Wednesday 14 October 2009

FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009
Ghana kuikwaa Brazil Fainali!!!!
Ghana wametinga Fainali ya Kombe la Dunia kwa Vijana wa Chini ya Miaka 20 huko Misri hii ikiwa ni mara yao ya 3 kufika hatua hiyo baada ya kuifunga Hungary mabao 3-2 na sasa watapambana na Brazil walioitoa Costa Rica bao 1-0.
Fainali itachezwa Ijumaa, Oktoba 16 huko mjini Cairo, Misri.
Magoli ya Ghana yalifungwa na Dominic Adiyiah bao 2 na Abeiku Quansah bao moja.
Hungary walipata bao zao kupitia Marko Futacs na Adam Balajti.
Kwenye mechi ya Brazil na Costa Rica, bao la kipindi cha pili la Alan Kardec limeiingiza Brazil Fainali kwa ushindi wa bao 1-0.
Benitez apewa onyo kwa kutoa ishara za Mikono kwa Refa!!!
FA, Chama cha Soka England, kimempa onyo kali Meneja wa Liverpool Rafael Benitez na kumtaka achunge mwenendo wake wa baadae hasa kwenye Mahojiano na Waandishi wa Habari baada ya kupatikana na hatia ya kutumia ishara mbaya ya mikono akimuashiria Refa Phil Dowd kwenye mahojiano baada ya mechi waliyofungwa na Tottenham bao 2-1 hapo Agosti 16.
Ishara ya Benitez inafuatia kuulizwa swali kuhusu Refa Phil Dowd na yeye bila kujibu akatoa mawani yake mfukoni na kuanza kuyachunguza kitendo ambacho FA imekiona ni cha kumdhalilisha Refa.
Benitez alikasirishwa kutokana na kudai kunyimwa penalti mbili na Refa Dowd.
Msaidizi wa Benitez, Sammy Lee, anakabiliwa na mashtaka ya utovu wa nidhamu uliotokea katika mechi hiyo hiyo kati ya Tottenham na Liverpool baada ya kukwaruzana na Refa wa Akiba, Stuart Attwell, kitendo ambacho kilimfanya Refa Phil Dowd amtoe nje ya uwanja Sammy Lee.
Capello: Rio ni muhimu kwa England!!
Kocha wa England Fabio Capello amesema Rio Ferdinand atacheza mechi ya leo ya Kombe la Dunia kati ya England na Belarus licha ya kuundamwa na Vyombo vya Habari wakimtuhumu kufanya kosa lililosababisha Kipa wa England Rob Green atolewe nje kwa Kadi Nyekundu kwenye mechi England waliyofungwa 1-0 na Ukraine Jumamosi iliyopita.
Capello alisema: “ Nimeongea na Rio. Tumeongea kuhusiu mechi iliyopita. Rio ni mtu mzuri, mtu mkubwa na muhimu sana kwa England na Manchester United! Atacheza mechi ya leo. Anahitaji kucheza! Ni mzoefu na mimi namwamini sana!”
Inategemewa leo Capello ataibadili Timu na huenda kina Agbonlahor, Crouch, Beckham na Kipa Ben Foster wakacheza.
Mechi ya leo si muhimu kwa England kwa vile washatinga Fainali Kombe la Dunia.

No comments:

Powered By Blogger