Thursday, 1 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Bifu la Pele v Maradona laendelea!!
Gwiji wa Brazil, Pele, ameendeleza vita ya maneno kati yake na Kocha wa sasa wa Argentina, Diego Maradona, na safari hii Pele amesema Maradona si Kocha mzuri kwa sababu ya staili yake ya maisha ni ya kutatanisha, kushangaza na mbovu.
Mwezi uliokwisha, Pele alikaririwa akisema Maradona alichukua kazi ya Ukocha wa Argentina kwa sababu tu ana shida ya pesa.
Na Maradona akajibu mapigo kwa kudai bora Pele arudi ‘Makumbusho’ kwa vile ni mtu wa kale.
Pele amesema: “Si Kocha mzuri kwa sababu maisha yake yana staili ya kutatanisha na hilo litaiathiri Timu!”
Argentina watakutana na Germany kwenye Robo Fainali ya Kombe la Dunia hapo Jumamosi huko Uwanja wa Green Park Mjini Cape Town.
Pele ameisifia Germany kwa kudai ni Timu ya Vijana yenye uwezo mzuri wa kuvuta mipira, kutoa pasi za uhakika na kushangaza dakika yeyote.
Refa wa Ligi Kuu akosa kuchezesha Robo Fainali Kombe la Dunia
Refa kutoka England, Howard Webb, hakupangiwa kuchezesha mechi yeyote kati ya mechi 4 za Robo Fainali za Kombe la Dunia.
Lakini Refa huyo bado amebakizwa huko Afrika Kusini na huenda akawa ndie Mwamuzi wa mechi ya Fainali endapo Timu mbili za Marekani Kusini ndizo zitakazocheza Fainali hiyo kwa sababu yupo Refa mmoja tu toka Ulaya, Olegario Benquerenca wa Ureno, atakaesimamia mechi ya Robo Fainali kati ya Uruguay na Ghana Siku ya Ijumaa.
Listi ya Marefa wa Robo Fainali:
-Holland v Brazil: Yuichi Nishimura [Japan]
-Uruguay v Ghana: Olegario Benquerenca [Ureno]
-Germany v Argentina: Ravshan Irmatov [Uzbekistan]
-Paraguay v Spain: Carlos Batres [Guatemala]

No comments:

Powered By Blogger