylor kwa kichwa dakika ya 75.
Vikosi vilikuwa:
Man Utd: Van der Sar, Neville, Ferdinand, Jonathan Evans, Evra, Valencia, Carrick, Anderson, Giggs, Owen, Berbatov. AKIBA: Kuszczak, Brown, Nani, Scholes, Welbeck, O'Shea, Macheda.
Bolton: Jaaskelainen, Ricketts, Knight, Cahill, Samuel, Lee, Cohen, Muamba, Gardner, Taylor, Kevin Davies.
AKIBA: Al Habsi, Robinson, Steinsson, Mark Davies, Klasnic, McCann, Basham.
Refa: Mark Clattenburg
Arsenal 3 Birmingham 1
Wakiwa kwao Emirates Stadium Arsenal wameifunga Birmingham 3-1 na sasa wako nafasi ya 4 wakiwa na pointi 18 kwa mechi 8.
Magoli ya Arsenal yaligungwa na Van Persie dakika ya 16, diaby ya 18 na Arshavin dakika ya 84.
Bao la Birmingham lilifungwa na Lee Bowyer dakika ya 38.
RATIBA LIGI KUU:
Jumapili, Oktoba 18: [saa za bongo]
Blackburn v Burnley [saa 9 mchana]
Wigan v Man City [saa 12 jioni]
Jumatatu, Oktoba 19
Fulham v Hull City
Kama Fergie nae Wenger amkandya Refa Alan Wiley!!!
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ameungana mkono na Sir Alex Ferguson wa Manchester United kwa kumlaumu Refa Alan Wiley lakini Wenger hakudai, kama alivyodai Ferguson, kuwa Refa huyo hayuko fiti ila amesema Refa huyo huongea vizuri sana na yuko karibu mno na Wachezaji.
Wenger anadai alimwona Refa Alan Wiley akiongea na Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney, wakati wa haftaimu wa mechi moja na hilo limemkera Wenger ambae amesema: “Naamini Marefa ili wafanye kazi yao vyema ni lazima wasiwe na uhusiano na Wachezaji na Mameneja!”
Nae Mlinzi na Nahodha wa Manchester United, Gary Neville, amemtetea Meneja wake Sir Alex Ferguson katika mzozo kuhusu Refa Wiley alipomwita hayuko fiti kwa kusema: “Wamemwandama Meneja wetu lakini Refa Wiley alikuwa akitumia muda mrefu sana kuwaonya Wachezaji na kuwaandika kwenye kitabu chake! Wachezaji na Mameneja hawawezi kushinda! Mashabi na kadamnasi inataka ukweli lakini FA inatushitaki sisi Wachezaji na Mameneja tukisema ukweli!”
Sir Alex Ferguson ametakiwa na FA kutoa maelezo kuhusu kauli yake ya kuwa Refa Alan Wiley hayuko fiti na inategemewa wiki ijayo FA itaamua kumfungulia mashitaka au la.
Aston Villa 2 Chelsea 1
Wakiwa uwanjani kwao Villa Park, Aston Villa wamewafunga vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, mabao 2-1 katika mechi ya leo iliyoanza mapema.
Hadi mapumziko mabao yalikuwa 1-1.
Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kufunga kwa mkwaju wa mbali wa Didier Drogba uliodunda mbele ya Kipa Brad Friedel na kutinga wavuni.
Richard Dunne aliisawazishia Aston Villa kwa kichwa baada ya kona na kipindi cha pili ni kona nyingine tena iliyowapa Aston Villa ushindi kupitia Mlinzi James Collins aliefunga kwa kichwa.
VIKOSI vilikuwa:
Aston Villa: Friedel, Cuellar, Collins, Dunne, Warnock, Petrov, Milner, Sidwell, Ashley Young, Carew, Agbonlahor. AKIBA: Guzan, Delph, Heskey, Reo-Coker, Shorey, Beye, Gardner.
Chelsea: Cech, Bosingwa, Carvalho, Terry, Ashley Cole, Essien, Malouda, Lampard, Deco, Anelka, Drogba. AKIBA: Hilario, Ivanovic, Joe Cole, Zhirkov, Kalou, Sturridge, Belletti.

Tevez atishia kujitoa Timu ya Taifa Argentina!!!
Wakati Kocha wake wa Argentina, Diego Maradona, yuko kwenye uchunguzi wa Kamati ya Nidhamu ya FIFA kwa kutukana akiwa kwenye TV laivu, Mchezaji wa Argentina Carlos Tevez ametishia kujitoa kuichezea Argentina kwa madai kuwa wanaandamwa na kusemwa bila msingi.
Tevez amesema: “Nikiichezea Argentina muda mwingi Napata karaha kuliko kupata raha! Mashabiki wanatutukana, Waandishi wanaponda kila kitu chetu! Nimechoka na haya yote! Sasa nafikiria kujitoa! Kwa nini nije Argentina ili kupata shida?”
Ufaransa, Ureno, Urusi na Ugiriki kutocheza kati yao mechi za Mtoano za Kombe la Dunia!!!!
Jumatatu inapangwa Droo maalum ili kupata mechi 4 zitakazochezwa na Nchi za Ulaya zilizoshika nafasi ya pili kwenye Makundi yao ya Kombe la Dunia ili kupata Nchi 4 zitakazoenda Fainali Kombe la Dunia na Timu zinazohusika kwenye Droo hiyo ni Ufaransa, Ureno, Urusi, Ugiriki, Republic of Ireland, Slovenia, Ukraine na Bosnia-Herzegovina.
Kufuatia FIFA kutangaza Listi ya Ubora Duniani, huku Brazil akiwa nambari wani, Nchi za Ufaransa, Ureno, Urusi na Ugiriki zimeibuka kuwa mbele ya Republic of Ireland, Bosnia, Slovenia na Ukraine na hivyo hii inamaanisha Ufaransa, Ureno, Urusi na Ugiriki haziwezi kupangwa kukutana kati yao kwenye Mechi hizo za Mtoano.
Hivyo Nchi hizo zitawekwa Kapu la Kwanza na Republic of Ireland, Bosnia. Slovenia na Ukraine zitakuwa Kapu la Pili na Nchi za Kapu la Kwanza zitapambanishwa na Nchi za Kapu la Pili.
Mechi hizo za Mtoano zitachezwa nyumbani na ugenini hapo Novemba 14 na Novemba 18.
Huko Ulaya tayari Nchi za Denmark, England, Germany, Netherlands, Serbia, Spain, Italy, Slovakia, Switzerland zimeshatinga Fainali Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010 baada kuongoza Makundi yao.
Liverpool leo bila Gerrard na Torres!!
Klabu ya Liverpool leo itashuka Uwanjani ugenini huko Stadium of Light kucheza na Sunderland kwenye Ligi Kuu England bila ya Nyota wao Nahodha Steven Gerrard na Straika Fernando Torres walioumia kwenye mechi za Nchi zao za Kombe la Dunia wikiendi iliyopita.
Wote, Gerrard na Torres, hawakuzichezea mechi za Kombe la Dunia za England na Spain Jumatano.
Rooney nje mechi ya Man U leo!!
Sir Alex Ferguson amethibitisha kuwa Mshambuliaji wa Manchster United, Wayne Rooney, hawezi kucheza mechi ya leo ya Ligi Kuu dhidi ya Bolton baada ya kuumia kwenye mechi ya England na Ukraine ya Kombe la Dunia Jumamosi iliyopita huko Ukraine.
Rooney hakucheza mechi ya England ya Jumatano waliyocheza na Estonia Wembley Stadium.
Vilevile, Sir Alex Ferguson amethibitisha kuwa Mshambuliaji mwingine, Dimitar Berbatov, alikuwa bado hajarudi toka kwao Bulgaria alikoichezea Nchi yake Jumatano na kuifungia bao 3 kwenye mechi ya Kombe la Dunia Bulgaria iliyoifunga Georgia bao 6-2.
Berbatov imebidi abaki kwao kwa vile Mpenzi wake anategemewa kujifungua mtoto wao.
Kukosekana kwa Rooney na Berbatov sasa kunampa mwanya Michael Owen kucheza leo.
Ferguson pia amethibitisha Kipa Edwin van der Sar atacheza mechi hiyo na Bolton ikiwa ni mara yake ya kwanza kucheza msimu huu baada ya kuvunjika na kufanyiwa operesheni ya mfupa wa mkononi kwenye mechi kugombea Kombe la Audi huko Ujerumani Man U walipocheza na Bayern Munich.
FIFA U-20 WORLD CUP Egypt 2009:
Ghana BINGWA!!!
Wanyakua Kombe kwa Matuta 4-3!!!
Ghanawamefanikiwa kutwaa Kombe la Dunia kwa Vijana wa Chini ya Miaka 20 walipoishinda Brazil kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya mechi kwisha 0-0 dakika 90 na kuongezwa dakika 30 bila Timu kupata bao.
Mchezaji wa Ghana, Dominic Adiyiah, alitunukiwa Mpira wa Dhahabu kwa kuibuka Mfungaji Bora wa Mashindano hayo akiwa amefunga bao 8.
FIFA yamchunguza Maradona!
Kocha wa Argentina, Diego Maradona, yupo kwenye uchunguzi na FIFA baada ya kubwata matusi mara baada ya Argentina kushinda huko ugenini Uruguay bao 1-0 na kufanikiwa kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrka Kusini mwakani.
Matusi ya Maradona akiwa kwenye TV iliyokuwa ikirusha matangazo laivu yaliwalenga Waandishi wa Habari na Watu wanaompinga.
Rais wa FIFA, Sepp Blatter, amesema hawana njia nyingine ila kuitaka Kamati ya Nidhamu kumchunguza.
Maradona, miaka 48, akipatikana na hatia atafungiwa mechi 5 na kupigwa faini.
Lakini, Mkuu wa Chama cha Soka cha Argentina, Julio Grondona, amemtetea Maradona kwa kudai ingekuwa Kocha mwingine hatua hiyo ya FIFA isingechukuliwa.
Maradona mwenyewe, ingawa amekataa kuomba radhi, ameahidi kutorudia vitendo hivyo na pia aliombamsamaha kwa Wanawake wote, Mama yake, Wanawake wa Argentina na Uruguay pamoja na Dunia nzima.
Chelsea kukata rufaa kupinga kifungo chao!!
Chelsea imetangaza kuwa itakata rufaa CAS [Court of Arbitration for Sports], Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo, kupinga kifungo walichopewa na FIFA cha kutosajili Wachezaji hadi 2011 baada ya kupatikana na hatia ya kumsajili na kumrubuni Chipukizi Gael Kakuta, miaka 18, avunje mkataba wake na Klabu ya Ufaransa Lens mwaka 2007.
Chelsea wamebakisha siku 10 za kukata rufaa.
Mbali ya kufungiwa kutosajili, Chelsea waliamriwa wailipe Lens fidia ya Euro 130,000 kama gharama zao za kumfundisha Gael Kakuta huku Mchezaji huyo akitakiwa ailipe Lens Euro 780,000 kama fidia.

Friday, 16 October 2009

Liverpool ipo Sokoni!!!
Mwana wa Kifalme wa huko Saudi Arabia Faisal bin Fahd bin Abdullah inasemekana ametamka Kampuni yake iitwayo F6 ipo kwenye hatua za mwisho za mazungumzo ya kununua hisa za Klabu ya Liverpool na Mikutano hiyo inafanyika huku mmoja wa Wamiliki wawili wa Kimarekani, George Gillett , yupo huko Saudi Arabia.
Ilitangazwa kuwa George Gillett ameenda huko Saudi Arabia ili kujadili mradi wa Liverpool kuuanzisha Vyuo vya Soka huko Arabuni.
Kwa muda mrefu George Gillett na Mmilki mwenzake Tom Hicks wamekuwa wakitafuta Mwekezaji mwingine ili wasaidiwe mzigo mkubwa wa madeni yanayoikabili Liverpool.
Mkuu wa F6, Barry Didato, amekaririwa akisema Mmiliki wa Kampuni hiyo, Mwana wa Kifalme Faisal, alikuwa akitafakari kuinunua Liverpool na anaweza kununua hisa kuanzia “sifuri hadi asilimia mia”.
Hata hivyo Didato amesema Faisal amekuwa akitafakari kwa undani zaidi hasa kutokana na kutokuelewana kati ya Wamiliki hao wawili wa Kimarekani wa Liverpool, Gillett na Hicks, na pia Madeni yaliyoendelea kuongezeka na kuisakama Liverpool tangu Wamarekani hao wainunue Liverpool mwaka 2007.
Robinho aanza kuweweseka?
Mshambuliaji kutoka Brazil, Robinho, amekiri kuwa angependa kuichezea Barcelona lakini mpaka sasa hajapata ofa yeyote kutoka huko Barca.
Robinho alisaini kucheza Manchester City mwaka jana kwa ada ya Pauni Milioni 32 kutoka Real Madrid na ada hiyo ni rekodi kwa ununuzi wa Mchezaji huko Uingereza lakini muda wote mpaka sasa uvumi wa yeye kuhama unamwandama na umezidi kushamiri baada ya Kocha wa Barca Pep Guardiola kuripotiwa akisema angependa kuwa na Mbrazil huyo mwenye miaka 25.
Gazeti la El Mundo Deportivo limemkariri Robinho akisema: “Hakika ntapenda kuchezea Barca! Nani atakataa kucheza huko? Ni furaha kubwa kucheza pamoja na Messi, Mbrazil mwenzangu Dani Alves, Xavi, Iniesta na Ibrahimovic! Barca wanacheza soka tamu kama Timu bora ya Brazil!”
Hata hivyo, Robinho amesema atabaki kuwa na moyo thabiti na Man City kwani bado ni Mchezaji wao.
FIFA U-20 WORLD CUP Egypt 2009:
NI FAINALI: Ghana v Brazil
Ghana wanakutana na Mabingwa mara 4 wa Kombe la Dunia kwa Vijana wa Chini ya Miaka 20, Brazil, kwenye Fainali ya Kombe hilo itakayochezwa Ijumaa Oktoba 16 Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, mjini Cairo, Misri.
Ghana walitinga Fainali baada ya kuifunga kwenye Nusu Fainali Hungary mabao 3-2 na Brazil waliwafunga Costa Rica bao 1-0.
Mwaka 1993, huko Sydney, Australia, Ghana na Brazil zilikutana Fainali na Brazil wakaibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-1.
Kikosi cha Ghana kinaongozwa na Kocha Sellas Tetteh na Nahodha wa Timu hiyo ni Andre Ayew, anaechezea Olympique Marseille ya Ufaransa, na ni mtoto wa Abedi Pele, Mchezaji wa zamani na Supastaa wa Ghana na Afrika nzima.
Kikosi cha Brazil kipo chini ya Kocha Rogerio.
VIKOSI:
Ghana:
Daniel Agyie, Robert Dabuo, Joseph Addo, Samuel Inkoom, Jonathan Mensah, Daniel Addo, David Addy, Ghandy Kassenu, Daniel Opare, Philip Boampong, John Benson, Bright Addae, Gladson Awako, Abeiku Quansah, Emmanuel Agyemang-Badu, Andre Ayew, Mohammed Rabiu, Latif Salif, Ransford osei, Dominic Adiyah
Brazi:
Rafael, Renan Ribeiro, Saulo Douglas, Dalton, Rafael Toloi, Renan, Diogo, Paolo Henrique, Fabricio, Wellington Junior, Bertucci, Alex Teixeira, Maylson, Giuliano, Douglas Costa, Souza, Boquita, Alan Kardec,
Kroenke aongeza kasi ya ununuzi hisa Arsenal!!!
Mmarekani Stan Kroenke ambae ni Mkurugenzi wa Arsenal na vile vile Mmilikiwa wa Hisa za Klabu ya Arsenal ameongeza kasi ya ununuzi wa Hisa zaidi na sasa anamiliki Hisa Asilimia 28.9.
Kufuatana na Sheria za Masoko huko Uingereza, Kroenke akifikisha kumiliki idadi ya Asilimia 29.9 ya Hisa zote za Arsenal atawajibika kutoa ofa ya ununuzi wa Hisa zilizobaki na hilo litamfanya awe ndio Mmiliki pekee wa Klabu ya Arsenal.
Stan Kroenke ni Tajiri wa Kimarekani ambae vile vile ni Mmiliki wa Timu ya Mpira wa Vikapu, NBA, huko Marekani iitwayo Denver Nuggets.
Klabu za Manchester United na Liverpool zote zinamilikiwa na Matajiri wa Kimarekani ambao pia wanamiliki huko Marekani Klabu mbalimbali za Michezo.
Manchester United inamilikiwa na Familia ya Kimarekani ya kina Glazier na Liverpool inamilikiwa na Wamarekani wawili George Gillett na Tom Hicks.

Thursday, 15 October 2009

MZOZO WA KUNG'OA JINO:
FIFA: Fellaini ruksa kuichezea Everton LIGI KUU Jumamosi!!
FIFA imewaruhusu Everton kumchezesha Kiungo wao Marouane Fellaini ambae amekumbwa na mzozo na Nchi yake Ubelgiji baada ya Mchezaji huyo kuondoka kwenye Kambi ya Timu ya Taifa ya Ubelgiji ambayo Jumamosi iliyokwisha ilicheza na Uturuki na jana ilicheza na Estonia na Chama cha Soka cha Ubelgiji [KBVB] kuijulisha Everton kuwa imemfungia Mchezaji huyo siku 5 kuanzia jana kama sheria za FIFA zinavyowapa uwezo.
Fellaini awali, baada ya mechi ya Uturuki Jumamosi iliyopita, aliruhusiwa na Kocha wa Ubelgiji Dick Advocaat kuondoka kambini kwenda kung'oa jino na hivyo kuruhusiwa kutokuwepo kambini kwa ajili ya mechi ya jana lakini inasemekana Kocha huyo alibadili mawazo na kumtaka Mchezaji huyo aendelee kuwepo kambini.
Hata hivyo Fellaini aliondoka kambini na ndipo KBVB ikawatumia faksi Everton kuwajulisha inatumia uwezo wanaopewa na FIFA kumfungia Mchezaji siku 5 kutochezea Klabu yake tangu aondoke kwenye mechi aliyotakiwa kuichezea Nchi yake na hivyo asingeruhusiwa kucheza Ligi Kuu Jumamosi ambapo Everton watacheza na Wolverhampton Wanderers.
Everton ililalamikia hatua hiyo ya KBVB na kusema wao kama Klabu hawahusiki na mzozo binafsi kati ya Mchezaji na Nchi yake.
FIFA leo asubuhi imewaruhusu Everton kumchezesha Fellaini hapo Jumamosi.
LIGI KUU ENGLAND KURUDI KILINGENI WIKIENDI!!!
Baada ya kuwa “mapumzikoni” kwa wiki mbili kupisha Mechi za Kimataifa za michuano ya Kombe la Dunia, wikiendi hii viwanja mbalimbali England vitawaka moto tena kwa mechi za Ligi Kuu England.
Mpaka sasa wakati karibu kila Timu imecheza mechi 8, Chelsea ndie alieshika uongozi akiwa na pointi 21 akifuatiwa na Mabingwa Watetezi Manchester United mwenye 19.
Nafasi ya 3 ipo kwa Tottenham mwenye pointi 16 sawa na Manchester City ingawa Man City wamecheza mechi moja pungufu.
Arsenal na Liverpool wamefungana kwa pointi 15 lakini Arsenal amecheza mechi 7 tu na Liverpool 8.
Mechi za Ligi Kuu zitafuatiwa na zile Mechi Kubwa za Ulaya za UEFA CHAMPIONS LEAGUE siku za Jumanne na Jumatano kwa Arsenal na Liverpool kucheza mechi zao Jumanne na Chelsea na Man U kucheza Jumatano.
RATIBA KAMILI:
LIGI KUU:
Jumamosi, Oktoba 17
Aston Villa v Chelsea [saa 8 na dak 45 mchana]
[saa 11 jioni]
Arsenal v Birmingham
Everton v Wolverhampton
Man United v Bolton
Portsmouth v Tottenham
Soke City v West Ham
Sunderland v Liverpool
Jumapili, Oktoba 18
[saa 9 mchana]
Blackburn v Burnley
Wigan v Man City
Jumatatu, Oktoba 19
[saa 4 usiku]
Fulham v Hull City
UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
[saa 3 dak 45 usiku]
Jumanne, 20 Oktoba 2009
AZ Alkmaar v Arsenal,
Barcelona v Rubin Kazan,
Debrecen v Fiorentina,
Inter Milan v Dynamo Kiev,
Liverpool v Lyon,
Olympiakos v Standard Liege,
Rangers v Unirea Urziceni,
VfB Stuttgart v Sevilla,
Jumatano, 21 Oktoba 2009
Bordeaux v Bayern Munich,
CSKA Moscow v Manchester United
Chelsea v Atletico Madrid,
FC Porto v Apoel Nicosia,
FC Zurich v Marseille,
Juventus v Maccabi Haifa,
Real Madrid v AC Milan,
Wolfsburg v Besiktas,
Argentina, Slovakia, Honduras na Uswisi zitashuka Bondeni 2010!!!
Nchi 8 Ulaya, zikiwemo Ufaransa na Ureno, kwenda Mtoano ili watinge Fainali!!!
Hatimaye Diego Maradona na Argentina yake jana walifanikiwa kuipata nafasi ya 4 na ya mwisho toka Kundi la Nchi za Marekani Kusini na kuingia Fainali ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani baada ya Mario Bolatti kuwafungia bao moja na la ushindi dakika za mwisho ugenini Uruguay.
Wenyeji Uruguay waliohitaji kushinda ili kupata nafasi hiyo waliyoitwaa Argentina wamemaliza wakiwa nafasi ya 5 na sasa wataenda kuvaana na Mshindi wa 4 toka Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Carribean ambae ni Costa Rica ili kupata Timu moja itakayoingia Fainali.
Huko Ulaya, Slovakia na Uswisi zimenyakua nafasi 2 za mwisho za kuingia Fainali moja kwa moja baada ya kumaliza washindi wa Makundi yao.
Slovakia waliifunga Poland 1-0 na Uswisi ilitoka suluhu 0-0 na Israel.
Katika Kundi la Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Carribean, Costa Rica walipokwa tonge mdomoni kwani huku wakiwa wanaongoza 2-1 katika mechi waliyocheza ugenini na USA na wakiichungulia Afrika Kusini ileeeeeee, USA walisawazisha sekunde za mwisho kabisa na kufanya mechi iishe 2-2 na hivyo kuwapa Honduras, walioishinda El Salvador 1-0 huko ugenini,  mwanya wa kuchukua nafasi ya 3 nyuma ya USA na Mexico na hivyo kwenda nao Afrika Kusini.
Sasa Costa Rica watakwaana na Uruguay kupata Timu moja itakayoenda Fainali.
Katika Makundi 9 ya Ulaya, Washindi wa Pili Bora wanane ambao watafanyiwa Droo maalum Jumatatu Oktoba 19 ili kupanga mechi 4 zitakazochezwa nyumbani na ugenini Novemba 14 na Novemba 19 ili kupata Washindi wanne watakaoingia Fainali ni:
-Bosnia-Herzegovina
-France
-Greece
-Portugal
-Republic of Ireland
-Russia
-Slovenia
-Ukraine
LISTI KAMILI YA TIMU ZILIZOINGIA FAINALI YA 2010:
WENYEJI: South Africa
AFRICA: Ghana, Ivory Coast
ASIA: Australia, Japan, North Korea, South Korea
EUROPE: Denmark, England, Germany, Netherlands, Serbia, Spain, Italy, Slovakia, Switzerland.
SOUTH AMERICA: Brazil, Paraguay, Chile, Argentina
NORTH, CENTRAL AMERICA AND CARIBBEAN: United States, Mexico, Honduras
MATOKEO MECHI ZA JANA:
ULAYA:
Kazakstan 1 Croatia 2
Andorra 0 Ukraine 6
Azerbaijan 1 Urusi 1
Ujerumani 1 Finaland 1
Uturuki 2 Armenia 0
Liechtenstein 0 Wales 2
Uswisi 0 Israel 0
Latvia 3 Moldova 2
Greece 2 Luxemborg 1
Italy 3 Cyprus 2
Bulgaria 6 Georgia 2
Ireland 0 Montenegro 0
Lithuania 2 Serbia 1
Romania 3 Faroe Islands 1
Estonia 2 Ubelgiji 0
Poland 0 Slovakia 1
Czech Republic 0 Northern Ireland 0
San Marino 0 Slovenia 3
Denmark 0 Hungary 1
Sweden 4 Albania 1
Ureno 4 Malta 0
Ufaransa 3 Austria 1
England 3 Belarus 0
MAREKANI YA KUSINI:
Peru 1 Bolivia 0
Uruguay 0 Argentina 1
Chile 1 Ecuador 0
Brazil 0 Venezuela 0
Paraguay 0 Colombia 2
MAREKANI YA KATI, KASKAZINI & CARRIBEAN:
El Salvador 0 Honduras 1
Trinidad & Tobago 2 Mexico 2
USA 2 Costa Rica 2

Wednesday, 14 October 2009

Jino lazua balaa kwa Fellaini!!!
Kiungo wa Everton na Ubelgiji, Marouane Fellaini, yuko kwenye mzozo na Chama cha Soka cha Ubelgiji [KBVB] pamoja na Kocha wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji, Dick Advocaat, baada ya kujitoa kwenye Kikosi cha Ubelgiji kilicho kwenye mechi za Mtoano za Kombe la Dunia ambacho Jumamosi kilicheza na Uturuki na leo Jumatano kinapambana na Estonia.
Kocha huyo wa Ubelgiji, Dick Advocaat, mara baada ya mechi ya Jumamosi ambayo Ubelgiji waliifunga Uturuki alimruhusu Fellaini ajitoe Kikosi cha Ubelgiji ili akafanyiwe operesheni ya kung’oa jino la gego lililomsumbua muda mrefu. Lakini, baadae, Kocha huyo alibadili msimamo na kumtaka Fellaini abaki Kambini ili awemo kwenye Kikosi cha kinachopambana na Estonia Jumatano Oktoba 14 mechi ambayo si muhimu kwa Ubelgiji kwa vile haiwezi kuingia Fainali za Kombe la Dunia.
Hata hivyo, Fellaini aliondoka Kambini na kwenda kutibiwa jino lake.
Kitendo hicho cha Fellaini kimewaudhi KBVB na kimewatumia faksi Everton kuwajulisha watatumia sheria ya FIFA inayowapa uwezo kumpiga marufuku Mchezaji huyo kuchezea Klabu yake kwa siku 5 baada ya mechi inayohusu Nchi yake ambayo amejitoa Kikosini.
Endapo KBVB itamfungia Fellaini kwa siku hizo 5 basi hataweza kuichezea Everton kwenye mechi ya Ligi Kuu Jumamosi dhidi ya Wolverhampton Wanderers.
Everton imelalamika kuhusu hatua hiyo ya KBVB na kusema wao kama Klabu hawahusiki kwenye mzozo wa Mchezaji huyo binafsi na Nchi yake.
Megson amtetea Fergie!!
Kocha wa Bolton Wanderers, Gary Megson, ambayo Timu yake itapambana na Manchester United kwenye mechi ya Ligi Kuu hapo Jumamosi, amemtetea Sir Alex Ferguson wa Man U katika mzozo unaoihusu kauli ya Ferguson kusema Refa Alan Wiley aliechezesha mechi ya Man U na Sunderland ‘hayuko fiti’ na kusababisha Chama cha Marefa kumjia juu na pia FA kumtaka Ferguson ajieleze.
Megson amesema: “Wanamwandama kwa vile ni mtu mwenye jina kwenye Soka! Ameomba radhi lakini kila mtu analaumu hata huko kuomba radhi kwake! Asingeomba radhi wangemsema, kaomba radhi wanamsema! Sasa afanyeje? Ameomba radhi huo ungekuwa mwisho wa mzozo!”
Mpaka sasa Sir Alex Ferguson binafsi hajazungumza lolote sakata hilo kwa vile yuko safarini huko New York, Marekani.
FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009
Ghana kuikwaa Brazil Fainali!!!!
Ghana wametinga Fainali ya Kombe la Dunia kwa Vijana wa Chini ya Miaka 20 huko Misri hii ikiwa ni mara yao ya 3 kufika hatua hiyo baada ya kuifunga Hungary mabao 3-2 na sasa watapambana na Brazil walioitoa Costa Rica bao 1-0.
Fainali itachezwa Ijumaa, Oktoba 16 huko mjini Cairo, Misri.
Magoli ya Ghana yalifungwa na Dominic Adiyiah bao 2 na Abeiku Quansah bao moja.
Hungary walipata bao zao kupitia Marko Futacs na Adam Balajti.
Kwenye mechi ya Brazil na Costa Rica, bao la kipindi cha pili la Alan Kardec limeiingiza Brazil Fainali kwa ushindi wa bao 1-0.
Benitez apewa onyo kwa kutoa ishara za Mikono kwa Refa!!!
FA, Chama cha Soka England, kimempa onyo kali Meneja wa Liverpool Rafael Benitez na kumtaka achunge mwenendo wake wa baadae hasa kwenye Mahojiano na Waandishi wa Habari baada ya kupatikana na hatia ya kutumia ishara mbaya ya mikono akimuashiria Refa Phil Dowd kwenye mahojiano baada ya mechi waliyofungwa na Tottenham bao 2-1 hapo Agosti 16.
Ishara ya Benitez inafuatia kuulizwa swali kuhusu Refa Phil Dowd na yeye bila kujibu akatoa mawani yake mfukoni na kuanza kuyachunguza kitendo ambacho FA imekiona ni cha kumdhalilisha Refa.
Benitez alikasirishwa kutokana na kudai kunyimwa penalti mbili na Refa Dowd.
Msaidizi wa Benitez, Sammy Lee, anakabiliwa na mashtaka ya utovu wa nidhamu uliotokea katika mechi hiyo hiyo kati ya Tottenham na Liverpool baada ya kukwaruzana na Refa wa Akiba, Stuart Attwell, kitendo ambacho kilimfanya Refa Phil Dowd amtoe nje ya uwanja Sammy Lee.
Capello: Rio ni muhimu kwa England!!
Kocha wa England Fabio Capello amesema Rio Ferdinand atacheza mechi ya leo ya Kombe la Dunia kati ya England na Belarus licha ya kuundamwa na Vyombo vya Habari wakimtuhumu kufanya kosa lililosababisha Kipa wa England Rob Green atolewe nje kwa Kadi Nyekundu kwenye mechi England waliyofungwa 1-0 na Ukraine Jumamosi iliyopita.
Capello alisema: “ Nimeongea na Rio. Tumeongea kuhusiu mechi iliyopita. Rio ni mtu mzuri, mtu mkubwa na muhimu sana kwa England na Manchester United! Atacheza mechi ya leo. Anahitaji kucheza! Ni mzoefu na mimi namwamini sana!”
Inategemewa leo Capello ataibadili Timu na huenda kina Agbonlahor, Crouch, Beckham na Kipa Ben Foster wakacheza.
Mechi ya leo si muhimu kwa England kwa vile washatinga Fainali Kombe la Dunia.

Tuesday, 13 October 2009

KOMBE LA DUNIA: KIMBEMBE MECHI ZA MWISHO KESHO HUKO ULAYA NA MAREKANI!!!
Huko Ulaya, hapo kesho, baadhi ya Nchi zitajua hatima yao kwenye Kombe la Dunia kwa ama kufuzu moja kwa moja au kuingia Kapu la pili la Mtoano au kubaki kama Watazamaji hapo mwakani wakati Fainali za Kombe la Dunia zikichezwa huko Afrika Kusini.
Huko Marekani ya Kusini kimbembe kipo pia kwa Argentina ya Diego Maradona ambao watakuwa ugenini huko Uruguay wakiwania kuipata nafasi ya 4 kuingia Fainali moja kwa moja na hali yao ni ngumu kwani Uruguay nao wanawania nafasi hiyo hiyo.
LISTI KAMILI YA TIMU AMBAZO TAYARI ZIKO FAINALI YA 2010:
WENYEJI: South Africa
AFRICA: Ghana, Ivory Coast
ASIA: Australia, Japan, North Korea, South Korea
EUROPE: Denmark, England, Germany, Netherlands, Serbia, Spain, Italy
SOUTH AMERICA: Brazil, Paraguay, Chile
NORTH, CENTRAL AMERICA AND CARIBBEAN: United States, Mexico
ULAYA:
Nafasi mbili za kuingia Fainali ziko wazi na ni Switzerland wanaoongoza Kundi la 2 na Slovakia wanaoongoza Kundi la 3 ndio wenye nafasi kubwa kufuzu.
Switzerland wanahitaji suluhu tu kwenye mechi yao ya kesho wakiwa nyumbani watakapocheza na Israel.
Slovakia wako ugenini na ni lazima waifunge Poland kwani wakishindwa tu Slovenia wanaocheza na “vibonde” San Marino, bila shaka, watashinda na kuwapiku.
Kwa Ulaya, Kapu la Pili ni Timu bora 8 zitakazomaliza nafasi za Pili kwenye Makundi yao kufanyiwa Droo maalum hapo Jumatatu Oktoba 19 ili kupanga mechi 4 za Mtoano zitakazochezwa nyumbani na ugenini Jumamosi Novemba 14 na Jumatano Novemba 18 ili kupata Timu 4 zitakazoenda Fainali.
MAREKANI YA KUSINI:
Imebaki nafasi moja ya kuingia Fainali moja kwa moja na moja ya kwenda kwenye Mtoano na Timu itakayomaliza nafasi ya 4 Kundi la Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Carribean.
Mechi ya kesho kati ya Uruguay v Argentina ndio ufunguo wa nani atafuzu kupata hiyo nafasi ya kuingia Fainali moja kwa moja.
Mshindi ndie ataingia Fainali ingawa suluhu kwa Argentina inaweza kuwaingiza Fainali endapo Ecuador akiwa ugenini atashindwa kuifunga Chile kwa mabao 5 bila.
Ikiwa Argentina atafungwa na Ecuador kushinda basi Argentina yuko nje ya Kombe la Dunia kwani hata ile nafasi ya kwenda kucheza Mtoano hatoipata.
MAREKANI YA KATI, KASKAZINI NA CARRIBEAN:
Imebaki nafasi moja ya kuingia Fainali moja kwa moja na moja ya kwenda Mtoano kucheza na Timu ya 5 ya Marekani ya Kusini.
Nafasi hizo zinagombewa na Costa Rica na Honduras.
Ikiwa Honduras atashindwa kuifunga El Salvador ugenini, Costa Rica wataingia Fainali bila kujali matokeo ya mechi yao na USA.
AFRICA:
Nafasi 3 kati ya 5 ndizo zimebaki na mechi za mwisho kwa Kundi hili zitachezwa Novemba 14.
Mpaka sasa Ghana na Ivory Coast wako Fainali na nafsi 3 zilizobaki ni moja kati ya Gabon au Cameroun, Tunisia au Kenya na Misri au Algeria.
Cameroun wako kwenye nafasi nzuri na watafaulu labda wafanye vibaya katika mechi yao na Morocco na Gabon wafanye vizuri ugenini Togo.
Tunisia wako kwenye hali njema na wataanguka tu ikiwa watashindwa kuifunga Mozambique huko Maputo na Nigeria aifunge Kenya huko Nairobi.
Egypt v Algeria ndie itakayoamua nani kati ya hawa anaingia Fainali ingawa Algeria anahitaji suluhu tu.
ASIA & OCEANIA:
Bahrain na New Zealand zilitoka sare 0-0 hapo Oktoba 10 huko Manama, Bahrain na marudiano ni ni Novemba 14 huko Auckland, New Zealand na Mshindi anatinga Fainali.
Sir Alex Ferguson kuwasilisha barua kwa FA kuomba radhi kuhusu Refa Wiley!!!
Baada ya hivi juzi kumtaka radhi Refa Alan Wiley kwa kumwita hayuko fiti, Sir Alex Ferguson sasa anategemewa kuiandikia barua FA ili kuwataka radhi kwa kauli hiyo.
Barua hiyo ndiyo inategemewa kuwa majibu ya barua aliyoandikiwa Ferguson na FA kutakiwa ajieleze kwa kauli yake kuhusu Refa Alan Wiley aliyoitoa mara baada ya mechi ya Ligi Kuu kati ya Manchester United na Sunderland iliyochezwa Oktoba 3 na kumalizika suluhu 2-2.
Kauli ya Ferguson imezua mzozo mkubwa huko England huku Marefa, hasa Chama chao, kikitaka Ferguson apewe adhabu kali.
FA imempa hadi Ijumaa ijayo Sir Alex Ferguson kutoa maelezo yake.
Cannavaro asafishwa, awajia juu waandishi!!
Nahodha wa Italia na Mlinzi wa Juventus, Fabio Cannavaro, amesafishwa na Kamati ya Olimpiki ya Italia kuhusu tuhuma za kutumia Dawa “Cortisone’ ambayo ipo kwenye listi ya dawa marufuku lakini amewajia juu Waandishi wa Magazeti kwa kumhukumu bila kumpa nafasi kujitetea.
Cannavaro aliumwa na Dondola hapo Agosti 28 na kupewa dawa ili kuzuia madhara ya kuumwa na Dondola kwa vile yeye hudhurika lakini wakati Klabu yake Juventus ikimwombea kibali cha kutumia dawa hiyo marufuku alipimwa na kugundulika ametumia dawa marufuku na ndipo alipoitwa kwenye Kamati ya Olimpiki kujieleza.
Cannavaro, alieonyesha hasira, alibwata: “Unaumwa na Mdudu na watu wanakuona unatumia Madawa marufuku! Baadhi ya Magazeti yalizidi kipimo!”

Monday, 12 October 2009

FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009
Kesho Nusu Fainali!!
Mashindano ya Kombe la Dunia kwa Vijana wa Chini ya Miaka 20 yanayochezwa huko Misri kesho yapo Nusu Fainali na mechi zote mbili zitachezwa hiyo kesho kwa Brazil kukutana na Costa Rica na Ghana kucheza na Hungary.
Fainali ni Ijumaa tarehe 16 Oktoba 2009.
Hargreaves: Nipo imara!!
Mchezaji wa Manchester United Owen Hargreaves amsema hana wasiwasi na atarudi uwanjani, baada ya kuwa nje kwa zaidi ya mwaka mmoja alipokuwa akitibiwa magoti yake, akiwa bora na fiti zaidi.
Mechi ya mwisho Hargreaves kuichezea Klabu yake ilikuwa dhidi ya Chelsea miezi 13 iliyopita na baada ya hapo alipelekwa Marekani kufanyiwa upasuaji magoti yake yote mawili kwenye Kliniki ya Dr Richard Steadman ambae ni Mtaalam aliewatibu kina Tiger Woods, Alan Shearer, Michael Owen na Ruud van Nistelrooy magoti kwa kutumia upasuaji na matibabu ya kisasa kabisa.
Hargreaves amesema: “Nitajitahidi nipate mafanikio! Nataka nilipe fadhila kwa Mashabiki kwa kuwa na imani na mimi!”

Ben Foster aitwa Kikosi cha England, Rooney ajitoa!
Kocha wa England, Fabio Capello, amemwita Kipa wa Manchester United Ben Foster kwenye Kikosi cha England kitakachocheza mechi ya mwisho ya Kundi lao Uwanjani Wembley Jumatano na Belarus ili kuchukua nafasi ya Robert Green aliefungiwa mechi hiyo baada ya kupewa Kadi Nyekundu katika mechi na Ukraine Jumamosi iliopita ambayo England walifungwa 1-0.
Mechi haina umuhimu wowote kwa England ambao tayari wako Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini.
Ben Foster hakuchaguliwa kwenye Kikosi cha England kilichocheza na Ukraine na ilitolewa sababu kuwa alikuwa majeruhi ingawa dhana ya wengi ni fomu yake hasa baada ya kuifungisha Manchester United kwenye mechi za Ligi Kuu walizocheza na Manchester City na Sunderland.
Wakati huohuo, Straika Wayne Rooney amejitoa kwenye Kikosi cha England baada ya kuumia musuli ya mguu nyuma ya ugoko.
Heskey: Ntahama Villa ili niende Fainali Kombe la Dunia!!
Emile Heskey ametoboa kuwa ikifika Januari wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa ataomba kuihama Klabu yake Aston Villa ikiwa hachezeshwi ili kwenda Klabu nyingine atayopata namba kwa sababu anataka kuweka hai nafasi yake kuichezea England Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani.
Jumamosi Emile Heskey alianza kwenye Kikosi cha England kilichofungwa na Ukraine 1-0 ikiwa ni mara yake ya 57 kuichezea England na ni mara ya 3 msimu huu kuichezea England lakini Klabuni kwake Aston Villa ameanza mechi moja tu msimu huu.
Aston Villa mara nyingi huwaanzisha Gabriel Agbonlahor na John Carew.
Heskey alihamia Aston Villa akitokea Wigan Januari mwaka huu.
MATOKEO KOMBE LA DUNIA:
Oktoba 11:
AFRIKA:
Benin 1 v Ghana 0
Nigeria 1 v Mozambique 0
Tunisia 1 v Kenya 0
Guinea 1 v Burkina Faso 2
Mali 1 v Sudan 0
Algeria 3 v Rwanda 1
MAREKANI YA KUSINI:
Bolivia 2 Brazil 1

Sunday, 11 October 2009

Wenger aambiwa muda wa kusubiri umekwisha, leta Kombe Emirates!!!
Arsene Wenger amejulishwa na Wamiliki wa Arsenal kuwa wamechoka kusubiri na msimu huu hamna subira na wanataka kuona Kombe linatua Uwanjani Emirates.
Tangu wachukue Kombe la FA mwaka 2005, Arsenal hawajanyakua tena Kombe lolote lile ingawa kosakosa ni nyingi na wana Kikosi cha Vijana wanaotandaza ‘Soka Tamu’ linalovutia Ulaya nzima.
Mkurugenzi Mtendaji wa Arsenal, Ivan Gazidis, amesema: “Ni lengo letu kuchukua Kikombe msimu huu! Kumaliza nafasi ya pili, tatu au nne si bora kwetu! Tuna imani tuna Kikosi kizuri!”
Gazidis, mwenye asili ya Afrika Kusini, aliingizwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Arsenal Novemba 2008, amesisitiza kuwa ingawa Soka ni biashara kubwa haiwezi kusahaulika kuwa Arsenal wapo hapo kwa ajili ya Mashabiki wao ambao hawajali Mahesabu mazuri ya Fedha bali hutaka ushindi uwanjani.
NANI KATINGA BONDENI 2010 JANA?
Ifuatayo ni taarifa nani ameingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani:
UNITED STATES (11 Oktoba, 2009)
USA walipata ushindi wa ugenini hapo jana walipowafunga Honduras 3-2 n kupata tiketi ya kwenda Afrika Kusini huku wakiwa na mechi moja mkononi.
MEXICO (11 Oktoba, 2009)
Mexico wamejihakikishia kucheza Fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya 14 huku wakiwa na mechi moja mkononi walipowafunga El Salvador 4-1 hapo jana.
CHILE (11 Oktoba, 2009)
Chile watatua Afrika Kusini baada ya kuifunga Colombia 4-2 na hii itakuwa ni mara yao ya kwanza tangu 1998.
ITALY (10 Oktoba, 2009)
Mabingwa Watetezi Italia walipata suluhu ya 2-2 ugenini huko Dublin, Ireland waliposawazisha bao dakika ya mwisho na kutinga Fainali za Kombe la Dunia kutetea taji lao.
SERBIA (10 Oktoba, 2009)
Serbia hapo jana waliwakung’uta Romania 5-0 mjini Belgrade na kuingia Fainali za 2010 huko bondeni.
DENMARK (10 Oktoba, 2009)
Baada ya kuwachomeka bao 1-0 Mahasimu wao wakubwa, Sweden, mjini Copenhagen, Denmark sasa wako Fainali huko Afrika Kusini.
GERMANY (10 Oktoba, 2009)
Tangu mwaka 1950, Germany hawajaikosa hata Fainali moja ya Kombe la Dunia na jana wakiwa ugenini huko Moscow, Urusi, waliwashinda Wenyeji wao Urusi bao 1-0 na kutinga Fainali kama desturi yao.
IVORY COAST (10 Oktoba, 2009)
Ivory Coast walitoka suluhu 1-1 na Malawi mjini Blantyre na hiyo ilikuwa tosha kuingia Fainali Afrika Kusini huku wakiwa na mechi moja mkononi.
LISTI KAMILI YA TIMU ZILIZOINGIA FAINALI YA 2010:
WENYEJI: South Africa
AFRICA: Ghana, Ivory Coast
ASIA: Australia, Japan, North Korea, South Korea
EUROPE: Denmark, England, Germany, Netherlands, Serbia, Spain, Italy
SOUTH AMERICA: Brazil, Paraguay, Chile
NORTH, CENTRAL AMERICA AND CARIBBEAN: United States, Mexico
MATOKEO MECHI ZA Oktoba 10:
Afrika:
Ivory Coast yaingia Fainali!
Zambia 0 v Egypt 1
Malawi 1 v Ivory Coast 1
Cameroun 3 v Togo 0
Gabon 3 v Morocco 1
Asia na Oceania:
Bahrain 0 New Zealand 0
[Marudio huko New Zealand]
MECHI ZA LEO Oktoba 11:
Benin v Ghana
Nigeria v Mozambique
Tunisia v Kenya
Guinea v Burkina Faso
Mali v Sudan
Algeria v Rwanda
Ulaya:
Oktoba 10:
Finland 2 v Wales 1
Luxemborg 0 v Switzerland 3
Belarus 4 v Kazakhstan 0
Russia 0 v Germany 1
Estonia 0 v Bosnia-Herzegovina 2
Montenegro 2 v Georgia 1
Ukraine 0 v England 1
Denmark 1 v Sweden 0
Liechtenstein 0 v Azerbaijan 2
Republic of Ireland 2 v Italy 2
Czech Republic 2 v Poland 0
Slovakia 0 v Slovenia 2
Austria 2 v Lithuania 1
Serbia 5 v Romania 0
Portugal 3 v Hungary 0
Belgium 2 v Turkey 0
Israel 3 v Moldova 1
Armenia 1 v Spain 2
France 5 v Faroe Islands 0
Greece 5 v Latvia 2
Marekani ya Kusini:
Oktoba 10:
Colombia 2 v Chile 4
Ecuador 1 v Uruguay 2
Venezuela 1 v Paraguay 2
Argentina 2 v Peru 1
Oktoba 11:
Bolivia v Brazil
FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009
Brazil na Costa Rica zatinga Nusu Fainali!!!
MATOKEO MECHI ZA Jumamosi, Oktoba 10:
Brazil 2 v Germany 1
UAE 1 v Costa Rica 2
NUSU FAINALI:
Oktoba 13:
Ghana v Hungary
Brazil v Costa Rica
FAINALI:
Oktoba 16
Powered By Blogger