Tuesday, 29 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Keane awaponda Wachezaji England
Roy Keane amewaponda Wachezaji wa England kwa kucheza vibaya hasa kwenye mechi na Germany waliyobamizwa 4-1 huko Afrika Kusini na kutupwa nja ya Kombe la Dunia hapo juzi.
Keane, aliekuwa Nahodha wa Manchester United na Mchezaji wa Kimataifa wa Ireland ambe sasa ni Meneja wa Ipswich Town, alimsifia Wayne Rooney pekee na kuwaponda wengine.
Keane alisema: “Tizama Makipa David James ameshushwa Daraja na Portsmouth na Robert Green alipona kushushwa na West Ham! Glen Johnson alicheza vizuri na Liverpool lakini Msimu wao ulikuwa mbovu! John Terry? Alikuwa na ishu nyingi na sidhani kama alikuwa na Msimu mzuri na Chelsea walichukua Ubingwa na FA Cup lakini si kwa sababu yake ni sababu ya Wachezaji wengine wazuri waliokuwa wakishambulia!”
Keane aliongeza: “Mathew Upson hakuwa na Msimu mzuri na West Ham. Ashley Cole ndio kwanza amerudi Uwanjani akitokea majeruhi! James Milner alicheza vizuri lakini Gareth Barry alikuwa wastani huko Man City! Emile Heskey amecheza na England lakini amefunga bao 3 tu akiwa na Aston Villa kwenye Ligi Kuu!”
Blatter aomba radhi kwa kukataliwa Mabao!
Rais wa FIFA, Sepp Blatter, ameomba radhi kwa matukio mawili kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambayo mabao mawili yalifungwa na moja likakataliwa na jingine kukubaliwa.
Bao safi la England, huku mabao yakiwa 2-1 katika mechi na Germany ambayo baadae England walifungwa 4-1, halikuonwa na Refa.
Katika mechi kati ya Argentina na Mexico, Carlos Tevez aliifungia Argentina bao la kwanza huku akiwa ofsaidi na Wachezaji wa Mexico walimzonga Refa na kumtaka aangalie marudio ya tukio hilo lililokuwa likionyeshwa kwenye Bigi Skrini hapo Uwanjani.
Blatter amesema watakutana na IFAB, International FA Board, ambayo ndiyo yenye majukumu ya kubadilisha sheria za Soka.
Blatter ametamka: “Ni wazi itakuwa upuuzi ikiwa matukio hayo kwenye Kombe la Dunia yataachwa bila kufungua mjadala wa kutumia teknoloji ya kisasa golini.”
Blatter amesema ameongea na Viongozi wa Soka toka England na Mexico na kuwaomba radhi.
FIFA imekuwa na msimamo wa kupinga matumizi ya kutumia teknlojia ya kisasa kusaidia Marefa katika maamuzi yao na kauli hii ya FIFA inaelekea kulainisha msimamo huo.
Barca yathibitisha kuwaacha Toure na Henry
FC Barcelona imethibitisha kuwa Wachezaji Thierry Henry na Yaya Toure wataondoka klabu hiyo.
Wakati Henry anasemekana ataelekea Marekani kucheza MLS [Major League Soccer], Yaya Toure yuko mbioni kujiunga na Manchester City, Timu ya ndugu yake Kolo Toure.
Hatua hiii ya kuhama Wachezaji hao imethibitishwa na tovuti ya Barca.
Wachezaji wote hao wawili hivi karibuni walikuwa Afrika Kusini wakichezea Nchi zao kwenye Kombe la Dunia, Henry akiwa na Ufaransa na Toure akiwa na Ivory Coast, na zote zilitolewa hatua ya kwanza ya Makundi.

No comments:

Powered By Blogger