Saturday 24 January 2009

Man U watinga Raundi ya 5 FA Cup: Man U 2 Tottenham 1

Ndani ya Uwanja wao Old Trafford, Manchester United wamewabwaga wapinzani wao watakaokutana nao kwenye Fainali ya Carling Cup Machi 1, 2009, Tottenham, kwa mabao 2-1 na hivyo kuwatoa kwenye Kombe la FA.
Magoli yote yalifungwa katika kipindi cha kwanza huku Tottenham wakitangulia kufunga dakika ya 5 tu kupitia Mrusi Roman Pavyluchenko kufuatia krosi ya Tom Hudllestone.
Man U wakafunga bao mbili za haraka ndani ya dakika moja kupitia Paul Scholes dakika ya 35 na Dimitar Berbatov dakika ya 36.
Kivutio kwenye mechi hii ni Sir Alex Ferguson, Meneja wa Manchester United, kuamua kumchezesha kwa mara ya kwanza pacha mwenza wa Rafael aitwae Fabio kama Beki wa pembeni kushoto na kabla ya kuumia alicheza vizuri sana na kushangiliwa sana na Watazamaji.
Rafael na Fabio da Silva ni vijana wa miaka 18 wanaotoka Brazil.
Rafael huwa anacheza Beki wa pembeni kulia.
Man Utd: Foster, O'Shea, Neville, Vidic, Fabio Da Silva (Eckersley 53), Welbeck (Fletcher 86), Carrick, Scholes, Ronaldo (Tosic 72), Berbatov, Tevez.
Akiba hawakucheza: Kuszczak, Giggs, Possebon, Chester.
Kadi: Vidic, Tevez.
Magoli: Scholes 35, Berbatov 36.
Tottenham: Alnwick, Gunter, Corluka, Dawson, Assou-Ekotto, Bentley (Defoe 72), Huddlestone, Zokora, Bale (Taarabt 67), Modric (Giovani 46), Pavlyuchenko.

Akiba hawakucheza: Gomes, Gilberto, Rocha, Dervite.
Goli: Pavlyuchenko 5.
Watazamaji: 75,014
Refa: Peter Walton


MECHI ZA JUMAPILI 25 JANUARI 2009 KOMBE LA FA:

Cardiff v Arsenal [saa 10 na nusu jioni]

Liverpool v Everton [saa 1 usiku]
Mabingwa Watetezi Kombe la FA Portsmouth watolewa na Timu ya Daraja la Chini Swansea!!
Aston Villa watoka suluhu na Timu ndogo Doncaster!!!


Mabingwa Watetezi wa FA Cup, Portsmouth, wamekula kipigo mbele ya umati wa Mashabiki wake nyumbani cha mabao 2-0 na Swansea ambao wako Daraja la chini ya LIGI KUU na kuaga mashindano hayo ya Kombe la FA.
Magoli ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Nathon Dyer dakika ya 26 na Jason Scotland dakika ya 45 kwa penalti ndio yaliyowaua Portsmouth.
Nao Aston Villa, wakicheza ugenini nyumbani kwa Doncaster, timu iliyo Daraja la Chini, ilibanwa na kutoka suluhu na sasa mechi itarudiwa nyumbani kwa Aston Villa.
Lakini kwenye dakika ya 87 Aston Villa walinusurika kufungwa baada ya frikiki ya Woods kumshinda Kipa Brad Friedel na kugonga besera.

MATOKEO KAMILI RAUNDI YA 4 KOMBE LA FA:

Hartlepool 0-2 West Ham
Chelsea 3-1 Ipswich
Doncaster 0-0 Aston Villa
Hull City 2-0 Millwall
Kettering 2-4 Fulham
Portsmouth 0-2 Swansea
Sheff United 2-1 Charlton
Sunderland 0-0 Blackburn
Torquay 0-1 Coventry
Watford 4-3 Crystal Palace
West Brom 2-2 Burnley
Wolves 1-2 Middlesbrough

Mechi inayofuata saa 2 na robo usiku: Manchester United v Tottenham
NI WIKIENDI YA KOMBE LA FA!

Wikiendi hii kutakuwa hamna mechi za LIGI KUU England na badala yake Vilabu vya Madaraja mbalimbali vitaingia dimbani kuwania nafasi za kusonga michuano ya Kombe hili.
Ratiba ni kama ifuatavyo:
Jumamosi, 24 Januari 2009 Mechi za Kombe la FA [mechi zote saa 12 jioni saa za bongo isipokuwa zilizotajwa]
Chelsea v Ipswich
Doncaster v Aston Villa
Hartlepool v West Ham [saa 9 dak 40]
Hull v Millwall
Kettering v Fulham
Man U v Tottenham [saa 2 na robo usiku]
Portsmouth v Swansea
Sheffield United v Charlton
Sunderland v Blackburn
Torquay v Coventry Watford v Crystal Palace
West Brom v Burnley
Wolverhampton v Middlesbrough
Jumapili, 25 Januari 2009 Mechi za Kombe la FA
Cardiff v Arsenal [saa 10 na nusu jioni]
Liverpool v Everton [saa 1 usiku]

Villa wamnunua Emile Heskey kutoka Wigan, Mido aenda Wigan kwa mkopo!

Aston Villa wamemsaini Emile Heskey kutoka Wigan kwa dau la Pauni Milioni 3.5 na wakati huohuo Mchezaji wa Kimataifa wa Misri Mido amechukuliwa na Wigan kwa mkopo kutoka Middlesbrough hadi mwisho mwa msimu huu.
Msimu huu Mido amefunga mabao manne katika mechi 13 alizochezea Middlesbrough.
Mido anakuwa Mshambuliaji wa pili kutua Wigan kufuatia kusainiwa kwa Hugo Rodallega kutoka Colombia kwa ada ya Pauni Milioni 4.5.

Thursday 22 January 2009

UHONDO WA LIGI KUU England: Msimu huu hautabiriki!!!

Wakati duru ya kwanza ya Ligi hii yenye jumla ya Timu 20 imeshamalizika, hakuna hata shabiki mmoja anaeweza kubashiri nani ataibuka Bingwa na Timu zipi 3 zitaporomoka daraja!
Mpaka sasa kitu kilichoibuka na kuwa dhahiri kabisa ni kuonekana kwa matabaka matatu katika msimamo wa Ligi hii.
Tabaka la kwanza ni lile linalojumuisha Klabu Vigogo kama Manchester United, Liverpool, Chelsea na Arsenal huku Aston Villa na pengine Everton wakivamia kundi hilo.
Tabaka hili ni lile la timu zinazoongoza msimamo wa Ligi na kuziacha nyingine zote kwa mbali kidogo.
Mpaka sasa, Man U, ingawa amecheza mechi moja pungufu, anaongoza akiwa na pointi 47 wakiwa sawa na Liverpool alie nyuma kwa sababu ya idadi ndogo ya tofauti ya magoli.
Nafasi ya 3 ni Chelsea wakiwa na pointi 45, wa nne ni Aston Villa pointi 44, wa tano Arsenal pointi 41 na wa sita kwenye kundi hili ni Everton akiwa na pointi 36.
Tabaka la pili lina Timu tatu ambazo ndio hasa zinastahili kuwa hapa na nazo ni Wigan [pointi 31], West Ham [29] na Hull City [27].
Zingine ambazo pengine unaweza kuziingiza hapa ni Fulham, ambao wamecheza mechi 2 pungufu, wakiwa na pointi 26 na hata Man City [pointi 25].
Tabaka la tatu ni zile timu zinazopigania kuzikimbia nafasi za 18, 19 na ya 20 kwenye msimamo wa Ligi kwa sababu hiyo ni 'Denja Zoni', yaani, Timu inayoshika nafasi yeyote kati ya hizo tatu mwisho wa ligi basi inashushwa daraja.
Utamu mkubwa wa Ligi ya msimu huu, mbali ya kutokuwa na fununu hata chembe wa nani anaunusa Ubingwa, upo kwenye tabaka hili lenye Timu 9 zinazogombea kuzikimbia nafasi ya 18, 19 na 20!!
Cha ajabu mno, kati ya Timu hizo 9, ya juu kabisa mpaka sasa iko nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi na iko pointi 3 tu juu ya Timu ambazo kwa sasa zinashikilia nafasi hizo za 'denja' za 18, 19 na 20!
Kingine cha kustaajabisha ni kuwa kwa sasa timu zote 3 zilizo kwenye 'Denja Zoni', yaani Middlesbrough alie nafasi ya 18, Stoke City nafasi ya 19 na wa mwisho kabisa ni West Bromwich Albion kwenye nafasi ya 20, wana pointi sawa kabisa, wote wakiwa na pointi 21 na wametofautishwa tu kwa tofauti ya magoli!!
Timu nyingine zenye pointi 21 pia na wako juu tu ya Timu hizo zilizo mkiani kwa idadi ya magoli tu ni Timu iliyo nafasi ya 17 Blackburn Rovers na Tottenham walio nafasi ya 16.
Juu ya Tottenham zipo Timu 3 nyingine zenye pointi 23 kila moja na hizo ni Sunderland [nafasi ya 15], Newcastle [14] na Bolton [13].
Kwenye nafasi ya 12 yuko Portsmouth mwenye pointi 24.
Hayo ndio maajabu ya LIGI KUU England msimu huu na ni dhahiri hili ndilo linaloifanya Ligi hii kuwa na ushindani, uhondo na kutokutabirika vitu vyote ambavyo vinailetea sifa ya kuwa LIGI BORA DUNIANI tofauti na Ligi nyingi zenye Maskandali ya rushwa na upangaji matokeo!!
Man City wagundua pesa hazinunui mapenzi!!!

Klabu ya Manchester City hivi sasa, polepole, wanaanza kugundua kuwa utajiri haununui mapenzi ya dhati baada ya Klabu hiyo kuwakosa Mchezaji mmoja baada ya mwingine waliomo kwenye Listi ya Wachezaji wanaowawinda!!
Man City ilinunuliwa na Koo tajiri sana ya Kifalme kutoka Abu Dhabi ambayo ni sehemu ya nchi tajiri ya Falme za Nchi za Kiarabu inayojumuisha pia mji wa Dubai.
Ni hivi juzi tu dunia ilistushwa kuskia Staa wa Brazil Kaka anaechezea AC Milan yuko mbioni kujiunga na Man City kwa uhamisho ambao ungekuwa rekodi ya dunia wa Pauni Milioni 100 na pia angelipwa mshahara wa Pauni Laki 500 kwa wiki ambayo pia ingekuwa ni rekodi ya dunia.
Wakati kila mtu akiamini ni mwenda wazimu tu ndie atakaekataa ofa kama hiyo, Kaka aligoma kwenda Man City kwa madai anaipenda AC Milan!
Kufuatia sakata hilo habari nyingi zimeibuka kwamba si Kaka tu aliegoma kwenda Man City ingawa Klabu hiyo ilikuwa inatoa ofa za ajabu!!
Wakati mwingine Man City walikwaa kizingiti cha klabu zilizo na tamaa ya kupindukia na zilizokuwa zikidai zilipwe ada za juu mno kupita kiasi.
Wachezaji walengwa wa Man City walikuwamo Masupastaa David Villa, Kipa Gianluigi Buffon na Thierry Henry.
Mwezi Desemba, msafara kutoka Man City ulitua Valencia ukiwa na kitita cha kuwasaini David Villa na mwenzake wa hapo Klabuni Valencia David Silva.
Kitita hicho kilikuwa ni Pauni Milioni 100 kwa Wachezaji hao wawili!
Valencia wakakaza uzi na kutaka walipwe Pauni Milioni 135 kwa Wachezaji hao wawili.

Mhusika mmoja mkuu kutoka Man City alieshiriki majadiliano ya Wachezaji hao wawili ambayo hayakukamilika anasema: 'Nia yao ilikuwa tuwape mtaji wa kuendesha klabu yao kwa miaka minne!'
Baada ya hapo msafara huo uliojaa 'vijisenti' wa Man City ukatua Turin kufungua majadiliano juu ya uhamisho wa Kipa wa Italia Gianluigi Buffon anaedakia Juventus.
Juventus wakata walipwe Pauni Milioni 100 kwa kipa huyo 'anaezeeka'!!
Msafara wa Man City ukapanda ndege kurudi Manchester huku mmoja wao akilalamika: 'Sisi sio wajinga! Tumeshindwa kukamilisha uhamisho wa Wachezaji hao watatu kwa sababu klabu zao zinadhani tuna pesa za kutupa tu! Na hata Wachezaji wenyewe wamekuwa wakitaka walipwe vitu visivyowezekana! Nadhani kuna dhana potofu sisi ni matajiri mno na tuna uwezo wa kumnunua Mchezaji kwa bei yeyote!'
Ingawa majadiliano yaliyomhusu Thierry Henry yalifika hatua nzuri lakini mwishoni yalipiga chini pale Henry alipokataa kwenda Man City!!
Baadhi ya wadau wanahisi Man City inakosa mvuto na wengi wanaitazama Klabu hiyo kama Klabu duni ukilinganisha na nyingine za LIGI KUU England kama Vigogo Man U, Arsenal, Chelsea na Liverpool.
Wadau hao wanaamini bila kusita kuwa endapo 'vijisenti' hivyo vingekuwa mikononi mwa Vigogo hao, bila shaka na bila kusita, Kaka, Villa, Silva na wengine wengi walio Nyota wasingefikiria mara mbili kujiunga!
Bila shaka, mapenzi ya dhati huenda yanapatikana pasipo ndururu!!


De Jong ajiunga Man City

Mchezaji Kiungo wa Kimataifa wa Uholanzi anaechezea Hamburg ya Ujerumani, Nigel de Jong, amejiunga Manchester City kwa mkataba wa miaka minne na nusu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa na kipengele kwenye mkataba wake na Hamburg kuwa anaweza kuihama Klabu hiyo mwisho mwa msimu huu kwa Pauni Milioni 1 Laki 8 tu lakini inaaminika Man City imelipa Pauni Milioni 18 kumnunua kwa sasa ikiwa ni miezi minne tu kabla msimu haujaisha!
De Jong amechezea mechi 66 hapo Hamburg tangu ahamia akitoka Ajax mwaka 2006 uhamisho ambao uligharimu Pauni Milioni 1 Laki 2 tu.
Katika dirisha hili la uhamisho la Januari, Man City wamewanunua Wayne Bridge kutoka Chelsea na Craig Bellamy kutoka West Ham.
Man City kwa sasa wako nafasi ya 11 kwenye msimamo wa LIGI KUU England wakiwa pointi 4 toka kwenye zile timu zilizo nafasi ya kuporomoka daraja
.
Tottenham chupuchupu kuikosa Fainali Carling Cup, wafungwa ila wamo!!!

Klabu ya Tottenham iliyo LIGI KUU England jana ilifungwa na Timu ya Darala la chini, Burnley, kwa mabao 3-2 lakini ilisonga mbele na kuingia Fainali ya Kombe la Carling kwa vile walishinda mechi ya kwanza waliyochezea kwao White Hart Lane kwa mabao 4-1.
Na laiti ingekuwa ile sheria ya mabao ya ugenini kuhesabiwa mawili endapo timu zinakuwa sawa kwa mabao mwisho wa mchezo basi Tottenham angekuwa marehemu kwani hadi mwisho wa gemu hiyo Burnley alikuwa kashinda 3-0 na hivyo kufanya jumla ya magoli kuwa 4-4 kwa mechi mbili.
Bahati mbaya kwa Burnley na nzuri kwa Tottenham ni kwamba sheria hiyo kwenye Kombe hili inatumika baada ya dakika 120!
Hivyo mpaka dakika 90 kwisha, ingawa Burnley alikuwa mbele 3-0 mechi iliongezwa nusu saa ya nyongeza na laiti matokeo yangekuwa hayo hayo 3-0 hadi mwisho Burnley angeingia Fainali.
Lakini katika hiyo nusu saa ya nyongeza Tottenham walipachika mabao 2 na kufanya mechi kuisha Burnley mshindi 3-2 lakini imetolewa kwa jumla ya magoli 6-4!
Sasa, Tottenham ambae ndie Bingwa mtetezi wa Kombe la Carling atapambana Fainali na Manchester United hapo tarehe 1 Machi 2009.

Abramovich alishitaki gazeti la Sunday Times!!!

Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich, amelishitaki gazeti la Uingereza Sunday Times na kudai fidia baada ya gazeti hilo kuandika kwamba tajiri huyo anataka kuiuza klabu yake hiyo.
Katika makala yake ya uchumi, gazeti hilo lilidai Abramovich yumo mbioni kuiuza klabu hiyo kwa Waarabu wa Ghuba au Koo ya Kifalme ya Saudi Arabia.
Mbali ya kudai fidia, Abramovich anataka mahakama ilizuie gazeti hilo kurudia madai hayo.

Wachezaji wa Newcastle watwangana makonde mazoezini!!!

Meneja wa Newcastle Joe Kinnear amesema hatochukua hatua zozote dhidi ya Wachezaji Charles N'Zogbia na Andy Carrol waliochapana makonde mazoezini juzi siku ya Jumanne.
Wachezaji hao walionyesheana ubabe na ilibidi waamuliwe mara kadhaa baada ya kuchezeana rafu mazoezini.
Ugomvi huo umekuja muda usiozidi wiki tangu Newcastle abamizwe 3-0 na Blackburn na kwenye mechi hiyo Watazamaji waliwashuhudia Wachezaji wa Newcastle Joey Barton na Jose Enrique wakibatukiana kwa hasira uwanjani huku mechi ikiendelea.
Newcastle ipo kwenye hali tata na hata Meneja mwenyewe Joe Kinnear ana kesi 3 za kujibu kwenye Kamati ya FA baada ya kushitakiwa kwa kukosa nidhamu kuhusiana na matukio mbalimbali yanayomhusu kwenye mechi za Newcastle.
Mpaka sasa Newcastle inasuasua nafasi ya 14 kwenye msimamo wa LIGI KUU England wakiwa pointi 2 tu juu ya timu zilizo kwenye ile n'ngwe hatari ya kushushwa daraja.

Wednesday 21 January 2009

Man U waingia FAINALI KOMBE LA CARLING!
-Wachezaji wao Evans, Anderson na Rafael waumia!
-Mdhamini wao AIG kutoongeza tena mkataba 2010!

Mabingwa wa England, Ulaya na Dunia, Manchester United, wamefuzu kuingia Fainali ya Kombe la Carling baada ya kuifunga Derby County mabao 4-2 huko Old Trafford na hivyo kuwatoa kwa jumla ya mabao 4-3 kwani Derby walishinda mechi ya kwanza kwa bao 1-0.
Man U wakicheza na Wachezaji wengi chipukizi walifunga mabao yao kupitia kwa Nani, dakika ya 16, O'Shea [22], Tevez [34] na Ronaldo alieingizwa kipindi cha pili [penalti dakika ya 89].
Wafungaji wa Derby ni Barnes [80] na kwa penalti [90].
Leo inachezwa Nusu Fainali nyingine kati ya Burnley na Tottenham huku Tottenham wakiwa washindi wa mechi ya kwanza kwa mabao 4-1 na mshindi kati ya timu hizi atakutana na Man U Fainali hapo tarehe 1 Machi 2009.
Ushindi huo wa Man U umekuja kwa gharama kubwa kwani Wachezaji wao Johnny Evans, Anderson na Rafael waliumizwa na huenda wakakosekana kwa wiki kadhaa.
Wakati huohuo, Wadhamini wa Man U, Kampuni kubwa ya Bima AIG ambayo maandishi yake 'AIG' huonekana kifuani mwa jezi za Man U wametangaza hawataongeza mkataba wao hapo utakapoisha mwaka 2010.
AIG ni moja ya Makampuni makubwa huko Marekani yaliyokumbwa na hali mbaya ya uchumi na ilibidi Serikali ya Marekani iingilie na kuwapa mtaji ili wasifilisike.

Portsmouth wamsaini Pennant kwa mkopo

Portsmouth wamemchukua Winga wa Liverpool Jermaine Pennant kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.
Pennant msimu huu hana namba Liverpool na ameweza kucheza mechi 4 tu tangu msimu uanze.


Robinho atimka kambini, ajitetea matatizo ya kifamilia yamemsibu!!

Mara tu baada ya kujulikana Manchester City wameshindwa kumchukua nyota wa Brazil Kaka kutoka AC Milan baada ya nyota huyo kugoma kuhamia huko, nyota mwingine wa Brazil, Robinho, ambae alikuwa kwenye kikosi cha Man City kilichokuwa kambini nchini Spain kikifanya mazoezi huko kwa sababu wikiendi hii timu hiyo haina mechi kwa vile zinachezwa mechi za Kombe la FA tu na wao wameshatolewa, mchezaji huyo alikimbia kambini na kuelekea kwao Brazil.
Robinho amejitetea hakuondoka kambini kwa hasira kwa Klabu hiyo kumkosa Kaka bali ni kwa sababu ya matatizo ya kifamilia.
Robinho anaetimiza miaka 25 hapo Januari 25 inasadikiwa alikwaruzana na Meneja Mark Hughes kabla ya kutimka.

Palacios atua Tottenham!

Kiungo kutoka Honduras, Wilson Palacios anaechezea Wigan, amenunuliwa na Tottenham kwa dau la Pauni Milioni 12.
Palacios alijiunga na Wigan Januari 2008 kwa dau kiduchu la Pauni Milioni 1 tu!

Middlesbrough matatani na FA!!
Mameneja wa Newcastle na Hull City pia kizimbani FA!!

Klabu ya Middlesbrough inatakiwa ijibu mashtaka na FA, Chama cha Soka England, kwa kosa la utovu wa nidhamu wa Wachezaji wake waliouonyesha kwa Refa Mark Hasey walipocheza na West Bromwich na kufungwa 3-0 mara tu baada ya mwenzao Didier Digard kulambwa Kadi Nyekundu kwa rafu mbaya dhidi ya Borja Valero.
Wachezaji kadhaa wa Middlesbrough walimzonga Refa huyo na kusababisha adondoshe moja ya Kadi zake.
Middlesbrough wamepewa mpaka tarehe 4 Februari 2009 kuwasilisha utetezi.
Wakati huohuo, Mameneja wa Newcastle Joe Kinnear na Phil Brown wa Hull City pia wameshtakiwa na FA kwa utovu wa nidhamu baada ya wao kukwaruzana pembeni mwa uwanja huku timu zao zikicheza mechi ya marudiano ya kuwania Kombe la FA hapo Januari 14 na ikabidi Refa Phil Dowd aingiilie na kuwatoa nje ya uwanja wote wawili.
Msuguano wao ulitokea pale Fabio Coloccini wa Newcastle alipomchezea rafu Daniel Cousin wa Hull.
Hii ni mara ya 3 kwa Joe Kinnear kushtakiwa na FA tangu achukue madaraka Septemba 2008 hapo Newcastle.
Kinnear na Brown wamepewa hadi Februari 3, 2009 kuwasilisha utetezi.

Tuesday 20 January 2009

TAKWIMU za LIGI KUU England: 5 BORA!

-WAFUNGAJI BORA:

Nikolas Anelka [Chesea] Magoli 14
Robinho [Man City] 11
Amr Zaki [Wigan] 10
Gabriel Agbonlahor [Aston Villa] 9
Frank Lampard [Chelsea] 9
Adebayor 8 [Pamoja na Cisse, Crouch, Defoe, Gerrard, Owen, Ronaldo na Van Persie]

-KADI NYEKUNDU:

Benot Assou-Ekotto [Tottenham] 2
Richard Dunne [Man City] 2
John Terry [Chelsea] 2
Adebayor [Arsenal] 1
Gareth Bale [Tottenham] 1

-KADI NJANO:

Marouane Fellaini [Everton] 10
Wilson Palacios [Wigan] 9
Lee Cattermole [Wigan] 8
Kevin Nolan [Bolton] 8
Alvaro Arbeloa [Liverpool] 7 [Pamoja na Ian Ashbee, Ricardo Fuller, Gavin McCann na Kieran Richardson]

-RAFU NYINGI:
Marouane Fellaini [Everton] 67
Kevin Davies [Bolton] 57
Carlton Cole [West Ham] 50
Bobby Zamora [Fulham] 47
Papa Bouba Diop [Portsmouth] 46


MECHI ZA KUANZIA WIKI HII MPAKA MWISHO WA MWEZI:

Leo na kesho usiku ni siku ambayo mechi za marudiano za Nusu Fainali za kugombea Kombe la Carling zitachezwa.
Hapo awali, wiki 2 zilizopita, Tottenham ilicheza nyumbani na Burnley na kushinda 4-1 na kesho watarudiana uwanjani kwa Burnley.
Derby County wakicheza kwao waliifunga Manchester United bao 1-0 katika Nusu Fainali nyingine na timu hizi zinarudiana leo usiku huko Old Trafford nyumbani kwa Man U.
Washindi wa Nusu Fainali hizo watakutana Fainali tarehe 1 Machi 2009.

Wikiendi hii kutakuwa hamna mechi za LIGI KUU na badala yake zinachezwa mechi za Raundi ya 4 ya Kombe la FA.

LIGI KUU England itarudi tena dimbani kuanzia tarehe 27 Januari 2009.

RATIBA KAMILI: [saa ni za kibongo]

NUSU FAINALI CARLING CUP: Mechi za marudiano

20 Januari 2009 [saa 5 usiku bongo taimu] Manchester United v Derby County
Mechi ya kwanza Derby 1 Manchester United 0

21 Januari 2009 [saa 4 dak 45 usiku bongo taimu] Burnley v Tottenham
Mechi ya kwanza Tottenham 4 Burnley 1

Fainali itachezwa Wembley Stadium tarehe 1 Machi 2009.

Jumamosi, 24 Januari 2009
Mechi za Kombe la FA [mechi zote saa 12 jioni isipokuwa zilizotajwa]

Chelsea v Ipswich
Cheltenham au Doncaster v Aston Villa
Hartlepool v West Ham [saa 9 dak 40]
Hull v Millwall
Kettering v Fulham
Man U v Tottenham [saa 2 na robo usiku]
Portsmouth v Swansea
Sheffield United v Charlton
Sunderland v Blackburn
Torquay v Coventry
Watford v Crystal Palace
West Brom v Burnley
Wolverhampton v Middlesbrough

Jumapili, 25 Januari 2009
Mechi za Kombe la FA

Cardiff v Arsenal [saa 10 na nusu jioni]
Liverpool v Everton [saa 1 usiku]

Jumanne, 27 Januari 2009
Mechi za LIGI KUU England

[saa 4 dak 45 usiku]
Sunderland v Fulham
West Brom v Man U

[saa 5 usiku]
Portsmouth v Aston Villa
Tottenham v Stoke

Jumatano, 28 Januari 2009
[saa 4 dak 45 usiku]

Chelsea v Middlesbrough
Man City v Newcastle
Wigan v Liverpool

[saa 5 usiku]
Blackburn v Bolton
Everton v Arsenal
West Ham v Hull

Jumapili, 31 Januari 2009
[saa 9 dak 45 mchana]

Stoke v Man City

[saa 12 jioni]
Arsenal v West Ham
Aston Villa v Wigan
Bolton v Tottenham
Fulham v Portsmouth
Hull v West Brom
Middlesbrough v Blackburn

Jumapili, 1 Februari 2009
[saa 10 na nusu jioni]

Newcastle v Sunderland

[saa 1 usiku]
Liverpool v Chelsea

Jumatatu, 2 Februari 2009

[saa 5 usiku]
Man U v Everton


Liverpool wakabwa, washindwa kutwaa uongozi LIGI KUU!!!

Watani wa jadi, watoto wa mjini Liverpool, Timu za Liverpool na Everton, jana usiku uwanjani Anfield zilitoka suluhu kwa kufungana bao 1-1 na hivyo kuifanya Liverpool iwe pointi sawa na Mabingwa Manchester United lakini Man U anaongoza kwa kuwa na tofauti ya magoli bora kuliko Liverpool ambao, hata hivyo, wamecheza mechi moja zaidi ya Manchester United.
Baada ya kwenda mapumziko wakiwa hawajafungana, Liverpool walipata bao lao kupitia Nahodha Steve Gerrard aliefumua shuti la mbali dakika ya 68.
Zikiwa zimesalia dakika 3 mechi kwisha frikiki ya Mikel Arteta ilimaliziwa kifundi na Tim Cahill kwa kichwa na kuisawazishia Everton.
Timu hizi zitakutana tena Jumapili kwenye uwanja huohuo wa Anfield safari hii kwenye mechi ya Raundi ya 4 ya Kombe la FA.
Liverpool: Reina, Carragher, Hyypia, Skrtel, Aurelio, Kuyt, Gerrard, Alonso, Riera (Babel 89), Keane (Benayoun 67), Torres (Leiva Lucas 85).
Akiba hawakucheza: Cavalieri, Dossena, Arbeloa, Mascherano.
Goli: Gerrard 68.
Everton: Howard, Hibbert, Lescott, Jagielka, Baines, Osman, Arteta, Neville, Pienaar, Cahill, Anichebe.
Akiba hawakucheza: Nash, Van der Meyde, Castillo, Rodwell, Jutkiewicz, Gosling, Kissock.
Kadi: Pienaar, Arteta.
Goli: Cahill 87.
Watazamaji: 44,382
Refa: Howard Webb (S Yorkshire).

Kaka agoma kuhamia Man City!!

Sasa dunia haitoshuhudia uhamisho wa bei mbaya katika historia baada ya kuthibitishwa Kaka amekataa kuhama AC Milan na kwenda Manchester City.
Iliripotiwa Kaka atahamia Man City kwa dau la Pauni Milioni 100 ambalo lingemfanya awe Mchezaji alieuzwa kwa bei mbaya kupita yeyote kwenye historia ya soka la kulipwa.
Mpaka sasa rekodi ya Mchezaji alieuzwa bei mbaya inashikiliwa na mauzo ya Zinedine Zidane alieuzwa Julai, 2001 kutoka Juventus kwenda Real Madrid kwa Pauni Milioni 46.
Klabu ya AC Milan ilitoa taarifa rasmi kuwa: KAKA ANABAKI AC MILAN na Silvio Berlusconi, Rais wa Klabu hiyo, alikiambia Kituo cha TV kimoja cha Italia: 'Huo ni mwisho wa hadithi hii! Kaka anabaki na nimefurahi sana!
Katika mechi ya Jumamosi ambayo AC Milan waliifunga Fiorentina bao 1-0 kwenye pambano la SERIE A, Mashabiki walibeba mabango na kuimba kumtaka Kaka asiondoke.

BAADA YA KUMKOSA KAKA, MAN CITY YAMNUNUA CRAIG BELLAMY!!!

Klabu ya Manchester City imemsaini Mshambuliaji Craig Bellamy, umri miaka 29, kutoka West Ham kwa ada ya Pauni Milioni 14.
Bellamy alijiunga West Ham kwa Pauni Milioni 7.5 msimu uliokwisha na mpaka sasa ameshawahi kuchezea Klabu za Norwich, Coventry, Newcastle, Celtic, Blackburn na Liverpool.

Sunday 18 January 2009

Tottenham 1 Portsmouth 1

Hii ni mechi iliyowafanya Meneja wa Tottenham Harry Redknapp na Mchezaji wake Jermaine Defoe kupambana na Klabu yao ya zamani kwa mara ya kwanza tangu waihame muda si mrefu uliopita.
Na alikuwa Defoe alieiokoa Tottenham kufungwa pale aliposawazisha kwa bao la dakika ya 70.
Portsmouth walifunga bao lao dakika ya 59 kupitia David Nugent kwenye dakika ya 59.

MECHI LIGI KUU: LIVERPOOL v EVERTON

LEO JUMATATU 19 JANUARI 2009 SAA 5 USIKU [saa za bongo]

Leo usiku Uwanjani Anfield, Liverpool watawakaribisha jirani zao wakazi wa mji mmoja, mji wa Liverpool, Timu ya Everton ambao ni wapinzani wao wa jadi.
Liverpool, waliocheza mechi 21 za LIGI KUU na wana pointi 46 pointi moja nyuma ya vinara wa ligi hiyo Mabingwa Manchester United waliocheza mechi 21 na kuwa na pointi 47, wanahitaji ushindi ili wachukue tena uongozi wa ligi hiyo baada ya kupitwa na Man U siku ya Jumamosi.
Nao Everton wako nafasi ya 7 na wana pointi 35.
Liverpool watawakaribisha kikosini Xabi Alonso na Fernando Torres ambao wote walikuwa majeruhi na sasa wamepona.
Everton watamkosa Kiungo Marouane Fellaini ambae amefungiwa kwa kuwa na Kadi pamoja na majeruhi wa muda mrefu James Vaughan, Aiyegbeni Yakubu, Louis Saha, Nuno na Joseph Yobo.

TIMU ZITATOKANA NA:

Liverpool: Reina, Carragher, Arbeloa, Agger, Hyypia, Skrtel, Aurelio, Alonso, Benayoun, Lucas, Mascherano, Gerrard, Babel, Keane, Kuyt, Torres, Riera, Ngog, El Zhar, Cavalieri.

Everton: Howard, Hibbert, Baines, Jagielka, Lescott, Neville, Arteta, Pienaar, Castillo, Cahill, Anichebe, Nash, Van der Meyde, Rodwell, Gosling, Jutkiewicz, Kissock.

NUSU FAINALI CARLING CUP: Mechi za marudiano

20 Januari 2009 [saa 5 usiku bongo taimu] Manchester United v Derby County

Mechi ya kwanza Derby 1 Manchester United 0

21 Januari 2009 [saa 4 dak 45 usiku bongo taimu] Burnley v Tottenham

Mechi ya kwanza Tottenham 4 Burnley 1

Fainali itachezwa Wembley Stadium tarehe 1 Machi 2009.

Baba yake Dodi, Al-Fayed, aitaka FA kudhibiti viwango vya madau ya uhamisho na mishahara ya Wachezaji!!!

Baada ya kuibuka stori za uhamisho wa Kaka kutoka AC Milan kwenda Manchester City timu inayomilikiwa na Koo ya Kifalme tajiri sana ya huko Abu Dhabi, Falme ya Nchi za Kiaarabu, Mohamed Al-Fayed, ambae ni Mmisri mmiliki wa Klabu ya Fulham na pia ni Baba Mzazi wa Dodi aliekufa kwenye ajali ya gari pamoja na Princess Diana huko Paris mwaka 1997, amewataka viongozi wa LIGI KUU England na FA kudhibiti madau ya uhamisho Wachezaji pamoja na mishahara yao.
Inaaminika Kaka anaweza kuhama AC Milan kwa dau la Pauni Milioni 100 na atapewa mshahara wa Pauni Laki 5 kwa wiki zote zikiwa ni rekodi za dunia.
Mohamed Al-Fayed alitamka: 'Ni wenda wazimu! Hilo dau ni Mchezaji mmoja tu, je wengine kwenye timu hiyo? Ni habari mbaya kwa soka, lakini Viongozi LIGI KUU na FA wana uwezo kudhibiti haya! Mimi silipi zaidi ya Pauni Milioni 15 kwa Mchezaji! Kuna vyuo vizuri kwenye klabu nyingi vinavyo kuza vipaji vya watoto na vijana na hiyo ndio njia bora kuliko kulipa Mamilioni!'
Mchezaji alienunuliwa kwa bei mbaya na timu ya Al-Fayed Fulham ni Steve Marlet mwaka 2001 kwa Pauni Milioni 11.


WACHEZAJI WALIOVUNJA REKODI YA KUNUNULIWA BEI MBAYA:

-Pauni Milioni 46 Zinedine Zidane (Juventus - Real Madrid)

-Pauni Milioni 37 Luis Figo (Barcelona - Real Madrid)

-Pauni Milioni 34 Hernan Jorge Crespo (Parma - Lazio)

-Pauni Milioni 33 Gianluigi Buffon (Parma - Juventus)

-Pauni Milioni 32.5 Robinho (Real Madrid - Man City)

-Pauni Milioni31 Christian Vieri (Lazio - Inter Milan)

-Pauni Milioni 30.75 Dimitar Berbatov (Tottenham - Manchester United)

West Ham 3 Fulham 1 huku Bellamy akiwa nje ya uwanja!!

Mshambuliaji wa West Ham Craig Bellamy hakuwepo kwenye kikosi ambacho leo kimeshinda 3-1 dhidi ya Fulham kwenye LIGI KUU mechi iliyoanza saa 10 na nusu bongo taimu.
Inasadikiwa Bellamy jana alisusa mazoezi baada ya West Ham kukataa ombi lake la kuhamia Tottenham waliotoa ofa ya Pauni Milioni 12 kumnunua.
David de Michele aliipatia West Ham bao la kwanza lakini Paul Konchesky alisawazisha kwa shuti kali sana.
Mark Noble aliifungia West Ham bao la pili kwa penalti baada ya Mshambuliaji Carlton Cole
kuchezewa rafu wakati akienda kufunga.
Carlton Cole akawapachikia West Ham bao la 3.


Joe Cole nje ya uwanja msimu wote!!

Mchezaji wa kutumainiwa wa Chelsea, Joe Cole, atalazimika kukaa nje ya uwanja msimu wote uliobaki baada ya kuumia goti kwenye mechi ya Kombe la FA iliyochezwa Jumatano kati ya Chelsea na Southend.
Joe Cole alifanyiwa upasuaji wa goti hilo jana na sasa anaungana na mwenzake wa Chelsea Michael Essien ambae pia aliumia goti na kupasuliwa kwa kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu
.

Joe Kinnear awalaumu Sam Allardyce na Kevin Keagan kwa matatizo ya Newcastle!!

Joe Kinnear, Meneja wa Newcastle, mara baada ya kubandikwa 3-0 kwenye mechi ya LIGI KUU jana na Blakburn Rovers amewarukia Mameneja waliokuwa nyuma yake hapo Newcastle na kuwabebesha zigo la lawama za kuwa na timu mbovu.
Kabla ya Kinnear, Meneja alikuwa Keagan ambae nae alirithi kutoka kwa Sam Allardyce.
Kinnear alilalama: 'Hawa si Wachezaji wangu! Nimewarithi! Tatizo kubwa timu haina Wachezaji wengi na wa maana! Sijui kwa nini Mameneja wa nyuma yangu hawakuona hilo!


UHAMISHO

Dirisha la Uhamisho wa Wachezaji lilifunguliwa tarehe 1 Januari na litafungwa mwisho wa mwezi na wafuatao ni baadhi tu ya Wachezaji waliohama au kuhamia kwenye Vilabu vya LIGI KUU:
-Manucho [Man U kwenda Hull kwa mkopo]
-Javan Vidal [Stoke kwenda Tranmere kwa mkopo]
-Kevin Kilbane [Wigan kwenda Hull kwa ada ambayo haikutajwa]
-Liam Miller [Sunderland – QPR mkopo]
-James Beattie [Sheffield United – Stoke kwa ada haikutajwa]
-Lee Bowyer [West Ham – Birmingham nkopo]
-Jermaine Defoe [Portsmouth – Tottenham ada Pauni Milioni 15]
-Sebastian Puygrenier [Zenit St Petersburg - Bolton mkopo]
-Hameur Bouazza [Fulham – Birmingham mkopo]
-Ritchie De Laet [Stoke – Man U ada haikutajwa]
-Mathew Etherington [West Ham – Stoke Pauni Milioni 2]
-Scott Sinclair [Chelsea – Birmingham mkopo]
-Wayne Bridge [Chelsea – Man City ada haikutajwa]
-Adem Ljajic [Partizan Belgrade – Man U ada haikutajwa]
-Adem Ljajic [Man U – Partizan Belgrade mkopo hadi mwisho wa msimu huu]
-Zoran Tosic [Partizan Belgrade – Man U ada haikutajwa]

MAREFA WA LIGI KUU WANAOONGOZA KWA KADI

1] Mike Riley Mechi 14 Kadi: Nyekundu 3 Njano 61 Wastani: kadi 4.57 kwa mechi
2] Mike Dean Mechi 16 Nyekundu 6 Njano 62 Wastani kadi 4.25
3] Howard Webb Mechi 18 Nyekundu 5 Njano 70 Wastani 4.17
4] Andre Mariner Mechi 14 Nyekundu 4 Njano 54 Wastani 4.14
5] Michael Jones Mechi 5 Nyekundu 2 Njano 17 Wastani 3.8
Powered By Blogger