Saturday 3 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Suarez kukiona cha moto na FIFA kwa ‘Ujangili’!
FIFA imetamka kuwa licha ya Luis Suarez wa Uruguay kutumikia adhabu ya kutocheza mechi moja baada ya kupewa Kadi Nyekundu aliposhika kwa makusudi kwenye mstari wa goli kuwazuia Ghana wasipate bao la ushindi na hatimaye Timu yake kuitoa Ghana kwa mikwaju ya penalti, huenda akafungiwa mechi zaidi baada ya kukaa kwa Kamati ya Nidhamu ya FIFA.
Suarez ataikosa mechi ya Nusu Fainali dhidi ya Holland na huenda pia akaikosa Fainali ikiwa Uruguay itafuzu au mechi ya Mshindi wa Tatu ikiwa watafungwa na Holland.
Huko kwao Suarez ni shujaa lakini kwa FIFA, chini ya Kampeni ya ‘Uchezaji wa Haki’ [Fair Play], ni jangili kwani ‘Uchezaji wa Haki’ tamko lake ni: “Ushindi hauna thamani ikiwa ushindi huo umepatikana kwa njia siyo ya haki au kwa udanganyifu. Kudanganya ni rahisi lakini hakuleti furaha.”
Gyan apozwa na Mandela
Staa wa Ghana, Asamoah Gyan, ambae alikosa penalti ya dakika ya 119 ambayo ingewapa ushindi wa bao 2-1 na hatimaye wakatolewa kwa mikwaju ya penalti na Uruguay, ametumiwa ujumbe wa kumpa pole na kumtuliza kutoka kwa Nelson Mandela.
Kabla ya mechi hiyo na Uruguay, Mandela alituma barua ya kuwaunga mkono Ghana na kuwatakia heri.
Nae Kocha wa Ghana, Milovan Rajevac, alizungumza: “Ule ni ukatili. Lakini ndio Soka. Utamwambia nini Gyan? Tulikuwa karibu mno kuweka historia lakini haikutokea. Kulikuwa na wakati ilijionyesha kama vile kuna mkono wa Mtu anaekontroli ile gemu!”

No comments:

Powered By Blogger