Saturday 3 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Argentina yasagwa na Mashine ya Kijerumani!!
Germany 4 Argentina 0
Ni wachache mno walioipa Germany nafasi yeyote katika Fainali hizi za Kombe la Dunia lakini baada ya kuibomoa England bao 4-1 leo huko Cape Town Uwanja wa Green Park walishusha kipondo kikubwa kwa Timu ya Maradona, Argentina, iliyokuwa ikisifiwa na wengi kwa kuisaga kwa mabao 4-0 na kutinga Nusu Fainali.
Germany, wakitumia staili ile ile ya kaunta ataki huku Wachezaji wao Viungo wakibadilishana pozisheni kila sekunde kiasi hujui nani anacheza wapi, waliizidi Argentina kwa muda mrefu wa gemu hi na kuwafunika kabisa Masupastaa Lionel Messi, Tevez, Mascherano na wenzao.
Ilichukua dakika 3 kwa Germany kupata bao kupitia Thomas Muller aliefunga kwa kichwa toka frikiki ya Schweinsteiger.
Hadi mapumziko Germany 1 Argentina 0.
Kipindi cha Pili ndipo mashine ya Kijerumani ikapata kasi na kutingisha bao 3.
Bao la pili alifunga Miroslav Klose dakika ya 68 kutoka pasi murua ya Podolski na kumkuta akiwa na nyavu tu mbele yake.
Dakika ya 74 Friedrich akapachika bao la 3 kutoka pande la Schweinsteiger na Klose akapata bao lake la pili na la 4 kwa Germany kwenye dakika ya 88.
Nusu Fainali Germany watacheza na Mshindi kati ya Spain v Paraguay.
Timu:
German: Neuer, Lahm, Mertesacker, Boateng, Friedrich, Schweinsteiger, Khedira, Muller, Ozil, Podolski, Klose.
Akiba: Wiese, Jansen, Aogo, Tasci, Kiessling, Badstuber, Trochowski, Kroos, Cacau, Marin, Butt, Gomez.
Argentina: Romero, Otamendi, Demichelis, Burdisso, Heinze, Maxi, Mascherano, Di Maria, Messi, Higuain, Tevez.
Akiba: Pozo, Rodriguez, Bolatti, Veron, Garce, Samuel, Aguero, Gutierrez, Palermo, Milito, Andujar,
Refa: Ravshan Irmatov (Uzbekistan)
CHEKI: www.sokainbongo.com

Suarez kukiona cha moto na FIFA kwa ‘Ujangili’!
FIFA imetamka kuwa licha ya Luis Suarez wa Uruguay kutumikia adhabu ya kutocheza mechi moja baada ya kupewa Kadi Nyekundu aliposhika kwa makusudi kwenye mstari wa goli kuwazuia Ghana wasipate bao la ushindi na hatimaye Timu yake kuitoa Ghana kwa mikwaju ya penalti, huenda akafungiwa mechi zaidi baada ya kukaa kwa Kamati ya Nidhamu ya FIFA.
Suarez ataikosa mechi ya Nusu Fainali dhidi ya Holland na huenda pia akaikosa Fainali ikiwa Uruguay itafuzu au mechi ya Mshindi wa Tatu ikiwa watafungwa na Holland.
Huko kwao Suarez ni shujaa lakini kwa FIFA, chini ya Kampeni ya ‘Uchezaji wa Haki’ [Fair Play], ni jangili kwani ‘Uchezaji wa Haki’ tamko lake ni: “Ushindi hauna thamani ikiwa ushindi huo umepatikana kwa njia siyo ya haki au kwa udanganyifu. Kudanganya ni rahisi lakini hakuleti furaha.”
Gyan apozwa na Mandela
Staa wa Ghana, Asamoah Gyan, ambae alikosa penalti ya dakika ya 119 ambayo ingewapa ushindi wa bao 2-1 na hatimaye wakatolewa kwa mikwaju ya penalti na Uruguay, ametumiwa ujumbe wa kumpa pole na kumtuliza kutoka kwa Nelson Mandela.
Kabla ya mechi hiyo na Uruguay, Mandela alituma barua ya kuwaunga mkono Ghana na kuwatakia heri.
Nae Kocha wa Ghana, Milovan Rajevac, alizungumza: “Ule ni ukatili. Lakini ndio Soka. Utamwambia nini Gyan? Tulikuwa karibu mno kuweka historia lakini haikutokea. Kulikuwa na wakati ilijionyesha kama vile kuna mkono wa Mtu anaekontroli ile gemu!”
CHEKI: www.sokainbongo.com

Suarez adai ni ‘Mkono wa Mungu!’
Luis Suarez wa Uruguay amesema hatua yake ya kushika mpira kwenye mstari wa goli ili kuokoa kichwa cha Dominic Adiyiah dakika ya 119 ulikuwa ni ‘Mkono wa Mungu’ kwa vile Uruguay imefanikiwa kuingia Nusu Fainali baada ya kushinda mikwaju ya penalti 4-2 dhidi ya Ghana.
Laiti kama Suarez, anaecheza Ajax huko Uholanzi, asingeshika hilo lingekuwa bao la pili na la ushindi kwani muda ulikuwa umekwisha.
Suarez alipewa Kadi Nyekundu kwa kitendo chake na Ghana ikapewa penalti ambayo Asamoah Gyan alikosa kufunga baada ya shuti lake kali kugonga mwamba.
Suarez amejigamba: “Ulikuwa ni mwisho wa Kombe la Dunia na ni lazima niokoe ili wenzangu washinde mikwaju ya penalti.”
Nae Kocha wa Uruguay Oscar Tabarez amemtetea Suarez kwa kudai kitendo cha Mchezaji huyo si udanganyifu bali ni kibinadamuy kuamua hivyo ghafla.
Barca wadai hawavunji Benki kwa Fabregas
Rais mpya wa Barcelona Sandro Rosell amesisitiza hawawezi kulipa pesa nyingi zisizostahili ili kumnunua Cesc Fabregas wa Arsenal.
Barca walishatoa ofa kwa Arsenal lakini imekataliwa na wachunguzi wanahisi Arsenal wanataka bei mbaya kwa Mchezaji huyo ambae mwenyewe ameonyesha nia ya kurudi Barca alikoanzia Soka akiwa mtoto.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Ghana 1 Uruguay 1
Ghana nje kwa penalti 4-2
Uruguay imetinga Nusu Fainali ya Kombe la Dunia na itacheza na Holland baada ya kuvunja mioyo ya Ghana na Afrika nzima waliposhinda mechi hii kwa penalti 4-2 baada ya kutoka sare 1-1 dakika 120.
Wachezaji John Mensah na Dominic Adiyiah ndio waliokosa penalti za Ghana.
Lakini nyota mbaya kwa ‘Nyota Nyeusi’ ilionekana pale Asamoah Gyan alipokosa kufunga penalti dakika ya 119 baada ya Luis Suarez kushika mpira kwenye mstari wa goli.
Refa Olegario Benquerenca toka Ureno akampa Kadi Nyekundu Suarez na ndipo Gyan akaachia bunduki toka kwenye penalti na mpira kugonga mwamba wa juu na kutoka nje.
Hilo lilikuwa pigo kubwa.
Awali Sulley Muntari aliipatia bao Ghana dakika ya 45 kwa shuti la Mita 35 na Diego Forlan wa Uruguay akasawazisha dakika ya 55 kwa frikiki.
Capello kubaki Kocha England
FA ya England imethibitisha kuwa Kocha Fabio Capello ataendelea kuwa Kocha wa England na hivyo kufuta ule wasiwasi kuwa atafutwa kazi baada ya England kutupwa nje ya Kombe la Dunia kwa kuchapwa 4-1 na Ujerumani.
Hatua hii inamaanisha Capello atashika hatamu hadi mwishoni mwa Fainali za EURO 2012 ambapo Mkataba wake ndio utakwisha.
Sunderland yamnasa Mmisri
Sunderland imemchukua kwa mkopo wa Mwaka mmoja Mchezaji wa Kimataifa wa Misri Ahmed Al-Muhammadi toka ENPPI.
Al-Muhammadi, Miaka 22, amechezea Misri mara 22 na ikiwa muda wake wa mkopo hapo Sunderland utakuwa wa mafanikio Mchezaji huyo atachukuliwa moja kwa moja.
Habari za kuchotwa Al-Muhammadi zimethibitishwa na Steve Bruce, Meneja wa Sunderland.
Huyu anakuwa Mchezaji wa tatu kuchukuliwa na Sunderland kwa ajili ya Msimu mpya wengine wakiwa ni Cristian Riveros na Simon Mignolet, Kipa kutoka Ubelgiji.

Friday 2 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Dunga abeba lawama zote
Kocha wa Brazil Dunga amebeba lawama zote kwa kutolewa na Uholanzi kwenye Robo Fainali ya Kombe la Dunia walipofungwa 2-1 na amedokeza ataondoka.
Dunga ametamka: “Bila ya doa lolote, mie ndio Kocha wa Brazil na ni jukumu kubwa!”
Dunga alitwaa uongozi wa Brazil toka kwa Carlos Alberto Parreira Mwaka 2006 na alishatamka tangu Mwaka jana kuwa baada ya Kombe la Dunia atang’atuka bila kujali matokeo.
Kuhusu mechi yenyewe, Dunga alitamka kifupi: “Inasikitisha, ni ngumu, hakuna Mtu anaejitayarisha kwa kipigo!”
ROBO FAINALI: Tathmini
Germany v Argentina
Uwanja: Green Point, Cape Town
Saa: 11 jioni [bongo]
Wengi walitegemea hii ingekuwa England v Argentina lakini ni Timu ya Vijana wa Ujerumani chini ya Kocha asie na makuu Joachim Low dhidi ya Diego Maradona wa Argentina mwenye kila aina ya sifa, mbovu na nzuri.
Hii ni mechi ambayo Masentahafu wa Ujerumani, Mertesacker na Friedrich, inabidi wawe makini na kufanya kazi ya ziada kuwazuia Lionel Messi, Carlos Tevez na Gonzalo Higuain.
Timu hizi zimecheza mara 18 kati yao na Argentina imeshinda mara 8, Germany mara 5 na sare mara 5.
Timu:
Argentina (Fomesheni 4-3-3): Romero; Otamendi, Demichelis, Burdisso, Heinze; Maxi, Mascherano, Di Maria; Tevez, Higuain, Messi
Akiba: Pozo, Rodriguez, Bolatti, Veron, Garce, Samuel, Aguero, Gutierrez, Milito, Palermo, Pastore, Andujar.
Germany (Fomesheni 4-4-1-1): Neuer; Lahm, Friedrich, Mertesacker, Boateng; Schweinsteiger, Khedira; Ozil, Podolski; Muller; Klose.
Akiba: Wiese, Butt, Aogo, Tasci, Badstuber, Jansen, Trochowski, Kroos, Marin, Kiesling, Gomez.
Refa: Ravshan Irmatov (Uzbekistan)
CHEKI: www.sokainbongo.com

Holland 2 Brazil 1
Brazil wametolewa nje ya Kombe la Dunia kwa kufungwa bao 2-1 na Holland katika mechi ya Robo Fainali ambayo Brazil walipata bao dakika ya 10 tu kupitia Robinho na kuitawala lakini bao 2 toka frikiki na kona yamewapa Uholanzi ushindi katika mechi ambayoWaholanzi  hawakutengeneza hata nafasi moja ya wazi hadi Brazil walipocheza Mtu 10 Felipe Melo alipopewa Kadi Nyekundu.
Uholanzi imetinga Nusu Fainali na Mshindi kati ya Uruguay na Ghana.
Bao la kwanza la Uholanzi lilikuwa la kujifunga wenyewe Felipe Melo alipogonga kwa kichwa mpira na kumchanganya Kipa Cesar.
Bao la pili alifunga Sneijder kwa kichwa kufuatia kona.
Mechi hii ilitawaliwa na uamuzi wenye utata wa Refa Yuichi Nishimura toka Japan akiwaacha Uholanzi wacheze rafu watakavyo na kudanganya waziwazi bila ya kuwapa Kadi na alievunja rekodi ni Van Bommel wa Uholanzi aliecheza kila aina ya rafu na triki na Refa Mjapan akiona ni sawa.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Man City yafungua Benki, yamchota Yaya Toure
Ndani ya wiki moja baada ya kumnasa David Villa kutoka Valencia, Manchester City imemchukua Yaya Toure kutoka FC Barcelona na sasa ataungana na Ndugu yake, Kolo Toure, ambae ni Nahodha wa Man City.
Meneja wa Man City Roberto Mancini amethibitisha habari hizi kwa kutamka: "Huu ni usajili mzuri kwetu kwani kila Mtu anajua Yaya ni Mchezaji mzuri aliecheza Barca kwa kiwango cha juu!”
Ada ya kumsajili Yaya Toure, Miaka 28, haikutajwa ingawa inavumishwa ni Pauni Milioni 28.
Man City tayari pia washamchukua Beki wa Ujerumani Jerome Boateng toka Hamburg na wapo mbioni kumsajili James Milner wa Aston Villa.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Ghana ni kitimtim!!
Jana Julai 1, Nchini Ghana ilikuwa ni mapumziko kusheherekea Siku yao ya Jamhuri lakini sherehe hizo huenda zikaendelea leo Nchini humo, na pengine Afrika yote, endapo Ghana wataifunga Uruguay na kutinga Nusu Fainali za Kombe la Dunia.
Wakipata mafanikio hayo, Ghana itakuwa Nchi ya kwanza kutoka Afrika kufika hatua hiyo.
Mechi hiyo inachezwa Uwanja wa Soccer City, Soweto, Jijini Johannesburg, Afrka Kusini lakini Ghana nzima inazizima kwa matarajio huku viroho vikidunda.
Jijini Accra, Mji Mkuu wa Ghana, Bigi Skrini zimeendelea kuwekwa sehemu mbalimbali ili Wananchi waweze kuona pambano hilo laivu.
Kwa sasa, zinafanywa ibada maalum ili kuiombea heri ‘Nyota Nyeusi’ kama Timu ya Ghana inavyojulikana.
Port Elizabeth yabanana!!
Uwanja wa Nelson Mandela, Port Elizabeth, Afrika Kusini umeshatumika kwa mechi 5 za Kombe la Dunia mpaka sasa na hakuna hata mechi moja kati ya hizo uliojaza Uwanja huo wenye kuchukua Watu 42,00 lakini leo wakati Brazil inacheza na Holland, hali ni tofauti kwani hamna hata upenyo wa kukaa.
Mbali ya Uwanja, katika kila Hoteli na Nyumba za Kupanga, utakutana na bango: ‘Vyumba Vimejaa.’
Benayoun njiani Stamford Bridge
Chelsea wanakaribia kumchota Kiungo wa Liverpool Yossi Benayoun kwa Mkataba wa Miaka minne na dau la Pauni Milioni 5.5.
Benayoun, Miaka 30, alijiunga na Liverpool Mwaka 2007 akitokea West Ham na ameichezea Liverpool mechi 91 na kufunga bao 18.
FIFA yaipa Nigeria Masaa 24
FIFA imeitaka Nigeria ifute uamuzi wake wa kujitoa kushiriki Mashindano ya Kimataifa kwa Miaka miwili la sivyo watasimamishwa uanachama FIFA.
Habari hizi zimethibitishwa na Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke.
Uamuzi wa kuitoa Nigeria kwenye Mashindano ya Kimataifa kwa Miaka miwili ulichukuliwa na Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan baada ya Timu hiyo kutolewa Raundi ya Kwanza ya Kombe la Dunia kwa kushika mkia kwenye Kundi lao.
Valcke ametamka: “Huwezi kuruhusu Serikali ziingilie Soka! Ufaransa tuliionya sasa kwa nini tushindwe kwa Nigeria? Tuna Wanachama 208 na tukiruhusu mmoja aanze kukiuka kanuni za Soka, mhimili wote wa Soka utaporomoka!”
Makocha Timu zilizotolewa Kombe la Dunia wazidi kutimka!!
Kocha wa Japan, Takeshi Okada, amejitoa toka Timu ya Japan baada ya Nchi hiyo kutolewa nje ya Kombe la Dunia na Paraguay kwenye mechi ya Raundi ya Pili ilipofungwa kwa penalti 5-3 baada ya mechi kuwa sare 0-0 kwa dakika 120.
Okada sasa amejiunga kwenye listi ya Makocha waliobwaga manyanga kufuatia kubwagwa nje ya Kombe la Dunia ambayo wapo Kocha wa Ugiriki, Otto Rehhagel, Javier Aguirre wa Mexico na Huh Jung-moo wa Korea ya Kusini.
Bila shaka, listi hii itaongezeka.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Hodgson ataka Gerrard na Torres wabaki Liverpool
Meneja mpya wa Liverpool Roy Hodgson ana nia ya kuwashawishi Mastaa wakubwa wa Liverpool hasa Nahodha Steven Gerrard na Fernando Torres wabaki Klabuni hapo licha ya kuwepo minong’ono mikubwa wapo njiani kuhama mara baada ya kuondoka Rafael Benitez kama Meneja.
Akiongea na Wanahabari kwa mara ya kwanza tangu athibitishwe kama Meneja mpya wa Liverpool, Roy Hodgson, alisema: “Hii ni Klabu kubwa yenye asili kubwa na kipaumbele kikubwa kwangu ni kuhakikisha Timu inafanya vizuri!”
Hodgson pia alisisitiza kuwa atajitahidi abakishe Wachezaji wote kwenye Timu wakiwemo Mastaa Gerrard na Torres.

Thursday 1 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

KOMBE LA DUNIA:
ROBO FAINALI: Tathmini
Holland v Brazil
Uwanja: Nelson Mandela Bay, Port Elizabeth
Saa: 11 jioni [bongo]
Timu hizi zimekutana mara 3 tu kwenye Kombe la Dunia na mechi zote hizo zilikuwa ni ‘Vita Takatifu’.
Mwaka 1974, huko Ujerumani, Holland iliifunga Brazil 2-0 kwenye Kundi lao na walifika Fainali ya Kombe la Dunia na kufungwa 2-1 na Ujerumani waliotwaa Ubingwa wa Dunia.
Mwaka 1994 huko USA, katika mechi ya Robo Fainali, Brazil waliinyuka Holland 3-2 na wakaendelea hadi Fainali na kuitoa Italia na kuwa Mabingwa wa Dunia.
Huko Ufaransa, Mwaka 1998, Brazil na Holland zilikutana Nusu Fainali na Brazil wakaibwaga Holland kwa matuta na kuingia Fainali waliyotolewa na Ufaransa.
Mpaka sasa Timu zote hazijaonyesha ile desturi yao, kwa Brazil kucheza Samba, yaani ‘Soka Tamu’, na Holland kucheza ule mpira uitwao ‘Soka Kamili’ ingawa kila Timu ni tishio kubwa.
Brazil itamkosa Ramires ambae amefungiwa mechi moja baada ya kuzikwaa jumla ya Kadi za Njano mbili na hivyo huenda wakamchezesha Dani Alves badala yake.
Pia Brazil watamkosa Kiungo Elano ambae ameumia enka.
Holland hawana wasiwasi wa kukosa Wachezaji na hata Staa wao Arjen Robben aliekuwa akisuasua kwa kuwa majeruhi sasa yuko fiti.
Makocha:
Dunga wa Brazil anataka kuifikia rekodi aliyoweka Franz Beckenbauer wa Ujerumani ya kunyakua Kombe la Dunia akiwa Mchezaji na pia Kocha.
Nae Kocha wa Uholanzi Bert Van Marwijk ni mzoefu, anaepanga vizuri mambo na ni mtulivu.
Sifa hizo ndizo bora kwa Uholanzi ambayo kihistoria hukumbwa na migogoro kwenye kila Timu zao hasa wakati wa Mashindano makubwa.
Mbinu:
Kila Kocha hupenda kutumia Viungo wawili wanaocheza Difensi, mbele ya Mabeki wanne, na kuachia Washambuliaji wanne wahangaike huku wakiongozwa na Mchezaji mmoja ambae ndie mchezeshaji.
Mchezeshaji kwa Brazil ni Kaka na Uholanzi ni Wesley Sneijder.
Nini wanasema:
Bert Van Marwijk: “Sisi ni Taifa dogo lakini ni wabunifu na kama anavyosema Johan Cruyff [Staa wa zamani Uholanzi] tuna ‘kiburi’ fulani kwenye Soka! Tutatumia kiburi hicho kitupe mafanikio!”
Dunga: “Holland wana staili ya uchezaji kama yetu. Wao ni kama Timu ya Marekani ya Kusini.”
Vikosi:
Holland (Fomesheni: 4-2-3-1): Stekelenburg; Van der Wiel, Heitinga, Mathijsen, Van Bronckhorst; Van Bommel, De Jong; Robben, Sneijder, Kuyt; Van Persie.
Brazil (Fomesheni: 4-2-3-1): Julio Cesar; Maicon, Lucio, Juan, Michel Bastos; Gilberto Silva, Melo; Dani Alves, Kaka, Robinho; Luis Fabiano
Refa: Yuichi Nishimura (Japan).
Uruguay v Ghana
Uwanja: Soccer City, Soweto, Johannesburg
Saa: 3.30 [bongo]
Uruguay ni Mabingwa wa Dunia mara mbili kwa kulichukua Kombe la Dunia Mwaka 1930 na 1950.
Ghana ni Nchi ya 3 toka Afrika kufikia hatua ya Robo Fainali nyingine zikiwa ni Cameroun Mwaka 1990 na Senegal 2002.
Lakini safari hii, kwa mara ya kwanza, Kombe linachezewa Afrika na Afrika yote inaomba Ghana ifanikiwe.
Uruguay wamefika hatua hii baada ya kutofungwa kwenye Kundi lao walipotoka sare na Ufaransa na kuzifunga Afrika Kusini na Mexico.
Raundi ya Pili wakaipiga Korea Kusini 2-1.
Ghana wamefika hapa walipoishinda Serbia 1-0, kutoka sare na Australia ya 1-1 na kufungwa na Germany 1-0.
Raundi ya Pili, Ghana wakaitupa nje USA 2-1 baada ya dakika 120 za Soka.
Uruguay itamkosa Diego Godin ambae ana maumivu lakini wengine wote wako fiti na mashambulizi yao yanategemewa kuongozwa na Diego Forlan, Suarez na Cavani.
Ghana walikuwa na wasiwasi na Asamoah Gyan alieumia pamoja Kevin-Prince Boateng lakini wote wanategemewa kuwa fiti.
Nae Kiungo wa Inter Milan Sulley Muntari anategemewa kuanza kwa vile Dede Ayew, Mwana wa Abedi Pele, amefungiwa mechi moja baada kupata Kadi za Njano mbili.
Ghana pia itamkosa Jonathan Mensah ambae amefungiwa kama Ayew.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Bifu la Pele v Maradona laendelea!!
Gwiji wa Brazil, Pele, ameendeleza vita ya maneno kati yake na Kocha wa sasa wa Argentina, Diego Maradona, na safari hii Pele amesema Maradona si Kocha mzuri kwa sababu ya staili yake ya maisha ni ya kutatanisha, kushangaza na mbovu.
Mwezi uliokwisha, Pele alikaririwa akisema Maradona alichukua kazi ya Ukocha wa Argentina kwa sababu tu ana shida ya pesa.
Na Maradona akajibu mapigo kwa kudai bora Pele arudi ‘Makumbusho’ kwa vile ni mtu wa kale.
Pele amesema: “Si Kocha mzuri kwa sababu maisha yake yana staili ya kutatanisha na hilo litaiathiri Timu!”
Argentina watakutana na Germany kwenye Robo Fainali ya Kombe la Dunia hapo Jumamosi huko Uwanja wa Green Park Mjini Cape Town.
Pele ameisifia Germany kwa kudai ni Timu ya Vijana yenye uwezo mzuri wa kuvuta mipira, kutoa pasi za uhakika na kushangaza dakika yeyote.
Refa wa Ligi Kuu akosa kuchezesha Robo Fainali Kombe la Dunia
Refa kutoka England, Howard Webb, hakupangiwa kuchezesha mechi yeyote kati ya mechi 4 za Robo Fainali za Kombe la Dunia.
Lakini Refa huyo bado amebakizwa huko Afrika Kusini na huenda akawa ndie Mwamuzi wa mechi ya Fainali endapo Timu mbili za Marekani Kusini ndizo zitakazocheza Fainali hiyo kwa sababu yupo Refa mmoja tu toka Ulaya, Olegario Benquerenca wa Ureno, atakaesimamia mechi ya Robo Fainali kati ya Uruguay na Ghana Siku ya Ijumaa.
Listi ya Marefa wa Robo Fainali:
-Holland v Brazil: Yuichi Nishimura [Japan]
-Uruguay v Ghana: Olegario Benquerenca [Ureno]
-Germany v Argentina: Ravshan Irmatov [Uzbekistan]
-Paraguay v Spain: Carlos Batres [Guatemala]
CHEKI: www.sokainbongo.com

Ronaldo aonywa
Kocha wa Ureno Carlos Queiroz amemuonya Cristiano Ronaldo kwamba itabidi ajitahidi la sivyo namba yake kwenye Timu ya Ureno ipo kwenye hatihati.
Mchezaji huyo wa bei mbaya Duniani alishindwa kuwika kwenye Kombe la Dunia na kufunga bao moja tu katika mechi 4 Ureno walizocheza na kutolewa nje na Spain walipofungwa 1-0.
Queiroz alikuwa na Ronaldo Manchester United kwa muda mrefu wakati alipokuwa Msaidizi wa Sir Alex Ferguson.
Queiroz ametamka: “Ureno inamuhitaji Ronaldo na Ronaldo anaihtaji Timu ya Taifa lakini ikiwa kuvaa jezi ya Taifa kunampa taabu basi hana sababu kuwa hapa!”
Wenger asema England imejiua yenyewe
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amedai England ilijimaliza yenyewe kwa kukosa utulivu na kuwa na papara katika mechi na Ujerumani waliyotandikwa 4-1 na kutupwa nje ya Kombe la Dunia.
Wenger amesema: “England walikuwa na papara. Walikuwa nyuma 2-1 na kweli walikuwa wanakontroli mpira. Kitu kilichonisikitisha ni kuwa wana Wachezaji wazoefu lakini walipatiwa! Toka frikiki yao golini mwa Ujerumani wanakwenda kufungwa wao bao la 3! Unafanya hivyo zikiwa zimebaki dakika 5 na si 25!”
Vilevile Wenger alihoji kwa nini England haikutumia silaha yao kubwa aliyoitaja kuwa ni kasi yao na kuuliza: “Je hiyo ilikuwa uchovu wa mwili au akili? Sijui lakini mpira wa England haukuonekana mechi ile!”
Hodgson kutua Liverpool
Liverpool huenda ndani ya Masaa 24 yajayo wakapata Meneja mpya baada ya kuondoka kwa Rafael Benitez endapo taratibu zote za kumhamisha Roy Hodgson toka Fulham zitakamilika.
Inasemekana inabidi Liverpool wailipe Fuham Pauni Milioni 2 ili Hodgson ang’oke kwenye Mkataba na Fulham.
Hadi sasa hamna tamko rasmi kutoka upande wowote mbali ya minong’ono kuwa majadiliano yapo hatua ya mbali na nyeti.
KOMBE LA DUNIA: ROBO FAINALI
Ijumaa Julai 2
Saa 11 jioni: Holland v Brazil
[Nelson Mandela Port Elizabeth]
Saa 3.30 usiku: Uruguay v Ghana
[Soccer City, Soweto, Johannesburg]
Jumamosi Julai 3
Saa 11 jioni: Argentina v Germany
[Green Point, Cape Town]
Saa 3.30 usiku: Paraguay v Spain
[Ellis Park, Johannesburg]

Wednesday 30 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Nigeria yajitia kibano wenyewe!!
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, ameamrisha Timu ya Taifa ya Nigeria isishiriki michuano ya Kimataifa kwa Miaka miwili kufuatia kutolewa kwenye Kombe la Dunia hatua ya mwanzo ya Makundi huku wakimaliza Kundi lao wakiwa mkiani baada ya kutoka sare na Korea Kusini na kufungwa na Argentina na Ugiriki.
Lakini hatua hiyo ya Serikali ya Nigeria bila shaka itawaletea matatizo makubwa na FIFA ambao hawataki Vyama vya Soka viingiliwe na Serikali na hivi juzi tu waliionya Serikali ya Ufaransa kuhusu hilo.
FIFA wametoa tamko kuhusu Nigeria kwa kusema: “Hatuna taarifa rasmi kuhusu hilo. Lakini, kwa ujumla, msimamo wa FIFA kuhusu kuingiliwa Soka na Wanasiasa unajulikana vizuri.”
CHEKI: www.sokainbongo.com

Brazil wakabiliwa na majeruhi
Ijumaa Brazil wanaivaa Timu ngumu Holland katika Robo Fainali ya Kombe la Dunia huko Uwanja wa Nelson Mandela, Port Elizabeth lakini wanakabiliwa na majeruhi kadhaa kwenye Kikosi chao na pia Mchezaji Ramires kufungiwa baada ya kupata Kadi za Njano mbili kwenye michuano hii na hivyo kulazimika kukosa mechi moja.
Wachezaji majeruhi ni Elano, Felipe Melo na Julio Baptista.
Elano aliumizwa na Cheik Tiote wa Ivory Coast baada ya kutimbwa vibaya kwenye enka.
Nae Felipe Melo pia ana tatizo la enka wakati Baptista ana tatizo la musuli.
WAFUNGAJI BORA KOMBE LA DUNIA:
-Higuain bao 4 [Argentina]
-Villa bao 4 [Spain]
-Vittek bao 4 [Slovakia]
-Donovan bao 3 [USA]
-Gyan bao 3 [Ghana]
CHEKI: www.sokainbongo.com

Silva kujiunga Man City
Kuna taarifa kuwa Davida Silva wa Valencia atajiunga Manchester City kwa dau la Pauni Milioni 30.
Silva, Miaka 24, anategemewa kusaini Mkataba wa Miaka minne na Man City.
Hivi sasa David Silva yuko Afrika Kusini akiwa na Kikosi cha Spain kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia.
Taratibu za kumsajili Silva zitakamilishwa mara baada ya Fainali za Kombe la Dunia.
Mchezaji mwingine ambae anategemewa kujiunga na Man City ni Yaya Toure anaetokea Barcelona.
Yaya Toure ataungana na ndugu yake Kolo Toure ambae ni Nahodha Man City.
Capello aungama: ‘Hamna vipaji Chipukizi England!’
Kocha wa England Fabio Capello ameungama na kudai hamna Wachezaji Chipukizi wanaojitokeza wenye uwezo wa kucheza England mechi za Kimataifa.
Mara baada ya kubwagwa nje ya Kombe la Dunia kwa kuwashwa bao 4-1 na Germany hapo juzi, sababu za nini kiliwasibu zimeaanza kutafutwa na hili la kutokuwa na Wachezaji Chipukizi limeanza kuchukua umuhimu ukizingatia Wachezaji wengi wa England ya sasa wanafikia tamati yao ya Uchezaji.
Katika kundi hilo la Wachezaji wanaokaribia kustaafu ni pamoja na Steven Gerrard, John Terry, David James na Frank Lampard ambao, bila shaka, hii ilikuwa Fainali yao ya mwisho ya Kombe la Dunia.
Bosi huyo wa England, Capello, kutoka Italia, amesema: “Wako wapi Wachezaji? Wazuri wapo Timu ya Vijana ya chini ya Miaka 21 lakini ni wawili au watatu wanaoweza kujiunga nasi Miezi 6 ijayo! Pia wapo wazuri kama Adam Johnson na Kieran Gibbs wa Arsenal. Pia wapo Michael Dawson, Gabby Agbonlahor na Bobby Zamora ingawa ni mkubwa lakini alikuwa majeruhi. Yupo Owen Hargreaves akiwa fiti ni mzuri!”

Tuesday 29 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Man United inamwania Kiungo wa Ugiriki
Manchester United wapo mstari wa mbele kumyakua Kiungo chipukizi wa Panathinaikos Sotiris Ninis na inaaminika ofa ya Pauni Milioni 9.6 itatolewa kwa ajili yake.
Ninis, Miaka 20, aling’ara kwenye Timu ya Ugiriki iliyotolewa Raundi ya Kwanza ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini.
Ninis anadaiwa pia kutakiwa na Klabu za Italia AS Roma, Inter Milan na AC Milan.
Hata hivyo, Man United bado haijathibitisha habari hizi.
FIFA yawaondoa Marefa ‘mabomu’
Inasemekana FIFA imewaondoa Marefa Jorge Larrionda kutoka Uruguay na Roberto Rosetti wa Italia toka kwenye listi ya Marefa watakaochezesha mechi za Robo Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa Ijumaa na Jumamosi hii inayokuja.
Marefa hao wawili wamekumbwa na mzozo na mjadala mkali Dunia nzima kufuatia kuboronga kwao katika mechi za Germany v England na Argentina v Mexico.
Wakati Larrionda alishindwa kuliona goli la Frank Lampard wa England liligonga posti juu na kutua mita moja ndani ya goli, Rosetti alikubali goli la kwanza la Argentina wakati Mfungaji Carlos Tevez akiwa ofsaidi ya wazi kabisa na mara baada ya kuzongwa na Wachezaji wa Mexico kulalamika TV kubwa hapo Uwanjani ilikuwa ikilirudia na ilikuwa wazi kabisa Tevez yuko ofasaidi.
Refa kutoka England Howard Webb na Wasaidizi wake, Darren Cannon na Michael Mullarkey, bado wapeta huko Afrika Kusini baada ya kuchezesha mechi kadhaa bila utata wala mzozo wowote.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Matuta yaifikisha Paraguay Robo Fainali!
Dakika 120 ngoma kati ya Paraguay na Japan ilikuwa 0-0 na ndipo ikaja tombola ya penalti na Paraguay wakaibwaga Japan kwa penalti 5-3.
Japan walikosa penalti moja baada ya shuti la Komano kugonga posti na penalti ya mwisho hawakuipiga kwani Paraguay alikuwa tayari Mshindi.
Kwenye Robo Fainali, Paraguay atacheza na Mshindi kati ya Spain na Ureno zinazocheza baadae leo.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Keane awaponda Wachezaji England
Roy Keane amewaponda Wachezaji wa England kwa kucheza vibaya hasa kwenye mechi na Germany waliyobamizwa 4-1 huko Afrika Kusini na kutupwa nja ya Kombe la Dunia hapo juzi.
Keane, aliekuwa Nahodha wa Manchester United na Mchezaji wa Kimataifa wa Ireland ambe sasa ni Meneja wa Ipswich Town, alimsifia Wayne Rooney pekee na kuwaponda wengine.
Keane alisema: “Tizama Makipa David James ameshushwa Daraja na Portsmouth na Robert Green alipona kushushwa na West Ham! Glen Johnson alicheza vizuri na Liverpool lakini Msimu wao ulikuwa mbovu! John Terry? Alikuwa na ishu nyingi na sidhani kama alikuwa na Msimu mzuri na Chelsea walichukua Ubingwa na FA Cup lakini si kwa sababu yake ni sababu ya Wachezaji wengine wazuri waliokuwa wakishambulia!”
Keane aliongeza: “Mathew Upson hakuwa na Msimu mzuri na West Ham. Ashley Cole ndio kwanza amerudi Uwanjani akitokea majeruhi! James Milner alicheza vizuri lakini Gareth Barry alikuwa wastani huko Man City! Emile Heskey amecheza na England lakini amefunga bao 3 tu akiwa na Aston Villa kwenye Ligi Kuu!”
Blatter aomba radhi kwa kukataliwa Mabao!
Rais wa FIFA, Sepp Blatter, ameomba radhi kwa matukio mawili kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambayo mabao mawili yalifungwa na moja likakataliwa na jingine kukubaliwa.
Bao safi la England, huku mabao yakiwa 2-1 katika mechi na Germany ambayo baadae England walifungwa 4-1, halikuonwa na Refa.
Katika mechi kati ya Argentina na Mexico, Carlos Tevez aliifungia Argentina bao la kwanza huku akiwa ofsaidi na Wachezaji wa Mexico walimzonga Refa na kumtaka aangalie marudio ya tukio hilo lililokuwa likionyeshwa kwenye Bigi Skrini hapo Uwanjani.
Blatter amesema watakutana na IFAB, International FA Board, ambayo ndiyo yenye majukumu ya kubadilisha sheria za Soka.
Blatter ametamka: “Ni wazi itakuwa upuuzi ikiwa matukio hayo kwenye Kombe la Dunia yataachwa bila kufungua mjadala wa kutumia teknoloji ya kisasa golini.”
Blatter amesema ameongea na Viongozi wa Soka toka England na Mexico na kuwaomba radhi.
FIFA imekuwa na msimamo wa kupinga matumizi ya kutumia teknlojia ya kisasa kusaidia Marefa katika maamuzi yao na kauli hii ya FIFA inaelekea kulainisha msimamo huo.
Barca yathibitisha kuwaacha Toure na Henry
FC Barcelona imethibitisha kuwa Wachezaji Thierry Henry na Yaya Toure wataondoka klabu hiyo.
Wakati Henry anasemekana ataelekea Marekani kucheza MLS [Major League Soccer], Yaya Toure yuko mbioni kujiunga na Manchester City, Timu ya ndugu yake Kolo Toure.
Hatua hiii ya kuhama Wachezaji hao imethibitishwa na tovuti ya Barca.
Wachezaji wote hao wawili hivi karibuni walikuwa Afrika Kusini wakichezea Nchi zao kwenye Kombe la Dunia, Henry akiwa na Ufaransa na Toure akiwa na Ivory Coast, na zote zilitolewa hatua ya kwanza ya Makundi.

Monday 28 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Brazil 3 Chile 0
Ni Brazil v Holland Robo Fainali!!
Brazil wamewatwanga wenzao wa Marekani ya Kusini Chile kwa bao 3-0 na hivyo kuingia Robo Fainali watakayocheza na Holland.
Ni mabao mawili ndani ya dakika 4, dakika ya 34 la Juan na dakika ya 38 la Luis Fabiano, ndio yaliyowalainisha Chile.
Kipindi cha Pili, Robinho alipachika bao la 3 dakika ya 59.
Ulikuwa ni ushindi laini kwa Brazil ambao wanaonyesha wao ni tishio kubwa kwenye Fainali hizi za Kombe la Dunia.
Timu:
Brazil: Julio Cesar, Maicon, Lucio, Juan, Michel Bastos, Ramires, Gilberto Silva, Dani Alves, Kaka, Robinho, Luis Fabiano.
Chile: Claudio Bravo, Mauricio Isla, Pablo Contreras, Ismael Fuentes, Arturo Vidal, Mark Gonzalez, Carlos Carmona, Gonzalo Jara, Humberto Suazo, Jean Beausejour, Alexis Sanchez.
Refa: Howard Webb (England)
CHEKI: www.sokainbongo.com

Holland kuivaa Brazil au Chile Robo Fainali
Holland leo wameifunga Slovakia bao 2-1 na Robo Fainali watacheza na Mshindi kati ya Brazil au Chile wanaocheza baadae leo.
Walikuwa ni Arjen Robben na Wesley Sneijder waliofunga mabao ya Holland na kuendeleza libeneke la Timu hiyo maarufu kwa jina la 'Chungwa' kufuatana na rangi zao.
Slovakia walipata bao lao dakika ya 90 kwa penalti iliyofungwa na Vittek baada ya Kipa wa Uholanzi Sketelenburg kumwangusha Jakubko.
Sketelenburg alitwangwa Kadi ya Njano kwa tukio hilo.
TATHMINI MECHI ZA Jumanne Juni 29
Spain v Portugal
Hii ni mechi yenye mvuto kwa wengi na ina ushindani wa jadi kwani Nchi hizi ni majirani.
Spain ndio Mabingwa wa Ulaya lakini kwenye Kombe la Dunia Miaka ya hivi karibuni Ureno ndio wenye rekodi nzuri walipomaliza nafasi ya 4 Mwaka 2006 huku Spain ikitolewa Raundi ya Pili tu.
Kwenye Kundi H, Spain walianza vibaya walipofungwa na Uswisi lakini wakaibuka na kuzitandika Honduras na Chile mechi zilizofuata na kuwa vinara wa Kundi hilo.
Ureno walimaliza wakiwa nafasi ya pili nyuma ya Brazil toka Kundi G wakitoka sare 0-0 na Brazil na Ivory Coast lakini waliinyuka Korea Kaskazini 7-0.
Ureno chini ya Carlos Queiroz ndio Timu pekee kwenye Fainali hizi za Kombe la Dunia bado haijafungwa hata goli moja.
Wakati Mastaa wa Timu zote mbili, Fernando Torres na Cristiano Ronaldo, hawajaonyesha cheche zozote huku Torres akiwa hana hata bao moja baada ya mechi 3, wamebaki Wachezaji wengine kama David Villa wa Spain, ndio wanabeba Timu zao.
Timu zote huenda zikawakosa Wachezaji muhimu kwa Spain kumkosa Alonso na Ureno kumpoteza Danny kwa kuwa na maumivu.
Paraguay v Japan
Japan wanaingia mechi hii kwa kuzifunga Timu ngumu Denmark na Cameroun toka Kundi lao na hivyo ndio wanaoonekana kama ni bora lakini Paraguay wanacheza staili tofauti ya kutumia nguvu na kucheza kitimu na mpaka sasa wamefungwa bao moja tu kwenye mechi ya sare ya 1-1 na waliokuwa Mabingwa wa Dunia Italia.
Chini ya Kocha Gerardo Martino na jopo la Wachezaji mahiri kama Roque Santa Cruz, Lucas Barrios, Nelson Valdez na Oscar Cardozo, Paraguay si mzaha.
Nao Japan, chini ya Kocha Takeshi Okada, wana Timu inayojituma kwa nguvu kazi ya pamoja ya Wachezaji kama Keisuke Honda, Yasuhito Endo na ‘Mbrazil’ Tulio Tanaka.
Hii ni mechi ngumu kuitabiri.
PITIA: www.sokainbongo.com

Wiki mbili Capello kujua hatma yake England!!
Kocha wa England Fabio Capello ametamka hatajiuzulu kufuatia kutolewa nje ya Kombe la Dunia kwa kipigo kitakatifu cha bao 4-1 toka kwa Germany hapo jana na pia ana nia kubwa ya kuendelea na kazi hiyo lakini amekiri kuwa itamchukua Wiki mbili kujua kama ataendelea kuwepo kwa vile FA bado inatafakari nini kifanywe.
Capello anao Mkataba na FA ambao utamalizika Mwaka 2012 mara tu baada ya Fainali za EURO 2012, michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya.
Msemaji wa FA amesema hawawezi kutoa uamuzi mara tu baada ya kubwagwa nje ya Kombe la Dunia kwani hilo linaweza kuathiri kutoa uamuzi sahihi na badala yake kutoa uamuzi kwa jazba.
Mwenyewe Capello amesema: “Bado naitaka kazi hii ya England na ndio maana nimekataa kuwa Meneja wa Klabu kubwa kadhaa zinazonitaka.”
Capello aligusia sababu za England kuwa goigoi kwenye Kombe la Dunia na kudai sababu kubwa ni uchovu wa Wachezaji uliosababishwa na kutokuwa na mapumziko majira ya baridi [Desemba na Januari] kama wanavyofanya Nchi nyingine [ikiwemo Ujerumani] ambao Misimu yao huanza Agosti hadi mwishoni mwa Desemba na kupumzika na kisha kuanza tena mwishoni mwa Januari hadi Mei.
England Msimu huanza Agosti hadi Mei mfululizo bila mapumziko.
CHEKI: www.sokainbongo.com

FIFA bubu na Teknolojia!!
FIFA imekataa kuongea lolote kuhusu makosa makubwa ya Marefa kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini huku Wadau wakibeba mabango makubwa wakitaka teknolojia ya kisasa itumike kusaidia Marefa hasa kwenye uamuzi wa mpira umevuka mstari wa goli au la.
Mechi za Jumapili Juni 27 ndizo zimeleta mjadala mkubwa kuhusu kutumika kwa teknolojia kwenye mechi baada ya England kunyimwa bao la wazi la kusawazisha wakati mechi ikiwa 2-1 wakati mpira uko ndani ‘maili moja’ nzima na hatimaye wakatandikwa 4-1 na Ujerumani.
Nao Mexico walifungwa bao la kwanza kwenye kipigo cha 3-1 toka kwa Argentina wakati kila Mtu alimwona Mfungaji Carlos Tevez yuko ‘maili moja’ ofsaidi.
Katika kikao cha kawaida cha kila siku cha FIFA na Wanahabari kinachofanyika huko Afrika Kusini huku Kombe la Dunia likiendelea, Msemaji wa FIFA Nicolas Maingot alikataa kujibu lolote kuhusu makosa ya Marefa kwa kudai si wakati muafaka kuongelea hilo wala ubora wa kutumia teknolojia ya kisasa kusaidia Marefa.
Rais wa FIFA Sepp Blatter amekuwa mpinzani mkubwa wa teknolojia kusaidia Marefa.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Argentina nayo….goli la utata!!
Argentina imeifunga Mexico 3-1 na itacheza na Ujerumani Robo Fainali lakini, kama Ujerumani walioifunga England 4-1 na kugubikwa na mzozo wa goli la wazi la England kukataliwa, Argentina nao bao lao la kwanza la dakika ya 26 alilofunga Carlos Tevez lilileta malamiko makubwa toka kwa Wachezaji wa Mexico wakidai Tevez alikuwa ofsaidi kitu ambacho kilikuwa wazi na walimzonga Refa Roberto Rosetti toka Italia wakimtaka aangalie Bigi Skrini ya hapo Uwanjani iliyokuwa ikionyesha marudio ya tukio hilo.
Hata hivyo Refa huyo hakuangalia TV hiyo kwani sheria hazimruhusu.
Mabao mengine ya Argentina yalifungwa na Higuain dakika ya 33 na Tevez tena dakika ya 52.
Bao la Mexico alifunga Mchezaji anaeenda Manchester United, Javier Hernandez ‘Chicharito’ dakika ya 71.

Sunday 27 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Luis Fabiano: ‘Man United inavutia!’
-Atangaza kutosaini tena Sevilla!
Straika wa Brazil, Luis Fabiano, Miaka 29, anaecheza Sevilla huko Spain, amedokeza kuwa mara baada ya Kombe la Dunia atahama Klabu hiyo na kusema Manchester United inavutia kwake kwa sababu Kocha wao ni Mshindi na Wachezaji ni Washindi.
Huko Afrika Kusini, Fabiano alipachika bao mbili kwa Brazil kwenye mechi na Ivory Coast waliyoshinda 3-1. 
Fabiano ametamka: “Nishaweka msimamo wangu, siwezi kusaini Sevilla kwani kwa umri wangu lazima nicheze Timu inayowania Mataji makubwa kila wakati. Siwezi kujiunga Tottenham ni afadhali nibaki Sevilla. Uamuzi wangu utakuwa ni Milan au Man United ingawa kucheza pamoja na Rooney ni jambo la kuvutia.”
Luis Fabiano aliongeza kwa kusema Manchester United inamvutia mno kwa vile Msimu baada ya Msimu huwa wanagombea Mataji England na Ulaya na hushinda mara nyingi.
Hivyo, mara baada ya Fainali za Kombe la Dunia atatoa uamuzi wapi atatua.
CHEKI: www.sokainbongo.com

WAHENGA WALISEMA: "Majuto ni Mjukuu.........."
“Ilikuwa muhimu sisi kupata bao la pili. Sielewi kwanini wakati huu tuna teknolojia ya hali ya juu, tunazungumzia hili. Tulicheza vizuri tulipokuwa 2-1 nyuma lakini tulistahili kuwa 2-2 lakini Germany ni timu kubwa na walicheza vizuri na sisi tulifanya makosa lakini Refa ndie aliefanya kosa kubwa! Hii ni Soka!”
Maneno ya Kocha wa England Fabio Capello mara ya baada ya kubwagwa nje ya Kombe la Dunia kwa kichapo cha 4-1 na Germany huku akijutia Refa Jorge Larrionda wa Uruguay kutoliona bao la England lililovuka mstari wa goli ‘maili moja’ ndani.
CHEKI: www.sokainbongo.com

England yashindiliwa!!
Germany 4 England 1
England imetupwa nje ya Kombe la Dunia walipotandikwa vibaya na Mahasimu wao wakubwa Germany kwa kushindiliwa bao 4-1 kwenye mechi ya Raundi ya Pili iliyochezwa Free State, Bloemfontein.
Ingawa England ilishindwa vibaya sana lakini mechi hii itakumbukwa kwa Miaka mingi ijayo kwa tukio moja wakati Germany wakiwa mbele kwa bao 2-1 shuti la Frank Lampard kugonga mwamba wa juu, kumpita Kipa Neuer wa Germany na kutua Mita moja ndani ya goli lakini kwa mshangao wa Dunia nzima Refa Jorge Larrionda wa Uruguay ghafla kugeuka kipofu kwa kutokukubali hilo ni goli na kuwaacha Wachezaji wa England wakishika vichwa kwa mfadhaiko na majonzi.
Pengine hiki ni 'kisasi' cha lile goli la Fainali za Kombe la Dunia kati ya England na Germany Mwaka 1966 huko Wembley wakati mechi iko 2-2 Geoff Hurst wa England alipopiga shuti lililogonga posti juu na kudunda chini na kuleta utata kama lilivuka mstari au la lakini Refa kutoka Urusi akasema weka kati na England wakaongeza bao moja na kuwa Mabingwa wa Dunia kwa kuipiga Ujerumani 4-2.   
Mechi hii ilionyesha waziwazi udhaifu mkubwa wa ngome na midifildi ya England kwa jinsi mabao ya Ujerumani yalivyofungwa.
Bao la kwanza la Germany lilianza kwa Kipa Neuer kupiga mpira ndefu wa juu mbele na kumkuta Straika Miroslav Klose akimwacha Beki Matthew Upson na kufunga dakika ya 20.
Mara nyingi goli aina hii unaliona kwa Timu za mchangani.
Mabao mengine matatu ya Germany, lile la Lukas Podolski, dakika ya 32 na mawili ya Thomas Muller, yote ni ya mtindo wa kaunta ataki ulioiacha kiungo na difensi ya England imepotezana na kukatika vibaya.
Germany Robo Fainali atacheza na Mshindi kati ya Argentina na Mexico.
Timu:
GERMANY: Neuer, Lahm, Friedrich, Mertesacker, Boateng, Schweinsteiger, Khedira, Muller, Ozil, Podolski, Klose.
Akiba: Wiese, Jansen, Aogo, Tasci, Kiessling, Badstuber, Trochowski, Cacau, Kroos, Marin, Gomez, Butt.
ENGLAND: James, Johnson, Terry, Upson, Ashley Cole, Milner, Lampard, Barry, Gerrard, Defoe, Rooney.
Akiba: Green, Dawson, Lennon, Crouch, Joe Cole, Warnock, Wright-Phillips, Carragher, Heskey, King, Carrick, Hart.
Refa: Jorge Larrionda (Uruguay)
MECHI ZA JUMATATU Juni 28:
Holland v Slovakia
Holland wataikwaa Slovakia Uwanja wa Moses Mabhida, Durban ili kuwania kuingia Robo Fainali.
Holland mpaka sasa wameshinda mechi zao zote walipozifunga Denmark, Japan na Cameroun kwenye Kundi E.
Wengine ni Argentina pekee ndio imeshinda mechi zote 3 za Kombe la Dunia.
Mshindi kati ya Holland v Slovakia atakutana na Mshindi kati ya Brazil v Chile Robo Fainali Jumamosi ijayo.
Lakini Slovakia, chini ya Kocha Vladimir Weiss, si vibonde baada ya kuwatoa nishai vigogo Italia kwa kuwafunga 3-2 na kuwatupa nje ya Kombe la Dunia.
Holland hawajahi kushinda Kombe la Dunia lakini wamekuwa Washindi wa Pili mara mbili hapo Mwaka 1974 na 1978.
Mwaka 2006 Holland walitolewa Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia na Ureno.
Safari hii, matumaini ya Holland yapo mikononi mwa Mastaa wao Robin van Persie na Arjen Robben ambae amekuwa majeruhi.
Hili ni Kombe la Dunia la kwanza kwa Slovakia na wanawategemea zaidi Wachezaji wao Juraj Kucka, Erik Jendrisek na Miroslav Stoch.
Brazil v Chile
Brazil, Mabingwa wa Dunia mara 5, wanakutana na Chile ambao ni wenzao toka Marekani ya Kusini na Mshindi atacheza na Mshindi wa Holland v Slovakia Robo Fainali.
Brazil bado hawajafungwa kwenye Fainali hizi na wameipiga Korea Kaskazini 2-1, Ivory Coast 3-1 na kutoka sare na Ureno 0-0.
Katika mechi zao za Mchujo huko Marekani ya Kusini ili kupata Timu za kuingia Fainali hizi za Kombe la Dunia, Brazil iliichapa Chile mechi zote mbili kwa bao 3-0 huko Nchini Chile na marudio ni 4-2 huko Brazil.
Lakini huko Afrika Kusini, Chile, chini ya Kocha Marcelo Bielsa, ipo imara na imeshinda mechi mbili kwa kuzifunga Honduras na Uswisi na kupoteza 2-1 na Spain.
Kwenye mechi hii, Marco Estrada wa Chile hatacheza baada ya kupewa Kadi Nyekundu kwenye mechi na Spain.
Brazil watamkaribisha tena Supastaa Kaka aliefungiwa mechi ya mwisho na Ureno baada ya kupewa Kadi Nyekundu ya uonevu Brazil walipocheza na Ivory Coast.
Pia Mchezaji wa zamani wa Manchester City, Elano, alieumizwa kwenye mechi ya Brazil v Ivory Coast amepona na atarudi Uwanjani kuimarisha Kiungo cha Brazil.

TEMBELEA: www.sokainbongo.com

Gyan azawadia ushindi wa Ghana kwa Africa
Asamoah Gyan ametoa zawadi bao lake la ushindi la Ghana ilipoifunga USA 2-1 kwenye dakika 120 za mechi ya Raundi ya Pili jana Jumamosi huko Royal Bafokeng, Rustenburg na kutinga Robo Fainali ambako watacheza na Uruguay Ijumaa Julai 2.
Hii ni mara ya kwanza kwa Ghana kufika Robo Fainali ya Kombe la Dunia na imekuwa Nchi ya 3 ya Afrika kufika hatua hiyo baada ya Cameroun Mwaka 1990 na Senegal 2002.
Asamoah Gyan, ambae bao lake la dakika ya 93 ndio liliibua mayowe kila kona ya Afrika, ametamka: “Mwaka 2006 tulifika Raundi ya Pili na safari hii tupo Robo Fainali. Hii ni fahari kwa Ghana na Afrika yote!”
Hili ni bao la 3 la Gyan kwenye Kombe la Dunia na limemfanya afungane na Suarez wa Uruguay kama Wafungaji Bora mpaka sasa.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Ghana yajikita Robo Fainali!!
Ghana 2 USA 1
Dakika 120 ziliwaibua Ghana kidedea baada ya Asamoah Gyan kupachika bao la ushindi mara tu baada ya dakika 30 za nyongeza kuanza na kuifanya Afrika nzima ishangilie Ghana kuingia Robo Fainali ya Kombe la Dunia.
Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Royal Bafokeng huko Rustenburg.
Hadi dakika 90, bao zilikuwa 1-1 na ndipo zikaongezwa dakika 30.
Ghana ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 5 Mfungaji akiwa Kevin-Prince Boateng.
Lakini USA walisawazisha Kipindi cha Pili kwa penalti iliyopigwa na Landon Donovan.
Penalti hiyo ilipatikana baada ya Difenda Jonathan Mensah kumwangusha Clint Dempsey ndani ya boksi.
Robo Fainali Ghana watacheza na Uruguay siku ya Ijumaa Julai 2.
Powered By Blogger