Saturday 3 July 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Ghana 1 Uruguay 1
Ghana nje kwa penalti 4-2
Uruguay imetinga Nusu Fainali ya Kombe la Dunia na itacheza na Holland baada ya kuvunja mioyo ya Ghana na Afrika nzima waliposhinda mechi hii kwa penalti 4-2 baada ya kutoka sare 1-1 dakika 120.
Wachezaji John Mensah na Dominic Adiyiah ndio waliokosa penalti za Ghana.
Lakini nyota mbaya kwa ‘Nyota Nyeusi’ ilionekana pale Asamoah Gyan alipokosa kufunga penalti dakika ya 119 baada ya Luis Suarez kushika mpira kwenye mstari wa goli.
Refa Olegario Benquerenca toka Ureno akampa Kadi Nyekundu Suarez na ndipo Gyan akaachia bunduki toka kwenye penalti na mpira kugonga mwamba wa juu na kutoka nje.
Hilo lilikuwa pigo kubwa.
Awali Sulley Muntari aliipatia bao Ghana dakika ya 45 kwa shuti la Mita 35 na Diego Forlan wa Uruguay akasawazisha dakika ya 55 kwa frikiki.
Capello kubaki Kocha England
FA ya England imethibitisha kuwa Kocha Fabio Capello ataendelea kuwa Kocha wa England na hivyo kufuta ule wasiwasi kuwa atafutwa kazi baada ya England kutupwa nje ya Kombe la Dunia kwa kuchapwa 4-1 na Ujerumani.
Hatua hii inamaanisha Capello atashika hatamu hadi mwishoni mwa Fainali za EURO 2012 ambapo Mkataba wake ndio utakwisha.
Sunderland yamnasa Mmisri
Sunderland imemchukua kwa mkopo wa Mwaka mmoja Mchezaji wa Kimataifa wa Misri Ahmed Al-Muhammadi toka ENPPI.
Al-Muhammadi, Miaka 22, amechezea Misri mara 22 na ikiwa muda wake wa mkopo hapo Sunderland utakuwa wa mafanikio Mchezaji huyo atachukuliwa moja kwa moja.
Habari za kuchotwa Al-Muhammadi zimethibitishwa na Steve Bruce, Meneja wa Sunderland.
Huyu anakuwa Mchezaji wa tatu kuchukuliwa na Sunderland kwa ajili ya Msimu mpya wengine wakiwa ni Cristian Riveros na Simon Mignolet, Kipa kutoka Ubelgiji.

No comments:

Powered By Blogger