Tuesday, 29 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Man United inamwania Kiungo wa Ugiriki
Manchester United wapo mstari wa mbele kumyakua Kiungo chipukizi wa Panathinaikos Sotiris Ninis na inaaminika ofa ya Pauni Milioni 9.6 itatolewa kwa ajili yake.
Ninis, Miaka 20, aling’ara kwenye Timu ya Ugiriki iliyotolewa Raundi ya Kwanza ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini.
Ninis anadaiwa pia kutakiwa na Klabu za Italia AS Roma, Inter Milan na AC Milan.
Hata hivyo, Man United bado haijathibitisha habari hizi.
FIFA yawaondoa Marefa ‘mabomu’
Inasemekana FIFA imewaondoa Marefa Jorge Larrionda kutoka Uruguay na Roberto Rosetti wa Italia toka kwenye listi ya Marefa watakaochezesha mechi za Robo Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa Ijumaa na Jumamosi hii inayokuja.
Marefa hao wawili wamekumbwa na mzozo na mjadala mkali Dunia nzima kufuatia kuboronga kwao katika mechi za Germany v England na Argentina v Mexico.
Wakati Larrionda alishindwa kuliona goli la Frank Lampard wa England liligonga posti juu na kutua mita moja ndani ya goli, Rosetti alikubali goli la kwanza la Argentina wakati Mfungaji Carlos Tevez akiwa ofsaidi ya wazi kabisa na mara baada ya kuzongwa na Wachezaji wa Mexico kulalamika TV kubwa hapo Uwanjani ilikuwa ikilirudia na ilikuwa wazi kabisa Tevez yuko ofasaidi.
Refa kutoka England Howard Webb na Wasaidizi wake, Darren Cannon na Michael Mullarkey, bado wapeta huko Afrika Kusini baada ya kuchezesha mechi kadhaa bila utata wala mzozo wowote.

No comments:

Powered By Blogger