Saturday 17 October 2009

Tevez atishia kujitoa Timu ya Taifa Argentina!!!
Wakati Kocha wake wa Argentina, Diego Maradona, yuko kwenye uchunguzi wa Kamati ya Nidhamu ya FIFA kwa kutukana akiwa kwenye TV laivu, Mchezaji wa Argentina Carlos Tevez ametishia kujitoa kuichezea Argentina kwa madai kuwa wanaandamwa na kusemwa bila msingi.
Tevez amesema: “Nikiichezea Argentina muda mwingi Napata karaha kuliko kupata raha! Mashabiki wanatutukana, Waandishi wanaponda kila kitu chetu! Nimechoka na haya yote! Sasa nafikiria kujitoa! Kwa nini nije Argentina ili kupata shida?”
Ufaransa, Ureno, Urusi na Ugiriki kutocheza kati yao mechi za Mtoano za Kombe la Dunia!!!!
Jumatatu inapangwa Droo maalum ili kupata mechi 4 zitakazochezwa na Nchi za Ulaya zilizoshika nafasi ya pili kwenye Makundi yao ya Kombe la Dunia ili kupata Nchi 4 zitakazoenda Fainali Kombe la Dunia na Timu zinazohusika kwenye Droo hiyo ni Ufaransa, Ureno, Urusi, Ugiriki, Republic of Ireland, Slovenia, Ukraine na Bosnia-Herzegovina.
Kufuatia FIFA kutangaza Listi ya Ubora Duniani, huku Brazil akiwa nambari wani, Nchi za Ufaransa, Ureno, Urusi na Ugiriki zimeibuka kuwa mbele ya Republic of Ireland, Bosnia, Slovenia na Ukraine na hivyo hii inamaanisha Ufaransa, Ureno, Urusi na Ugiriki haziwezi kupangwa kukutana kati yao kwenye Mechi hizo za Mtoano.
Hivyo Nchi hizo zitawekwa Kapu la Kwanza na Republic of Ireland, Bosnia. Slovenia na Ukraine zitakuwa Kapu la Pili na Nchi za Kapu la Kwanza zitapambanishwa na Nchi za Kapu la Pili.
Mechi hizo za Mtoano zitachezwa nyumbani na ugenini hapo Novemba 14 na Novemba 18.
Huko Ulaya tayari Nchi za Denmark, England, Germany, Netherlands, Serbia, Spain, Italy, Slovakia, Switzerland zimeshatinga Fainali Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010 baada kuongoza Makundi yao.

No comments:

Powered By Blogger