Thursday 1 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Ronaldo aonywa
Kocha wa Ureno Carlos Queiroz amemuonya Cristiano Ronaldo kwamba itabidi ajitahidi la sivyo namba yake kwenye Timu ya Ureno ipo kwenye hatihati.
Mchezaji huyo wa bei mbaya Duniani alishindwa kuwika kwenye Kombe la Dunia na kufunga bao moja tu katika mechi 4 Ureno walizocheza na kutolewa nje na Spain walipofungwa 1-0.
Queiroz alikuwa na Ronaldo Manchester United kwa muda mrefu wakati alipokuwa Msaidizi wa Sir Alex Ferguson.
Queiroz ametamka: “Ureno inamuhitaji Ronaldo na Ronaldo anaihtaji Timu ya Taifa lakini ikiwa kuvaa jezi ya Taifa kunampa taabu basi hana sababu kuwa hapa!”
Wenger asema England imejiua yenyewe
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amedai England ilijimaliza yenyewe kwa kukosa utulivu na kuwa na papara katika mechi na Ujerumani waliyotandikwa 4-1 na kutupwa nje ya Kombe la Dunia.
Wenger amesema: “England walikuwa na papara. Walikuwa nyuma 2-1 na kweli walikuwa wanakontroli mpira. Kitu kilichonisikitisha ni kuwa wana Wachezaji wazoefu lakini walipatiwa! Toka frikiki yao golini mwa Ujerumani wanakwenda kufungwa wao bao la 3! Unafanya hivyo zikiwa zimebaki dakika 5 na si 25!”
Vilevile Wenger alihoji kwa nini England haikutumia silaha yao kubwa aliyoitaja kuwa ni kasi yao na kuuliza: “Je hiyo ilikuwa uchovu wa mwili au akili? Sijui lakini mpira wa England haukuonekana mechi ile!”
Hodgson kutua Liverpool
Liverpool huenda ndani ya Masaa 24 yajayo wakapata Meneja mpya baada ya kuondoka kwa Rafael Benitez endapo taratibu zote za kumhamisha Roy Hodgson toka Fulham zitakamilika.
Inasemekana inabidi Liverpool wailipe Fuham Pauni Milioni 2 ili Hodgson ang’oke kwenye Mkataba na Fulham.
Hadi sasa hamna tamko rasmi kutoka upande wowote mbali ya minong’ono kuwa majadiliano yapo hatua ya mbali na nyeti.
KOMBE LA DUNIA: ROBO FAINALI
Ijumaa Julai 2
Saa 11 jioni: Holland v Brazil
[Nelson Mandela Port Elizabeth]
Saa 3.30 usiku: Uruguay v Ghana
[Soccer City, Soweto, Johannesburg]
Jumamosi Julai 3
Saa 11 jioni: Argentina v Germany
[Green Point, Cape Town]
Saa 3.30 usiku: Paraguay v Spain
[Ellis Park, Johannesburg]

No comments:

Powered By Blogger