Friday 2 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Dunga abeba lawama zote
Kocha wa Brazil Dunga amebeba lawama zote kwa kutolewa na Uholanzi kwenye Robo Fainali ya Kombe la Dunia walipofungwa 2-1 na amedokeza ataondoka.
Dunga ametamka: “Bila ya doa lolote, mie ndio Kocha wa Brazil na ni jukumu kubwa!”
Dunga alitwaa uongozi wa Brazil toka kwa Carlos Alberto Parreira Mwaka 2006 na alishatamka tangu Mwaka jana kuwa baada ya Kombe la Dunia atang’atuka bila kujali matokeo.
Kuhusu mechi yenyewe, Dunga alitamka kifupi: “Inasikitisha, ni ngumu, hakuna Mtu anaejitayarisha kwa kipigo!”
ROBO FAINALI: Tathmini
Germany v Argentina
Uwanja: Green Point, Cape Town
Saa: 11 jioni [bongo]
Wengi walitegemea hii ingekuwa England v Argentina lakini ni Timu ya Vijana wa Ujerumani chini ya Kocha asie na makuu Joachim Low dhidi ya Diego Maradona wa Argentina mwenye kila aina ya sifa, mbovu na nzuri.
Hii ni mechi ambayo Masentahafu wa Ujerumani, Mertesacker na Friedrich, inabidi wawe makini na kufanya kazi ya ziada kuwazuia Lionel Messi, Carlos Tevez na Gonzalo Higuain.
Timu hizi zimecheza mara 18 kati yao na Argentina imeshinda mara 8, Germany mara 5 na sare mara 5.
Timu:
Argentina (Fomesheni 4-3-3): Romero; Otamendi, Demichelis, Burdisso, Heinze; Maxi, Mascherano, Di Maria; Tevez, Higuain, Messi
Akiba: Pozo, Rodriguez, Bolatti, Veron, Garce, Samuel, Aguero, Gutierrez, Milito, Palermo, Pastore, Andujar.
Germany (Fomesheni 4-4-1-1): Neuer; Lahm, Friedrich, Mertesacker, Boateng; Schweinsteiger, Khedira; Ozil, Podolski; Muller; Klose.
Akiba: Wiese, Butt, Aogo, Tasci, Badstuber, Jansen, Trochowski, Kroos, Marin, Kiesling, Gomez.
Refa: Ravshan Irmatov (Uzbekistan)

No comments:

Powered By Blogger