Saturday 3 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Suarez adai ni ‘Mkono wa Mungu!’
Luis Suarez wa Uruguay amesema hatua yake ya kushika mpira kwenye mstari wa goli ili kuokoa kichwa cha Dominic Adiyiah dakika ya 119 ulikuwa ni ‘Mkono wa Mungu’ kwa vile Uruguay imefanikiwa kuingia Nusu Fainali baada ya kushinda mikwaju ya penalti 4-2 dhidi ya Ghana.
Laiti kama Suarez, anaecheza Ajax huko Uholanzi, asingeshika hilo lingekuwa bao la pili na la ushindi kwani muda ulikuwa umekwisha.
Suarez alipewa Kadi Nyekundu kwa kitendo chake na Ghana ikapewa penalti ambayo Asamoah Gyan alikosa kufunga baada ya shuti lake kali kugonga mwamba.
Suarez amejigamba: “Ulikuwa ni mwisho wa Kombe la Dunia na ni lazima niokoe ili wenzangu washinde mikwaju ya penalti.”
Nae Kocha wa Uruguay Oscar Tabarez amemtetea Suarez kwa kudai kitendo cha Mchezaji huyo si udanganyifu bali ni kibinadamuy kuamua hivyo ghafla.
Barca wadai hawavunji Benki kwa Fabregas
Rais mpya wa Barcelona Sandro Rosell amesisitiza hawawezi kulipa pesa nyingi zisizostahili ili kumnunua Cesc Fabregas wa Arsenal.
Barca walishatoa ofa kwa Arsenal lakini imekataliwa na wachunguzi wanahisi Arsenal wanataka bei mbaya kwa Mchezaji huyo ambae mwenyewe ameonyesha nia ya kurudi Barca alikoanzia Soka akiwa mtoto.

No comments:

Powered By Blogger