Wednesday 30 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Silva kujiunga Man City
Kuna taarifa kuwa Davida Silva wa Valencia atajiunga Manchester City kwa dau la Pauni Milioni 30.
Silva, Miaka 24, anategemewa kusaini Mkataba wa Miaka minne na Man City.
Hivi sasa David Silva yuko Afrika Kusini akiwa na Kikosi cha Spain kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia.
Taratibu za kumsajili Silva zitakamilishwa mara baada ya Fainali za Kombe la Dunia.
Mchezaji mwingine ambae anategemewa kujiunga na Man City ni Yaya Toure anaetokea Barcelona.
Yaya Toure ataungana na ndugu yake Kolo Toure ambae ni Nahodha Man City.
Capello aungama: ‘Hamna vipaji Chipukizi England!’
Kocha wa England Fabio Capello ameungama na kudai hamna Wachezaji Chipukizi wanaojitokeza wenye uwezo wa kucheza England mechi za Kimataifa.
Mara baada ya kubwagwa nje ya Kombe la Dunia kwa kuwashwa bao 4-1 na Germany hapo juzi, sababu za nini kiliwasibu zimeaanza kutafutwa na hili la kutokuwa na Wachezaji Chipukizi limeanza kuchukua umuhimu ukizingatia Wachezaji wengi wa England ya sasa wanafikia tamati yao ya Uchezaji.
Katika kundi hilo la Wachezaji wanaokaribia kustaafu ni pamoja na Steven Gerrard, John Terry, David James na Frank Lampard ambao, bila shaka, hii ilikuwa Fainali yao ya mwisho ya Kombe la Dunia.
Bosi huyo wa England, Capello, kutoka Italia, amesema: “Wako wapi Wachezaji? Wazuri wapo Timu ya Vijana ya chini ya Miaka 21 lakini ni wawili au watatu wanaoweza kujiunga nasi Miezi 6 ijayo! Pia wapo wazuri kama Adam Johnson na Kieran Gibbs wa Arsenal. Pia wapo Michael Dawson, Gabby Agbonlahor na Bobby Zamora ingawa ni mkubwa lakini alikuwa majeruhi. Yupo Owen Hargreaves akiwa fiti ni mzuri!”

No comments:

Powered By Blogger