Monday 28 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

FIFA bubu na Teknolojia!!
FIFA imekataa kuongea lolote kuhusu makosa makubwa ya Marefa kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini huku Wadau wakibeba mabango makubwa wakitaka teknolojia ya kisasa itumike kusaidia Marefa hasa kwenye uamuzi wa mpira umevuka mstari wa goli au la.
Mechi za Jumapili Juni 27 ndizo zimeleta mjadala mkubwa kuhusu kutumika kwa teknolojia kwenye mechi baada ya England kunyimwa bao la wazi la kusawazisha wakati mechi ikiwa 2-1 wakati mpira uko ndani ‘maili moja’ nzima na hatimaye wakatandikwa 4-1 na Ujerumani.
Nao Mexico walifungwa bao la kwanza kwenye kipigo cha 3-1 toka kwa Argentina wakati kila Mtu alimwona Mfungaji Carlos Tevez yuko ‘maili moja’ ofsaidi.
Katika kikao cha kawaida cha kila siku cha FIFA na Wanahabari kinachofanyika huko Afrika Kusini huku Kombe la Dunia likiendelea, Msemaji wa FIFA Nicolas Maingot alikataa kujibu lolote kuhusu makosa ya Marefa kwa kudai si wakati muafaka kuongelea hilo wala ubora wa kutumia teknolojia ya kisasa kusaidia Marefa.
Rais wa FIFA Sepp Blatter amekuwa mpinzani mkubwa wa teknolojia kusaidia Marefa.

No comments:

Powered By Blogger