Thursday 15 October 2009

Argentina, Slovakia, Honduras na Uswisi zitashuka Bondeni 2010!!!
Nchi 8 Ulaya, zikiwemo Ufaransa na Ureno, kwenda Mtoano ili watinge Fainali!!!
Hatimaye Diego Maradona na Argentina yake jana walifanikiwa kuipata nafasi ya 4 na ya mwisho toka Kundi la Nchi za Marekani Kusini na kuingia Fainali ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani baada ya Mario Bolatti kuwafungia bao moja na la ushindi dakika za mwisho ugenini Uruguay.
Wenyeji Uruguay waliohitaji kushinda ili kupata nafasi hiyo waliyoitwaa Argentina wamemaliza wakiwa nafasi ya 5 na sasa wataenda kuvaana na Mshindi wa 4 toka Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Carribean ambae ni Costa Rica ili kupata Timu moja itakayoingia Fainali.
Huko Ulaya, Slovakia na Uswisi zimenyakua nafasi 2 za mwisho za kuingia Fainali moja kwa moja baada ya kumaliza washindi wa Makundi yao.
Slovakia waliifunga Poland 1-0 na Uswisi ilitoka suluhu 0-0 na Israel.
Katika Kundi la Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Carribean, Costa Rica walipokwa tonge mdomoni kwani huku wakiwa wanaongoza 2-1 katika mechi waliyocheza ugenini na USA na wakiichungulia Afrika Kusini ileeeeeee, USA walisawazisha sekunde za mwisho kabisa na kufanya mechi iishe 2-2 na hivyo kuwapa Honduras, walioishinda El Salvador 1-0 huko ugenini,  mwanya wa kuchukua nafasi ya 3 nyuma ya USA na Mexico na hivyo kwenda nao Afrika Kusini.
Sasa Costa Rica watakwaana na Uruguay kupata Timu moja itakayoenda Fainali.
Katika Makundi 9 ya Ulaya, Washindi wa Pili Bora wanane ambao watafanyiwa Droo maalum Jumatatu Oktoba 19 ili kupanga mechi 4 zitakazochezwa nyumbani na ugenini Novemba 14 na Novemba 19 ili kupata Washindi wanne watakaoingia Fainali ni:
-Bosnia-Herzegovina
-France
-Greece
-Portugal
-Republic of Ireland
-Russia
-Slovenia
-Ukraine
LISTI KAMILI YA TIMU ZILIZOINGIA FAINALI YA 2010:
WENYEJI: South Africa
AFRICA: Ghana, Ivory Coast
ASIA: Australia, Japan, North Korea, South Korea
EUROPE: Denmark, England, Germany, Netherlands, Serbia, Spain, Italy, Slovakia, Switzerland.
SOUTH AMERICA: Brazil, Paraguay, Chile, Argentina
NORTH, CENTRAL AMERICA AND CARIBBEAN: United States, Mexico, Honduras
MATOKEO MECHI ZA JANA:
ULAYA:
Kazakstan 1 Croatia 2
Andorra 0 Ukraine 6
Azerbaijan 1 Urusi 1
Ujerumani 1 Finaland 1
Uturuki 2 Armenia 0
Liechtenstein 0 Wales 2
Uswisi 0 Israel 0
Latvia 3 Moldova 2
Greece 2 Luxemborg 1
Italy 3 Cyprus 2
Bulgaria 6 Georgia 2
Ireland 0 Montenegro 0
Lithuania 2 Serbia 1
Romania 3 Faroe Islands 1
Estonia 2 Ubelgiji 0
Poland 0 Slovakia 1
Czech Republic 0 Northern Ireland 0
San Marino 0 Slovenia 3
Denmark 0 Hungary 1
Sweden 4 Albania 1
Ureno 4 Malta 0
Ufaransa 3 Austria 1
England 3 Belarus 0
MAREKANI YA KUSINI:
Peru 1 Bolivia 0
Uruguay 0 Argentina 1
Chile 1 Ecuador 0
Brazil 0 Venezuela 0
Paraguay 0 Colombia 2
MAREKANI YA KATI, KASKAZINI & CARRIBEAN:
El Salvador 0 Honduras 1
Trinidad & Tobago 2 Mexico 2
USA 2 Costa Rica 2

No comments:

Powered By Blogger