Tuesday 13 October 2009

KOMBE LA DUNIA: KIMBEMBE MECHI ZA MWISHO KESHO HUKO ULAYA NA MAREKANI!!!
Huko Ulaya, hapo kesho, baadhi ya Nchi zitajua hatima yao kwenye Kombe la Dunia kwa ama kufuzu moja kwa moja au kuingia Kapu la pili la Mtoano au kubaki kama Watazamaji hapo mwakani wakati Fainali za Kombe la Dunia zikichezwa huko Afrika Kusini.
Huko Marekani ya Kusini kimbembe kipo pia kwa Argentina ya Diego Maradona ambao watakuwa ugenini huko Uruguay wakiwania kuipata nafasi ya 4 kuingia Fainali moja kwa moja na hali yao ni ngumu kwani Uruguay nao wanawania nafasi hiyo hiyo.
LISTI KAMILI YA TIMU AMBAZO TAYARI ZIKO FAINALI YA 2010:
WENYEJI: South Africa
AFRICA: Ghana, Ivory Coast
ASIA: Australia, Japan, North Korea, South Korea
EUROPE: Denmark, England, Germany, Netherlands, Serbia, Spain, Italy
SOUTH AMERICA: Brazil, Paraguay, Chile
NORTH, CENTRAL AMERICA AND CARIBBEAN: United States, Mexico
ULAYA:
Nafasi mbili za kuingia Fainali ziko wazi na ni Switzerland wanaoongoza Kundi la 2 na Slovakia wanaoongoza Kundi la 3 ndio wenye nafasi kubwa kufuzu.
Switzerland wanahitaji suluhu tu kwenye mechi yao ya kesho wakiwa nyumbani watakapocheza na Israel.
Slovakia wako ugenini na ni lazima waifunge Poland kwani wakishindwa tu Slovenia wanaocheza na “vibonde” San Marino, bila shaka, watashinda na kuwapiku.
Kwa Ulaya, Kapu la Pili ni Timu bora 8 zitakazomaliza nafasi za Pili kwenye Makundi yao kufanyiwa Droo maalum hapo Jumatatu Oktoba 19 ili kupanga mechi 4 za Mtoano zitakazochezwa nyumbani na ugenini Jumamosi Novemba 14 na Jumatano Novemba 18 ili kupata Timu 4 zitakazoenda Fainali.
MAREKANI YA KUSINI:
Imebaki nafasi moja ya kuingia Fainali moja kwa moja na moja ya kwenda kwenye Mtoano na Timu itakayomaliza nafasi ya 4 Kundi la Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Carribean.
Mechi ya kesho kati ya Uruguay v Argentina ndio ufunguo wa nani atafuzu kupata hiyo nafasi ya kuingia Fainali moja kwa moja.
Mshindi ndie ataingia Fainali ingawa suluhu kwa Argentina inaweza kuwaingiza Fainali endapo Ecuador akiwa ugenini atashindwa kuifunga Chile kwa mabao 5 bila.
Ikiwa Argentina atafungwa na Ecuador kushinda basi Argentina yuko nje ya Kombe la Dunia kwani hata ile nafasi ya kwenda kucheza Mtoano hatoipata.
MAREKANI YA KATI, KASKAZINI NA CARRIBEAN:
Imebaki nafasi moja ya kuingia Fainali moja kwa moja na moja ya kwenda Mtoano kucheza na Timu ya 5 ya Marekani ya Kusini.
Nafasi hizo zinagombewa na Costa Rica na Honduras.
Ikiwa Honduras atashindwa kuifunga El Salvador ugenini, Costa Rica wataingia Fainali bila kujali matokeo ya mechi yao na USA.
AFRICA:
Nafasi 3 kati ya 5 ndizo zimebaki na mechi za mwisho kwa Kundi hili zitachezwa Novemba 14.
Mpaka sasa Ghana na Ivory Coast wako Fainali na nafsi 3 zilizobaki ni moja kati ya Gabon au Cameroun, Tunisia au Kenya na Misri au Algeria.
Cameroun wako kwenye nafasi nzuri na watafaulu labda wafanye vibaya katika mechi yao na Morocco na Gabon wafanye vizuri ugenini Togo.
Tunisia wako kwenye hali njema na wataanguka tu ikiwa watashindwa kuifunga Mozambique huko Maputo na Nigeria aifunge Kenya huko Nairobi.
Egypt v Algeria ndie itakayoamua nani kati ya hawa anaingia Fainali ingawa Algeria anahitaji suluhu tu.
ASIA & OCEANIA:
Bahrain na New Zealand zilitoka sare 0-0 hapo Oktoba 10 huko Manama, Bahrain na marudiano ni ni Novemba 14 huko Auckland, New Zealand na Mshindi anatinga Fainali.
Sir Alex Ferguson kuwasilisha barua kwa FA kuomba radhi kuhusu Refa Wiley!!!
Baada ya hivi juzi kumtaka radhi Refa Alan Wiley kwa kumwita hayuko fiti, Sir Alex Ferguson sasa anategemewa kuiandikia barua FA ili kuwataka radhi kwa kauli hiyo.
Barua hiyo ndiyo inategemewa kuwa majibu ya barua aliyoandikiwa Ferguson na FA kutakiwa ajieleze kwa kauli yake kuhusu Refa Alan Wiley aliyoitoa mara baada ya mechi ya Ligi Kuu kati ya Manchester United na Sunderland iliyochezwa Oktoba 3 na kumalizika suluhu 2-2.
Kauli ya Ferguson imezua mzozo mkubwa huko England huku Marefa, hasa Chama chao, kikitaka Ferguson apewe adhabu kali.
FA imempa hadi Ijumaa ijayo Sir Alex Ferguson kutoa maelezo yake.
Cannavaro asafishwa, awajia juu waandishi!!
Nahodha wa Italia na Mlinzi wa Juventus, Fabio Cannavaro, amesafishwa na Kamati ya Olimpiki ya Italia kuhusu tuhuma za kutumia Dawa “Cortisone’ ambayo ipo kwenye listi ya dawa marufuku lakini amewajia juu Waandishi wa Magazeti kwa kumhukumu bila kumpa nafasi kujitetea.
Cannavaro aliumwa na Dondola hapo Agosti 28 na kupewa dawa ili kuzuia madhara ya kuumwa na Dondola kwa vile yeye hudhurika lakini wakati Klabu yake Juventus ikimwombea kibali cha kutumia dawa hiyo marufuku alipimwa na kugundulika ametumia dawa marufuku na ndipo alipoitwa kwenye Kamati ya Olimpiki kujieleza.
Cannavaro, alieonyesha hasira, alibwata: “Unaumwa na Mdudu na watu wanakuona unatumia Madawa marufuku! Baadhi ya Magazeti yalizidi kipimo!”

No comments:

Powered By Blogger