Saturday, 17 October 2009

Liverpool leo bila Gerrard na Torres!!
Klabu ya Liverpool leo itashuka Uwanjani ugenini huko Stadium of Light kucheza na Sunderland kwenye Ligi Kuu England bila ya Nyota wao Nahodha Steven Gerrard na Straika Fernando Torres walioumia kwenye mechi za Nchi zao za Kombe la Dunia wikiendi iliyopita.
Wote, Gerrard na Torres, hawakuzichezea mechi za Kombe la Dunia za England na Spain Jumatano.
Rooney nje mechi ya Man U leo!!
Sir Alex Ferguson amethibitisha kuwa Mshambuliaji wa Manchster United, Wayne Rooney, hawezi kucheza mechi ya leo ya Ligi Kuu dhidi ya Bolton baada ya kuumia kwenye mechi ya England na Ukraine ya Kombe la Dunia Jumamosi iliyopita huko Ukraine.
Rooney hakucheza mechi ya England ya Jumatano waliyocheza na Estonia Wembley Stadium.
Vilevile, Sir Alex Ferguson amethibitisha kuwa Mshambuliaji mwingine, Dimitar Berbatov, alikuwa bado hajarudi toka kwao Bulgaria alikoichezea Nchi yake Jumatano na kuifungia bao 3 kwenye mechi ya Kombe la Dunia Bulgaria iliyoifunga Georgia bao 6-2.
Berbatov imebidi abaki kwao kwa vile Mpenzi wake anategemewa kujifungua mtoto wao.
Kukosekana kwa Rooney na Berbatov sasa kunampa mwanya Michael Owen kucheza leo.
Ferguson pia amethibitisha Kipa Edwin van der Sar atacheza mechi hiyo na Bolton ikiwa ni mara yake ya kwanza kucheza msimu huu baada ya kuvunjika na kufanyiwa operesheni ya mfupa wa mkononi kwenye mechi kugombea Kombe la Audi huko Ujerumani Man U walipocheza na Bayern Munich.
FIFA U-20 WORLD CUP Egypt 2009:
Ghana BINGWA!!!
Wanyakua Kombe kwa Matuta 4-3!!!
Ghanawamefanikiwa kutwaa Kombe la Dunia kwa Vijana wa Chini ya Miaka 20 walipoishinda Brazil kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya mechi kwisha 0-0 dakika 90 na kuongezwa dakika 30 bila Timu kupata bao.
Mchezaji wa Ghana, Dominic Adiyiah, alitunukiwa Mpira wa Dhahabu kwa kuibuka Mfungaji Bora wa Mashindano hayo akiwa amefunga bao 8.
FIFA yamchunguza Maradona!
Kocha wa Argentina, Diego Maradona, yupo kwenye uchunguzi na FIFA baada ya kubwata matusi mara baada ya Argentina kushinda huko ugenini Uruguay bao 1-0 na kufanikiwa kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrka Kusini mwakani.
Matusi ya Maradona akiwa kwenye TV iliyokuwa ikirusha matangazo laivu yaliwalenga Waandishi wa Habari na Watu wanaompinga.
Rais wa FIFA, Sepp Blatter, amesema hawana njia nyingine ila kuitaka Kamati ya Nidhamu kumchunguza.
Maradona, miaka 48, akipatikana na hatia atafungiwa mechi 5 na kupigwa faini.
Lakini, Mkuu wa Chama cha Soka cha Argentina, Julio Grondona, amemtetea Maradona kwa kudai ingekuwa Kocha mwingine hatua hiyo ya FIFA isingechukuliwa.
Maradona mwenyewe, ingawa amekataa kuomba radhi, ameahidi kutorudia vitendo hivyo na pia aliombamsamaha kwa Wanawake wote, Mama yake, Wanawake wa Argentina na Uruguay pamoja na Dunia nzima.
Chelsea kukata rufaa kupinga kifungo chao!!
Chelsea imetangaza kuwa itakata rufaa CAS [Court of Arbitration for Sports], Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo, kupinga kifungo walichopewa na FIFA cha kutosajili Wachezaji hadi 2011 baada ya kupatikana na hatia ya kumsajili na kumrubuni Chipukizi Gael Kakuta, miaka 18, avunje mkataba wake na Klabu ya Ufaransa Lens mwaka 2007.
Chelsea wamebakisha siku 10 za kukata rufaa.
Mbali ya kufungiwa kutosajili, Chelsea waliamriwa wailipe Lens fidia ya Euro 130,000 kama gharama zao za kumfundisha Gael Kakuta huku Mchezaji huyo akitakiwa ailipe Lens Euro 780,000 kama fidia.

No comments:

Powered By Blogger